SueIsmael
JF-Expert Member
- Dec 11, 2013
- 932
- 1,282
Hapo zamani za kale, kale ile ya umilele. Kale iliyozama hata isitambulike ilipoanza wala kuisha. Haswaa ni kale ya zama za enzi na enzi. Hapo kale basi, palikuwa naye neno, asijulikane alipoanza wala alipotoka. Neno alitanda juu ya enzi.
Naye Neno akawa, akaunda, akaumba akaumbika. Hata kale akavuta hatua na tazama Neno akachukua maumbo zaidi na zaidi. Ikawa kila umbo likapewa neno na kila neno likapewa sauti, ilhali si kila umbo lilipata sauti. Tazama sauti ikasikika katika neno, “enyi maumbo enendeni katika enzi mkaendeleze vizazi nami nitakuwa nanyi katika kukamilisha umilele. Albadani, kama ilivyo mchana na usiku, mwanga na giza; nami ni nguvu ya kuumba na kuangamiza, kustawisha na kudhoofisha”
Naam, kila umbo likapewa nguvu ya neno, nguvu ya uumbaji. Na vizazi vikaenea katika enzi kadri kale ilipopiga hatua. Upekee ukatawala kwa kila umbo kadiri ya vizazi vya uumbaji. Naye neno hakusita nguvu, akichukua upekee katika kila umbo na kila kizazi.
Maumbo nayo yakiendeleza uumbaji katika upekee waliamsha utofauti. Naam tofauti zilimea na nguvu ya neno ikatawala kwa viumbe kadha zaidi ya kadhaa. Nguvu ya neno ilijaa katika fikra na katika sauti za viumbe. Na kwa kila sauti ilizaa matokeo ya giza na mwanga, ukuu na unyongefu. Nguvu ya neno ilitumika na maumbo kubadili enzi na hata maumbo yakalewa nguvu ya neno yakijiridhisha nguvu hiyo. Naam tofauti zilishamiri hata vizazi vya maumbo visirithi historia ya mzizi wa uwepo wao.
Vizazi vikamteka neno, vikimtumikisha kwa uuaji na vikamgeuza kuwa silaha za maangamizi, hata enzi akajawa na simanzi na ghadhabu kubwa. Tazama, Neno akatimiza ahadi ya kale, kale ile ya enzi ya umilele. “Enyi Maumbo kumbuka! Tazama! Hii minyororo imenifunga au imewafunga? Je mmeniteka au nyie ndio mmejiteka? Hata sasa bado mwajiona Maumbo na sio Maangamizi? Hebu Tazama, mimi ni Neno, mimi ni alfa na omega, enzi na milele.”