Kisanga

Bin wamakamo

Member
Dec 12, 2021
77
92
KISANGA
________

visa vya bi mkubwa vilipo komaa akaona isiwe tabu akamtoa hamadi wake kipindoni aka tafuta chumba akapanga ,visa avikuwa kwake tu hata kwa baadhi ya vijana wenzake pale mtaani walipokuwa wakiishi, siku moja akafatwa na kijana mwenzake ambaye walishibana kweli kweli kumuomba waishi pamoja naye pia visa vya bi mkubwa alivichoka , maisha ya marafiki hawa wawili yakaanza.

Kisanga kikaanzia hapa!

Mwenye chumba siku moja alipotoka katika pilika pilika zake akamkuta yule rafiki yake yuko na mwanamke kisha akamwambia mwanamke yule alihitaji hifadhi ya siku moja tu kisha kesho asubuhi angeondoka, kwakuwa walishibana kweli kweli hakuwa na chaguo.

Basi mbilinge mbilinge za usiku jamaa mwenye chumba akalala sofani tu kuupisha mtanange ule wa mechi ya ugenini akabaki shabiki bubu, asubuhi kulipo kucha saa 11 akamka na kuondoka zake , ata alipo rudi jioni hali ikawa ile ile yule bidada alikuwepo na rafiki yake sababu azikumuisha

Wiki ya kwanza ikaaisha yule bidada bado yupo dah jamaa mwenye chumba ikambidi alale sasa alipokuwa akifanya kazi , wiki ya pili nayo ikaaisha, yule jamaa aliyekuja kuomba kuishi na rafikiye akamfata lafiki yake na kumwambia kuwa anataka kupanga chumba na yeye hivyo akachukua jiko ambalo lilikuwepo na baadhi ya vitu alivyoona vinafaa wakaondoka na bidada wake hao wakaenda kujipangia zao, huyu mwenye chumba akuisha kumwambia kuwa asimuamini sana yule bidada kwani hamjui hata undani wake alafu anakuwa na ujasiri wa kwenda kukaa naye tena,

Lakini jamaa damu zake na yule binti zilifatana hakujali hakusikia, wenyewe wakawa wanaishi wanacho kura wanajua wenyewe wanacho vaa wanajua wenyewe.

Yule bidada alikuwa ni mtu wa mafia si unajuwa tena watoto waki mafia wanakuwa wanachanganya kila radha ubantu uhindi uarabu umo umo na alitoka huko kuja kuwa tafuta nduguzo alitoroka alikuwa mzuri haswa, akawa na anawasiliana na rafiki yake ambaye aliolewa huku dar es salaam mwishowe akafika na hali aliyotegemea haikuwa akadondokea mikononi mwa mwamba [majina yamehifadhiwa]

Maisha kati ya bidada na yule kijana aliyemuomba mwenzake waishi pamoja yakawa ya kusua sua mno , siku moja yule bidada akaaga kuwa anakwenda vingunguti kuna ndugu yake mmoja amepata kuwasiliana nae yupo uko , akaenda jiii siku zikakatika.

Jamaa siku moja akapokea simu ya yule bidada akamwambia kuwa yuko vingunguti aende kumfata na kwa vile jamaa alikaa mda bila kuonana na yule bidada kimue mue kweli kweli kika mnasa kwenye kolomero akafunga safari na jamaa yake waliokuwa wakiishi katika chumba kimoja huuuuu mpaka vingunguti, sasa wakashuka katika gari wakawa wanawasiliana na yule bidada kuweelekeza mtaa ambao yeye yupo , mtaa ule wakafika mwanzoni kabisa mwamtaa kulichangamka madufu yalipigwa pale hatarii kaswida ziliibwa usipime, hamadi mashekhee wakawa zonga wakasikia wakisema ndo "hawa eeh ? ndo hawa bwana" Jamaa wakachukuliwa na walee mashekhe na vinjunga vyao vidukwi kichwani dakika kazaa wakabadilika utawajua kama wao wakavalishwa kanzu pale za bei mbaya yule mwenye chumba tena ndo mshenga babu harusi ndo rafikiye, bidada anatolewa ndani ndoa ikapita madufu yakakolezwa hapo hatari

Mtu na lafiki yake awakuamini kilichokuwa kikiendelea mihili kama ilipigwa virungu na mgambo aliyetoka mafunzoni, basi baada ya ndoa kupita mtu na mshenga wake waka ahidi watamfata mke wao siku itakayo fata wamepanda garini hakuna hata aliye msemesha mwenzie taarifa zilivyofika kwa mama wa yule mwamba aliyepigwa cha muajara akawaka hatari.

Navyokwambia mpaka leo bado wanaishi pamoja na watoto wamezaa
Kweli katika maisha watu wamebeba hatima zetu kuna watu watakutoa sehemu mmoja na kukupeleka nyingine so be careful mdada mkaka.

ingekutokea wewe ungefanyaje?

#wamakamo
 
Picha limeisha
 
Back
Top Bottom