Suleman Jr
JF-Expert Member
- Jun 28, 2022
- 341
- 526
Habari wana jf,
Kuna mambo wakati mwingine huyaona ya kawaida ila ukifikiria kiundani unagundua kuna majuto ndani yake..
Niliingia kwenye mahusiano na dada mmoja ana duka kkoo tunalingana umri lakini yeye aliolewa na mwanaume umri umeenda sanaa,
Tulianza kama masihara namuuzia bidhaa flani za mchongo, kuna kipindi akawa na upungufu wa wafanyakazi akaniomba niwe namsaidia siku akiwa na oda kubwa mwishowe akanihodhi mazima nkaacha biashara zangu (maduka ya mtaani yalikua vizuri tu) nilizokua nasimamia mwenyewe akasimamia mdogo angu kwa wazo nipige huku nae apige kule tukuze uchumi wa familia baadae, maana mshahara ulikua mzuri sana kipindi hicho kwangu.
Miezi kadhaa baada ya kunikabidhi duka moja akanitongoza nkajikuta nimeingia 18 zake, (ifahamike sikukubali sababu ya pesa zake bali uzuri wake na pesa hakua nazo maana kipindi naingia mimi wafanyakzi walishamfilisi kabaki mweupe maduka ma2 lkn mizigo hakuna) mapenzi yalikua moto moto kweli adi mitaa ya kazi kkoo walijua hilo, akanifosi nimuache mpenzi wangu tuliependana sana nkafanya hivyo (ila sasa ndio mke wangu baada ya kuachana miaka mi3) na alikua na wivu kupindukia, tulikua bize na mapenzi kuliko kazi, akiwashwa asubuhi mnaenda stoo, akiwashwa mchana mnaenda stoo akiwashwa mida ya jioni mnawahi kufunga kabla ya mda wa kawaida tunaenda gheto kwangu... Yaani ilikua ni vurugu tupu ndani ya miaka miwili lkn mimi sikusahau wajibu wangu nilipiga kazi ivoivo, nkamshauri afunge duka moja tukomae na moja akafanya hivyo, mi nawaza kazi ili nitoke kwenye umaskini yeye mda wote ni mapenzi tuuuu, ilipekea adi kufunga biashara zangu kwa kua mdogo angu nilimpa uhuru kama zake akafilisi.
Akanipa moyo tutafungua mengine tu,
Miaka mi3 inaishia hakuna la maana nililofanya zaidi ya kumjengea mama angu nyumba ya vyumba vi2 hapa dar,
Nkaanza harakati za kumkataa haikua kazi ndogo tuligombana sana adi ilifikia kipindi nkamshikia kisu aniache na maisha yangu ajabu akaenda kuwafata wazazi wangu kuwaeleza kilichotokea, niko gheto naskia gari inaingia uani kuchungulia kawabeba mama na baba, nkajiuliza hajui kama yeye ni mke wa mtu tena wa ndoa?
Nkajifungia wakaita weee nkawa kimya wakaondoka,
Tukaja yamaliza mambo yakaendelea,
Nkamtafuta zilipendwa wangu kama zali huyu hapa tukawekana sawa tukaendelea tulipoishia, mke wa mtu kuja kujua ikawa balaa tena tuligombana sana adi siku 2 hatukufungua duka akawa anatukanana na mpenzi wangu sana nae alishaambiwa niko na jimama lakini hakuniacha wakawa wanajibizana wenyewe kwa wenyewe.
Adi sasa hivi niko na huyo mke wangu mwaka wa kumi huu na kazi bado nafanya kwa huyo dada, kuna mambo yalitokea hadi ikwezekana kua hivyo sema siwezi yaweka hapa naeza fungua code maana huyo dada ni mtu maarufu eneo flani au hapa dar na stori zilijulikana sana.
Najutia kwa kua pengine ningekua na maisha mazuri zaidi ya niliyonayo sasa maana alinifanya nkawa napenda sana wanawake + nyota ya kupendwa kwa kua nilikua na kipato nilizalisha wanawake wengi sana ambao sasa hivi kipato nnachopata kinaishia kwenye kutunza baadhi na bado nna familia ya watoto wa4, pengine ningetulia na mke wangu tangu kipindi kile ningeendelea na displing niliyokua nayo ya kuheshimu hela na kufanya maendeleo lkn kupitia uhuru wa kuachiwa duka (tukiwa kwenye mahusiano hadi sasa) kulinifanya niwe na tabia ovu ambayo sikua nayo kabla sijaingia kwenye mahusiano na huyu dada.