Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,800
- 34,189
SIYO KILA MWENDAWAZIMU NI MWENDAWAZIMU !!
Palikua na mfalme na mwendawazimu ambao walikutana makaburini.
Mfalme: imekuaje wewe unaishi makaburi siku zote?! Na hutaki kuondoka mahala hapa? Je huna hata chembe ya akili hata ya
kukuonesha matatizo ya hapo? Ni swali alouliza mfalme baada ya kumuona chizi amejenga kibanda makaburini.
Mwendawazimu: nadhani itakuwa wewe ndiwe hujielewi! Au huna chembe ya akili!!
Mfalme: kwanini unasema hivyo?!
Mwendawazimu: Mimi nimeona hakuna nyumba ya kubaki ila hizi hapa, nikaamua kusogea karibu hapa! Na wewe
Umeona fahari kujenga kasri nyumba lako kubwa la kifahari na kupakimbia mahala hapa, unasahau kama nawe ipo siku utafika hapa, kwanini usipaimarishe?
Kwani hawa hawakua RAIA zako? Kwani hawataki tena kuishi vizuri? Kwani Hawataki kutembelewa tena?! Pamoja na ufalme wako
umeshindwa kuweka waangalizi mahala hapa ambapo kila MTU atarejea? Umejenga kwa gharama nyumba utakayoiacha na kuitupa nyumba utakayoishi milele??!!
Mfalme alibubujikwa na machozi huku akisema sio kila mwendawazimu ni
Mwendawazimu, nimekosaje chembe ya akili Mimi????!
Mfalme akamwambia Mwendawazimu omba utakacho nitakupa,
Mwendawazimu akasema naomba mambo matatu?! Naomba uniongezee umri wangu, naomba unipe ulinzi siku atakaponijia malakul-maut, naomba unihakikishie kuingia peponi.. Mfalme akapiga kelele sana!!
Mwendawazimu akamuuliza. Nani kati yetu Mwendawazimu?!
Mfalme akasema. Mimi, Mimi, Mimi.. Mwendawazimu akamuuliza kwanini akasema yote uliyoyaomba sina uwezo nayo, na nilikuwa
natembea kwa fahari sana nikidhani Nina uwezo kumbe Mimi si lolote si chochote!! Hata Mimi mwenyewe hayo siwezi kujipatia!!!
Basi Mwendawazimu akamwambia yupo anaeweza nae ni MWENYEEZI MUNGU MMOJA MFALME WA KILA KITU, nami na akili zangu zote zimekwisha kumfikiria yeye!! Mwisho:
jifunze kitu hapo.