Kisa cha vijana wa Wales na vifo vya kujitakia ili kutafuta umaarufu...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha vijana wa Wales na vifo vya kujitakia ili kutafuta umaarufu...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 7, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  [​IMG]
  Kizungumkuti cha vijana hawa kujimaliza kimchezo mchezo kiliazishwa na Dale Crole kijana wa umri wa miaka 18 ambaye alijimaliza kwa kujinyonga katika jumba bovu hapo mnamo Januari 5, 2007. Majuma machache baadae katikati ya mwezi wa Februari rafikie ambaye ndiye aliyewapeleka Polisi katika eneo la tukio aitwae David Dilling aliyekuwa na umri wa miaka 19, na yeye alijiua kwa njia hiyo hiyo ya kujinyonga.

  Wiki iliyofuata rafiki yao mwingine aitwae Thomas Davies aliyekuwa na umri wa miaka 20 nae akajinyonga. Miezi miwili baadae kijana mwingine aitwae Alan Price aliyekuwa na umri wa miaka 21 na yeye vile vile kama wenzie akajinyonga. Miezi kadhaa baadae mnamo Juni rafikie wa karibu aitwae Leigh Jenkins aliyekuwa na umri wa miaka 22 na yeye akajinyonga chumbani kwa rafikie. Kama mchezo vile, mwezi Desemba 2007 wakati wa sherehe za Krismas rafikiye na Dale aitwae Liam Clarke aliyekuwa na umri wa miaka 20 na yeye akajinyonga kama wenzie ikiwa zimepita siku mbili baada ya Krismas.

  Mnamo Januari 5, 2008 wakati wa kumbukumbu za kuadhimisha mwaka mmoja tangu Dale Crole ajinyonge, zafikie mwingine aitwae Gareth Morgan aliyekuwa na umri wa miaka 27 nae akajinyonga nyumbani kwao. Mtiririko wa vijana kujinyonga ulioukumba mji wa Bridgend ulioko Wales nchini Uingereza ulianza kuwatisha watu hasa wakazi wa mji huo kwani tangu Dale Crole ajinyonge, na kufuatiwa na wenzie mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2008 ilikuwa imefikia idadi ya vijana 18 ambao wamejinyonga na kuacha simanzi kwa wapendwa wao.

  Baadhi ya wakazi wa mji huo wameelezea hisia zao kuwa mtiririko huo wa vijana kujinyonga sio jambo la kawaida, na limewashitua sana. Kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana zimebainisha kwamba idadi ya watu kujinyonga katika eneo la Wales ni mara mbili ukilinganisha na Uingereza (Wales ni sehemu ya Uingereza ambayo iko chini ya Malkia). Hali ni mbaya zaidi katika mji huo wa Bridgend wenye idadi ya watu wapatao 130,000 na ni mji ambao umetamalaki kwa umasikini ukilinganisha na miji mingine ya Wales. Takwimu zaidi zimebainisha kwamba idadi ya vijana kujiuwa iliongezeka sana mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2008.
  [​IMG]
  Ilikuwa kila inapotokea kijana mmoja kujinyonga inakuja kugundulika taarifa yake ya kumbukumbu aliyoisambaza kwa wenzake kupitia mtandao wa kijamii wwa inteneti maarufu kwa vijana kusambaza taarifa zao na unaowapa fursa ya kuwa na kurasa zao zinazo wawezesha kufunguwa mijadala na kubadilishana uzoefu. Hilo ndilo lilikuwa lengo kuu la waanzilishi wa mtandao huo, lakini siku za karibuni kumeibuka wimbi la vijana katika mji huo wa Bridgend kutumiana salaam za kuagana kabla ya ya kujinyonga.

  Kwa mfano mnamo Januari 15, 2007 Binti mmoja aliyepoteza maisha kwa mtindo huo huo wa kujinyonga aitwae Natasha Randall aliyekuwa na umri wa miaka 17 alituma salaam za kumbukumbu kwenye ukurasa wa mwenzie aliyefariki kwa kujinyonga katika mtandao maarufu wa Bebo akimweleza kuwa atamkumbuka sana, kwa maneno yake mwenyewe aliandika "kwako Clarky, nitakukumbuka sana rafiki yangu, kila wakati kumbuka wakati wetu wa furaha"

  Siku mbili baadae Natasha alijinyonga, na huo ukawa ni mwanzo wa utata mwingine kuhusiana na wimbi hili la vijana wa Ki Welsh kujinyonga. Kwani uliibuka mjadala mingoni mwa madaktari kuwa ni vigumu sana kwa wanawake kujiuwa kwa jinsi alivyojiuwa Natasha, wataalam hao wa tiba walibainisha kuwa mara nyingi wanawake hupendelea kujiuwa kwa kunywa sumu na sio kwa kujinyonga kama alivyofanya Natasha. Hata hivyo siku iliyofuata rafikie Natasha alijaribu kujinyonga nyumbani kwao lakini kwa bahati nzuri akaokolewa na baba yake akiwa tayari ananing'inia kwenye kamba.

  Wiki mbili baadae binti mwingine aitwae Angelina Fuller aliyekuwa na umri wa miaka 18 nae akajinyonga. Idadi hiyo haikuishia hapo kijana mwingine aitwae Nathaniel Pritchard aliyekuwa na umri wa miaka 15 nae akajinyonga hapo mnamo Februari 15, 2007, akifuatiwa kwa masaa machache na kijana mwingine aliyekuwa na umri wa miaka 20 aitwae Kelly Stephenson. Siku nne baadae alifuatia jirani yao aitwae Jenna Parry aliyekuwa na umri wa miaka 16 na yeye akakutwa akiwa amejinyonga juu ya mti nje ya nyumbani kwao.

  Ndugu jamaa na mararfiki walimiminika na kuweka maua na kadi kwenye mti huo aliojinyongea Parry, hata hivyo baadhi ya kadi zilizowekwa ujumbe wake uliwatisha wengi, miongoni mwa kadi hizo iko iliyoandikwa "Niwekee nafasi jirani na wewe" nyingine iliandikwa "uko katika mahali pa usalama zaidi" na nyingine tena ikaandikwa "Tutaonana muda si mrefu, nakupenda sana!" kadi zote hizo hazikuwa zimesainiwa hivyo kuwa vigumu kuwafahamu walioweka kadi hizo pale chini ya ule mti.

  Baadhi ya wananchi nchini humo walianza kuvilaumu vyombo vya habari na hasa magazeti ya udaku kuwa yanahusika na wimbi hilo la vijana kujinyonga kwani vyombo hivyo vimekuwa vikiandika habari za kujinyonga kwa vijana hao katika hali ya ushabiki kiasi cha kuwapa umaarufu wale waliojinyonga. Akiongea na waandishi wa habari msemaji wa Polisi katika mji huo alivilaumu sana vyombo vya habari kwa jinsi walivyoandika habari za kujinyonga kwa Natasha Randall kwa namna ambayo ilichochea vijana wengine kujinyonga ili kujipatia umaarufu hata baada ya kufa. Hata hivyo baadhi ya wakazi wa mji huo waliliangalia jambo hili kwa mkabala tofauti.
  [​IMG]
  Mkazi mmoja wa mji huo wa Bridgend aitwae Tracy Roberts alisema si busara kuvilaumu vyombo vya habari. Aliendelea kuvitetea vyombo vya habari kuwa ndivyo vilivyoonyesha kuwa kuna tatizo la vijana kujinyonga katika mji huo kwa hiyo si vyema kuvitupia lawama. Mama huyo alimpoteza mwanae wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka 19 ambaye alikufa kwa kujinyonga mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka 2006, hata hivyo mama huyo hakuhusisha kifo cha mwanae na mtiririko wa vijana kujinyonga katika mji huo wa Bridgend.

  Naye Profesa mmoja wa Saikolojia katika maswala ya kijamii aitwae Arthur Cassidy ambaye anaendesha mtandao wa kuzuia wimbi la vijana kujinyonga katika mji wa Belfast mtandao uitwao Youth-Suicide Intervention group, naye aliungana na Tracy kuyatetea magazeti ya udaku akisema kuwa vifo hivyo havikuchangiwa na na magazeti ya udaku.

  "Hatuna ushahidi kuwa magazeti ya udaku yameshiriki kwa njia moja au nyingine kuchochea vijana hawa kujinyonga, kwa kawaida vijana wa siku hizi hawasomi magazeti bali hupata habari kupitia mtandao wa inteneti" Alisema Profesa Cassidy. Hata hivyo baadhi ya wataalam wa mambo ya kiuchumi walitafsiri hatua hiyo ya vijana kujimaliza kwa kujinyonga kuwa inatokana na vijana wengi kupoteza matumaini ya maisha baada ya kumaliza masomo kwani mji huo wa Bridgend umezungukwa na umasikini kutokana na kukosekana kwa vyanzo vya ajira hasa kwa vijana wanapomaliza masomo.
  [​IMG]
  Historia inaonyesha kuwa mji huo ulikuwa ni eneo la machimbo ya makaa ya mawe miaka ya nyuma, hivyo baada ya machimbo hayo kufungwa kumekuwa hakuna chanzo kingine cha ajira mbadala na hivyo vijana wengi katika mji huo kujikuta wakiwa na wakati mgumu mara baada yas kumaliza masomo yao, hivyo kujikuta wakitumia muda wao mwingi kwenye mitandao ya inteneti.

  Mtoto mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 14 ambaye wazazi wake waliomba jina lake lihifandhiwe alisema kuwa, Inteneti imekuwa ikiwaandaa vijana hawa kujinyonga katika mji huu wa Bridgend, na hata ukingalia vijana wote hao waliojinyonga walikuwa ni wanachama wa mtandao wa Bebo na walikuwa wakitumiana salaam za kumbukumbu katika ukurasa maalum wa kutuma salaam za kumbukumbu kwa wale waliopoteza wapendwa wao.

  "Naamini vijana hawa walikuwa wanafahamiana, na nimetokea kuwafahamu vijana sita miongoni mwa waliofariki kwani nilishawahi kutembelea kurasa zao kwenye mtandao wa inteneti wa Bebo, na walichokuwa wakikizungumzia sidhani kama nitakuja kujihusisha nacho, na sikudhani kuwa watakuja kutekeleza yale waliyoyaandika"
  alisema kijana huyo aneishi jirani na familia moja iliyopoteza kijana wao kwa mtindo huo huo wa kujinyonga.

  Naye rafikie aitwae George alidai kuwa vijana wengi wanachukulia kujinyonga kama fasheni fulani hivi. Nao Polisi kwa upande wao wanatembelea familia za vijana ambao wametuma taarifa kwenye kurasa zao katika mtandao huo wa Bebo wakiashiria kutaka kujinyonga. Hata hivyo wamiliki wa mtandao huo wamekuwa wakitoa baadhi ya taarifa hizo kutoka kwenye mtandao wao.

  Msemaji wa mtandao huo alisema kuwa wamekuwa wakitoa waraka wowote wa kumbukumbu ya kifo au dalili ya mtumaji kuonyesha kuwa huenda na yeye akajiua, ikiwa tu watakuwa wameombwa na familia ya kijana husika au wameagizwa na mamlaka ya kisheria.

  Wamiliki wa mtandao huo wa Bebo walishirikiana na Polisi katika kuchunguza vifo hivyo. Lakini hata hivyo, hali hiyo haijaukumba mtandao wa Bebo pekee kwani hata mitandao mingine nayo imechukua hatua kadhaa katika kuchunguza wimbi hilo la vijana kujinyonga ili kujua kama linatokana na inteneti.

  Kwa mfano Mtandao maalum wa inteneti wa kutuma salaam za kumbukumbu za vifo uitwao "GoneTooSoon.co.uk" uliondoa kumbukumbu zilizotumwa kwa vijana wote waliojinyonga katika mji huo wa Bridgend na kisha kuweka taarifa ya kuomba radhi na kufafanua sababu ya kuondoa kumbukumbu hizo.

  Mwanzilishi wa mtandao huo Terry George alisema kuwa anataka kuepuka dalili zozote za kuuhusisha mtandao wake na wimbi la vijana wa Ki Welsh kujinyonga.
  "Ikiwa unajinyonga kwa matumaini kuwa utakuwa mtu maarufu hata baada ya kufa basi hiyo haiwezi kutokea kwenye mtandao wetu, hatuwezi kuruhusu jambo hilo litokee, na lazima kufanyike juhudi za kuzuia vijana wetu kujiuwa" alisema Terry George.

   
 2. Triple G

  Triple G JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 745
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  mkuu huwa najaribu kufuatilia post zako kweli ziko kipekee,huwa zina mafundisho ndani yake kabisa.nakupongeza kwa hilo.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hawa vijana walikata tamaa ya maisha ndio maana walikuwa wanajinyonga. Kisa hiki kinasikitisha sana, asante sana Mtambuzi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Hao wamekumbwa na roho ya mauti. Roho ya mauti ikikuandama unakuwa unatamani kufa tu tena ujiue mwenyewe
   
 5. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  ni kukata tamaa ya maisha!so sad though naweza kuimagine wazazi wa hilo eneo walikuwa na hofu ya aina gani kila uchao.lakini hili liwe changamoto kwetu wazazi .DO WE KNOW WHAT OUR KIDS DOING BEFORE THE MONITORS?
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Duu, hayo matukio yanasikitisha kwa kweli hasa ukizingatia kuwa wanajiua wakiwa na umri wa ujana mbichi ambao ndiyo umri wa kushiriki kwenye shughuli za kujenga uchumi wa familia na nchi zao. Sijui walikumbwa na nini, sijui ni mob psychology kupitia internet (Internet suicide)?

  Tukiridi kwenye teknolojia ya internet, hapo ndipo utagundua kuwa pamoja na internet kutupa faida nyingi na kurahisishwa kwa kiasi kikubwa suala zima la mawasiliano, bado pia inatumiwa vibaya na baadhi ya watu. Mifano dhahiri ndiyo hiyo ya hao waliojiua kwa kuiga watu fulani na kuandika ujumbe wa kuaga kana kwamba kwa kufanya hivyo wanatenda kitendo cha kishujaa. Huu ni ukauzu wa hali ya juu kuliko ule wa dagaa!
   
 7. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyu mtu akili zake ni kama nabii huwa kila nikimfikiria huwa anawaza nini sipati jibu,cha kufanya ni kumtakia uhai mrefu tu ili maarifa yake yawafikie watu wengi zaidi.yangu ni hayo tu.
   
 8. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wamefanya kama dini au imani fulani maana ukiwaona watu wanatiana moyo ili kujiua hiyo sio hali ya kawaida kabisa mpaka nahisi ni zaidi ya huo umasikini.
   
 9. LexAid

  LexAid JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 1,950
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hawa lazima kiini cha asili yao wametokea mkoa wa Iringa!
   
 10. p

  pretty n JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera sana kaka MTAMBUZI kwakwel post zako huwa ni za maana sana na pia zinamafundisho mungu akuongezee upeo zaidi
   
 11. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,215
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi umetuelezea jinsi matukio yalivyotokea ila haujatueleza jinsi polisi walivyoshughulikia tatizo hilo na km kuna kesi yoyote ilifunguliwa nahisi km umeikatiza hiki kisa. Nasubilia umalizie kisa hiki ndo nichangie. Asante
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo roho ya umauti inaweza kuwakumba watu wa eneo moja tu?
   
 13. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  So sad,
  Kwakweli hilo ni pepo baya sana.
  Limenikumbusha miaka ya 80s kulitokea wimbi la vijana wanafunzi kujiua hapa bongo na hao sijui walikuwa na matatizo gani.

  Thanks Mtambuzi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  eeMungu tupe mioyo ya nyama na ondoa ya jiwe iliyoko kati yetu.
   
 15. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Huko nako kuna wanyalu?
   
 16. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  Aksante mkuu kazi njemaaaaaaaaaa!!!!!
   
 17. telitaibi

  telitaibi JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nilikuwa nimepotea lakini lo jamani mtambuzi ngumu hii kumeza vijana ni mapepo ya kuzimu yameingia au
   
 18. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Sidhani hata kama ni UMAARUFU ndiyo unawasukuma hadi kujiua!!! Kuna tatizo kubwa zaidi la kisaikolojia katika vichwa vya hao vijana!!!!!!

  Jamii za wenzetu nchi zilizoendelea kuna pressure kubwa sana katika jamii inayowafanya vijana wawe kama MBUZi ISIYOKUWA NA MCHUNGAJI......Kama unaelewa usumbufu wa mbuzi machungoni (hekaheka za vijana na kuamini wanajua kila kitu) sasa wa imagine bila mchungaji!!!!!

  Haina tofauti na upuuzi unaokomaa katika vijana wa kwetu hapa nchini; kuongezeka kwa kasumba mbovu kama ushoga; kutumia madawa ya kulevya kama fashion...nk.....Vyote tutasingizia MITANDAO; UTANDAWAZi. nk lakini TAABU KUBWA IKO NDANI YETU SISI WENYEWE KAMA WANA JAMII!!!!! TUkiweza kuishi kama BINADAMU (tena; maana tuliwahi kuishi hivyo) haya maupuuzi walau yatapungua.....
   
 19. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  inasikitisha, yaani mtiririko wa kujiua hao vijana waliokuwa wanaishi eneo moja lazima uliwaathiri sana wazazi wao na community nzima..
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  mtaa huo kutakua na mapepo yanataka kafara.!
   
Loading...