Kisa cha mwanamke wa ziwani

Mhhh ndefu sana japo nimeisoma yote
Ila swali ambalo halijajibiwa nani alimuua Carol na kwa nini Gordons alijiua

Kama ingekuwa ni movie then tungemkodi Jack Bouer atusaidie in this. It's very complicated kwa kweli...)
 
hiyo issue itkauwa mume anahusika katika mauaji, lakini kuna mtu wa tatu hapo most likely yule aliyefumaniwa nae, lazima hicho kitendo cha kuua kilifanyika mbele yake, wakaweka ugomvi kando wakashirikiana kudispose mwili sasa kwa kuwa mume ameshatumikia kifungo wasiwasi wa mtu wa tatu ni hapo atakapotoka lazima angefanya revenge! ukiangalia channel 252 DisID ya DsTV ndio utajua wazungu wanauana sana! tena si kwa ujambazi ila watu walio na uhusiano wa karibu na kujaribu kupoteza ushahidi lakini huwa wanashikwa hata kama ipite miaka mingapi!!
 
Mkuu Mtambuzi!
Kwanza nikushukuru kwa haka "kauzi" kenye kisa kitamu sana....
Tofauti na wengi, mi kwangu naona imekuwa fupi sana aisee lol
Ndio nimeipitia leo mida ya mchana nilikuwa safarini, matokeo yake vyote vikawa vifupi yaani hii hadithi na safari yenyewe....
Ila naona kila mtu ametoa ubashiri wake juu ya hatma ya hichi kisa, kwa upande wangu nadhani na nahisi bwana Gordon P ndio muuaji wetu na anahusika katika hili sokomoko......
Hiyo kujiua kwake ni vile sasa moyo wake umeshindwa kuvumilia kuwa anadhani soon ataeleza ukweli afu hatoweza tena kuuface ulimwengu wake..... yah ni hisia tu na nadhani ndio zinazowaongoza hao polisi ndio maana wapo biased!
Part iliyonifurahisha zaidi ni pale kwa wale mateja wa jela kila mmoja kutoa ushahidi wake na kusisitiza kuwa walisimuliwa na muhusika wakati muhusika hata hawakumbuki hahahahaha.....
Nawatakia wataalamu wa mikasa kila la kheri kwenye kukamilisha hichi kisa ili ikibidi wengine turudi mapema kumtaka radhi bwana Gordon kwa kumuhisi vibaya.
 
Paragraph ya mwisho ndo jibu lenyewe tungebeba. Labda tuiulize bahari ya hindi imehifadhi vifurushi vingapi hapo chini?

By the way story nzuri inavutia na inamfanya msomaji atake kujua the next line kuna nini. Na mwisho wake umekuwa wa kuruka sana sijui umeifupisha kama member wengine alivyoomba, ila in short "maswali mengi kuliko majibu na kukitegua kitendawili hiki kazi sana."

Hapa kuna nadharia nyingi sana zimezungumzwa kuhusiana na kesi hii, inawezekana ukawa sahihi, kwani bado kuna waandishi wa habari za kiuchunguzi wanendelea kuchimba ili kupata ukweli............... Kama mnavyowajuwa wenzetu, haliwezi kupita jambo likaachwa hivihivi, ni lazima kuna watu watadadisi ili kujiridhisha..................tusubiri.

Kingine ambacho mimi, wewe na wengine huenda tunajiuliza, ni Je iwapo tukio kama hili linatokea hapa nchini, Je Polisi wetu wamejandaa vipi kiuchunguzi, je tunavyo vifaa vya kitekolojia katika kufanya uchunguzi wa kesi za namna hii? Kama inavyojulikana kwamba uchunguzi wa kesi za namna hii zinahitaji fedha tena za kutosha, sasa je tumewawezesha vipi Polisi wetu kumudu kuendesha uchunguzi wa kesi za namna hii? Au yatakuwa ni yale yale ya kusema, "Amejitakia mwenyewe, kwa nini tujisumbue na mtu aliyeuawa miaka 20 iliyopita kwa ujinga wake mwenyewe" nimewaza kwa sauti tu
 
Naikumbuka vizuri hadithi hii na huyo lady on the lake alipotolewa kutoka baharini nilikuwepo UK. Hii story vile vile ilitoka kwenye Forensic detectives.

Kitu ambacho ulisahau kukiandika ni kuwa yule mume wake mara nyingi alikuwa anakwenda kule ziwani 'kutafakari', lakini kwanza hata polisi hawakufahamu link yake na kule ziwani mpaka ilipopatikana hiyo maiti.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom