Kisa cha Mchungaji John Nelson Canning na ajuza wawili…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha Mchungaji John Nelson Canning na ajuza wawili…!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jul 6, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mchungaji John Nelson Canning
  [​IMG]
  Mchungaji Canning na mkewe siku alipowafungisha ndoa Bwana Leo Gleese na Bibi Hazel Gleese katikati
  [​IMG]
  Mchungaji Canning siku ya mazishi ya ajuza hao

  Mnamo January 3, 1995 mchungaji mmoja aitwae John Nelson Canning alikwenda katika kituo cha Polisi cha mji mdogo wa Sebring ulioko katika jimbo la Florida nchini Marekani na kutoa taarifa juu ya mauaji ya vikongwe wawili mtu na mkewe Bwana Leo na bibi Hazel Gleese.

  Mchungaji huyo aliyekuwa na umri wa miaka 59 wakati huo aliwaeleza Polisi kwamba aligundua mauaji hayo baada ya kuwa amewatembelea nyumbani kwao kama ilivyo kawaida yake ya kuwatembelea waumini wake na kukuta miili ya vikongwe hao ikiwa imelala sakafuni kwenye dimbwi la damu.Mchungaji Canning aliendelea kuwaeleza Polisi kwamba bwana na bibi Gleese ni waumini wa siku nyingi katika kanisa la Fountain of life ambalo yeye ni muanzilishi wake.

  Mchungaji huyo alibainisha kwamba katika kipindi cha miaka ya karibuni alikuwa ni muangalizi wa vikongwe hao ambao hawakubahatika kupata watoto katika maisha yao ya ndoa ambapo waliamua kumuasili (Adopt) mchungaji huyo na kumfanya mtoto wao na hivyo akawa anawaita Baba na Mama.
  Mara baada ya kupata taarifa hizo Polisi walikimbilia kwenye eneo la tukio na kukutana na hali ya kutisha katika eneo la tukio ambayo hawatakuja kuisahau.

  Kwani waliukuta mwili wa Bibi Hazel Gleese ambae alikuwa na umri wa miaka 90 wakati huo umelala jikoni ukiwa umetapakaa damu.
  Na mwili wa mumewe Leo Gleese nao pia ulikutwa ukiwa umeegemea ukuta wa chumbani. Wote walikuwa wanaonyesha kwamba walikuwa wamepigwa na kunyongwa. Katika eneo ambalo miili ya ajuza wale ililala polisi wa upelelezi walikuta pia baadhi ya nyaraka za kibenki zikiwa zimesambaa pale sakafuni huku baadhi ya nyaraka hizo zikiwa zimelowa damu, pia kulikuwa na dalili zote kwamba kulikuwa na purukushani za kupigana kati ya bibi Gleese na mtuhumiwa au watuhumiwa wa mauaji.

  Siku ya mazishi ya maajuza hao umati mkubwa wa watu wa mji wa Sebring walihudhuria mazishi hayo na yaliyoongozwa na mchungaji John Nelson Canning.
  Akiongoza mazishi hayo mchungaji Canning, kwa maneno yake mwenyewe alisema "Miongoni mwenu mlikuwa marafiki wa muda mrefu wa baba na mama yangu hawa, lakini ninayo mashaka kwamba hakuna mtu yeyote aliyekuwa karibu na na familia hii zaidi yangu na mke wangu."

  Huku akitokwa na machozi, mchungaji huyo aliendelea kusema "Najivunia familia ya ajuza hawa kuniomba waniasili (Adopt) niwe mtoto wao, na nilijivunia kuwaita baba na mama kama wazazi wangu." Familia ya Gleese haikubahatika kupata watoto katika maisha yao ya ndoa ndio sababu waliamua kuwaasili Canning na mkewe Judy hapo mnamo mwaka 1994.

  Hata hivyo wakati wa mazishi hayo bado Polisi wa upelelezi walianza kumtilia mashaka mchungaji huyo kwa kumhusisha na mauaji ya ajuza wale. Polisi hao wa upelelezi walianza kumtilia mashaka mchungaji Canning tangu siku ile ya kwanza alipokwenda kutoa taarifa ya kutokea kwa mauaji ya ajuza wale ambao aliwachukulia kama wazazi wake.

  Akiandikisha maelezo yake Polisi namna alivyogundua mauaji ya Bi Hazel na bwana Leo Gleese, Canning aliwaeleza Polisi akiwa katika hali ya kawaida kabisa. Kwa maneno yake mwenyewe Canning alisema "kwa kweli niligundua mauaji hayo jana asubuhi." Polisi wa upelelezi walistushwa na habari hizo, kwani kwa mujibu wa maelezo yake ilionyesha kuwa miili ya Hazel na Leo Gleese ilikuwa imelala pale sakafuni kwa masaa 24 tangu kuuwawa pamoja na kuwa mchungaji Canning alifahamu kuhusu kutokea mauaji tangu jana asubuhi.

  Alipoulizwa kwamba kwa nini hakutoa taarifa mapema, mchungaji Canning alidai kwamba aliogopa kutoa taarifa kwa sababu hapakuwa na shahidi mwingine zaidi yake, hivyo aliogopa kuwa mtuhumiwa wa kwanza kuhusishwa na mauaji yale. Kwa maneno yake mwenyewe Canning alsema "Niliingia ndani na kustushwa na mauaji yale, nilichanganyikiwa na kufunga mlango kisha nikaondoka kwani niliogopa kutoa taarifa za vifo hivi kwa kuhofia kwamba nitahusishwa navyo mpaka leo ndio nikakata shauri nije nitoe taarifa."

  Mchungaji Cunning aliendelea kuwaambia polisi wa upelelezi kwamba akiwa ameshikwa na kihoro alishinda kutwa nzima akifikiria jinsi atavyotoa taarifa za vifo vile. Alipoulizwa kwamba siku hiyo ya kihoro aliitumia akiwa wapi, Mchungaji Canning aliwashangaza polisi kwa kuwaambia kuwa alishinda ufukweni mwa Bahari akiwa na marafiki zake na kisha usiku wakaungana pamoja kwenye mghahawa mmoja kwa ajili ya kupata mlo wa usiku.

  Kwa ujumla maelezo ya Mchungaji Canning yalikuwa yanatia mashaka kwani Polisi wa upelelezi walibaki wakijiuliza kuwa, hivi hiyo ndio tabia ya mtu aliyeshuhudia mauaji ya kikatili ya watu ambao aliwafanya kuwa wazazi wake? Kuanzia hapo Polisi wa upelelezi walianza kumuhoji Mchungaji Canning kwa makini zaidi. Msemaji wa Polisi Phil Ramer akizungumza na waandishi wa habari alisema "Kama inamchukuwa mtu siku nzima kutoa taarifa za vifo vya watu wanaomuhusu waliouwawa kikatili, hiyo haiwezi kuwachukuwa wanasayansi wa kutengeneza Roketi kugundua kwamba muuaji ni nani."

  Kwani kwa jinsi Canning anavyojieleza, ndivyo anavyozidi kudhihirisha kwamba kuna jambo analificha kuhusiana na mauaji hayo, alibainisha askari wa upelelezi anaeongoza timu ya wapelelezi wanaochunguza mauaji hayo Sajent Steven Carr. Kwa muda mfupi wapelelezi wa polisi walikuja kugungua kuwa Mchungaji Canning na familia ya Gleese walikuwa na uhusiano wa karibu sana.Historia inaonyesha kuwa awali Mchungaji Canning alikuwa ni Mchungaji wa kanisa moja lilipo katika mji wa Maine lakini baadae akaja akahamia katika mji wa Sebring na kuanzisha kanisa lake mwenyewe aliloliita Fountain of life hapo mnamo mwaka 1980.

  Miongoni mwa waumini wa kanisa hilo kulikuwa na wazee zaidi ya 50 ambao walikuwa ni wafuatiliaji wazuri wa mahubiri ya mchungaji Canning kupitia luninga kabla ya kujiunga na kanisa hilo.
  Hapo ndipo kwa mara ya kwanza ilipotokea Leo Gleese mhasibu mstaafu na mkewe Hazel mwana mitindo wa zamani kujuana na mchungaji Canning. Ni katika kipindi hicho ndipo familia ya Gleese ilipomuasili mchungaji Canning na mkewe na kuwaamini kiasi cha kuwafanya kama watoto wao ambapo kutokana na hali zao kuwa dhaifu kwa sababu ya uzee walimpa mamlaka ya kumiliki akaunti zao na kuwa mshauri wa familia hiyo katika maswala ya kifedha, kosa ambalo lilikuja kuwagharmu maisha yao.

  Pia polisi wa upelelezi walikuja kugundua kwamba mchungaji Canning hakuwa ameaminiwa na familia ya Gleese tu bali pia waumini wengi katika kanisa lake walimuamini na kumfanya mshauri wao wa maswala ya kifedha. Pia wapelelezi hao wa polisi walikuja kushangaa baada ya kugundua kwamba, kwa takribani miaka 15 kanisa la Fountain of life lilikuwa likiendeshwa katika ghala chakavu alilolinunua mara baada ya kuhamia Sebring, na katika kipindi cha miaka kadhaa mchungaji Canning alikuwa kichangisha fedha kwa waumini wake ili ajenge jengo la kisasa la kanisa lake ambalo mwenyewe alisema litakuwa ni la karne.

  Ni katika kipindi hicho ambapo ujenzi wa kanisa hilo ulipoanza ndipo mauaji ya Gleese na mkewe yalipotokea. Polisi wa upelelezi waliona ni vyema wakaanza upelelezi wao kwa kuangalia vyanzo vyake vya mapato pamoja na matumizi. Katika upelelezi wao ndipo walipokuja kugundua kwamba ndani ya wiki moja tangu mchungaji Canning apewe jukumu la kusimamia akaunti za familia ya Gleese ndipo alipolipa deni lake lote la manunuzi ya lile ghala aliloligeuza kuwa kanisa, na baada ya hapo akaanza matumizi makubwa ya fedha kwa kununua nyumba mbili zenye thamani ya dola 83,000, na wakati huo huo alianza upanuzi wa nyumba aliyokuwa akiishi kwa kuifanya kuwa ya kisasa zaidi.


  Kwa muda mfupi akaunti za familia ya Gleese ilikuwa imekauka ikiwemo akaunti yao nyingine ya akiba iliyokuwa na kiasi cha dola 16,000, zilikuwa zimetoweka kusikojulikana. Polisi wa upelelezi walipowahoji marafiki wa familia ya Gleese, walidai kwamba wiki moja kabla ya kuuwawa kwao mke wa Gleese bibi Hazel Gleese alianza kumtilia mashaka mchungaji Canning kuhusiana na namna anavyosimamia fedha zao. Bi Hazel aliwaambia majirani zake kwamba anapanga kwenda katika benki jijini New York alipoweka fedha zao ili kuonana na meneja wa benki ili kupata taarifa ya fedha zao kwa mwaka mzima, lakini ikiwa imebaki siku chache kabla ya bi Hazel kwenda benki wakakutwa waameuwawa na hiyo ilitokea baada ya familia hiyo kugundua kwamba mchungaji Canning alikuwa ameghushi sahihi zao na kujiandikia hundi ambapo alikuwa akijilipa yeye mwenyewe.

  Polisi wa upelelezi waliamua kuhamishia upelelezi wao katika benki hiyo iliyoko katika jiji la New York ambapo walikwenda na zile taarifa za benki (Bank statements) walizozikuta zimesambaa sakafuni baada ya mauaji yale kutokea. Hata hivyo mpaka kufikia hapo, bado polisi walikuwa hawajapata ushahidi wa kina wa kumfungulia mchungaji Canning mashitaka kuhusiana na mauaji ya ajuza wale.

  Msemaji mwingine wa timu hiyo ya upelelezi wa Robert Glick alisema kwamba wanao ushahidi mwingine kutoka kwa raia mwema anaeishi jirani na kanisa la mchungaji Canning ambae alibainisha kwamba siku ile yalipotokea mauaji alimuona mchungaji huyo akienda na kurudi mara kwa mara kwenye shimo la taka lililoko jirani na kanisa hilo ambapo inasemekana kwamba huenda alikuwa anatafuta namna ya kuizika miili ya ajuza wale.Askari wa upelelezi walipoenda kuchunguza nyumbani kwa mchungaji huyo walikuta saa ya mkononi ambayo ilikuwa na matone ya damu, damu hiyo ilipochunguzwa katika maabara ilikuja kugundulika kuwa ilikuwa ni ya Leo Gleese.

  Mpaka kufikia hapo Polisi wakawa na uhakika kwamba sasa wamembaini muuaji wa Leo na Hazel Gleese, nae si mwingine bali ni Mchungaji John Nelson Canning. Siku chache baada ya kuongoza mazishi ya ajuza wale mchungaji Canning alikamatwa na kushitakiwa kwa mauaji ya ajuza hao. Katika kesi hiyo mchungaji Canning alikiri kuwa aliwauwa Leo na mkewe Hazel Gleese kwa kuwapiga kwa kitu kizito na kisha kuwanyonga usiku wa Januari 3, 1995, hiyo ilitokea baada ya kuwa amebanwa na ajuza hao kuhusiana na namna alivyotumia fedha zao huku wakimuonyesha taarifa ya benki inayoonyesha kwamba alijiandikia hundi na kujilipa yeye mwenyewe.

  Mnamo Februari 1996 mchungaji John Nelson Canning alipatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya Leo na Hazel Gleese ambapo alihukumiwa kifungo cha maisha jela bila ya uwezekano wa kupata msamaha wa kifungo cha nje (Parole). Mara baada ya kusomwa hukumu hiyo msemaji wa Polisi Phil Ramer aliwaambia wandishi wa habari kwamba hili ni tukio ambalo hatakuja kulisahau katika maisha yake.
  Kwa maneno yake mwenyewe alisema "ni vyema watu wakawa waaminifu, ni jambo la kushangaza kukuta mchungaji ambae ameaminiwa na waumini wake kisha anakuja kuwauwa baadae kwa sababu ya pesa"
   
 2. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Asante sana Bw.Mtambuzi kwa habari hii ya kusisimua.
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Leo ni Ijumaa nyingine tena, kama ilivyo ada, nimekuja na kesi hii ya Mchunga Kondoo wa Bwana wa kule nchini Marekani ambaye aliuwa kondoo wa Bwana kwa tamaa ya fedha. Tumekuwa tukishuhudia utitiri wa Makanisa yakiibuka hapa nchini kama uyoga, lakini ni vyema wale wanaojiunga na makanisa hayo wakawa makini sana na wachunga kondoo hao, kwani hata katika maandiko matakatifu tuliaswa kwamba watakuja wengi kwa jina lake lakini sio wote wakweli................

  Mchungaji John Nelson Canning aliaminiwa sana na waumini wake kiasi cha baadhi ya waumini kumfanya mshauri wao wa masuala ya kifedha, lakini Bwana na Bibi Leo Gleese walienda mbali zaidi kwa kumuasili (Adopt) na kumkabidhi akaunti zao za benki ili awe msimamizi wa fedha zao........ Masikini hawakujua jambo hilo litawaletea umauti........

  RIP Bwana Leo Gleese na Bibi Hazel Gleese
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hata wachungaji nao si wa kuwaamini, asante sana Mtambuzi.
   
 5. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu mtambuzi nakushukuru sana kwa kuendelea kutupatia habari hizi
   
 6. h

  hamic mussa JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Keep it up braza kisa kinasisimua sana. Sasa kaka vp ile kesi ya 'Vicent na hukumu ya kunyongwa' aliyeuwa familia yake mwenyewe uliifuatilia mwisho wake km jamaa alinyongwa au la? Ktk kesi zako zote ile ndio niliyoipenda zaidi na ndio nliamini wamarekani wana akili ya upelelezi maana hadi kumpeleka jamaa mahakaman walifanya kazi kubwa sana.
   
 7. M

  Mponjori JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 2,210
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Keep it up mtambuzi,wengi tunafuatilia japo hatu-comment!
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,542
  Trophy Points: 280
  Hivi ndo walivyo hawa akina Rev.???
  wachungaji wa kondoo wa Bwana, lol,
  na hii itafanya watu waogope
  kumuasili (Adopt)
  hawa watoto wengine
  .

  Habari ya zanzibar,
  je umeleta marashi ya pemba???
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  hamic mussa ni kweli kesi ya Vincent Brothers ni miongoni mwa kesi zilizokuwa na upelelezi makini sana ukiacha ile kesi ya kisa cha mwanamke ziwani ambayuo nayo niliwahi kuiweka hapa.
  Kuhusu kunyongwa, bado hukumu haijatekelezwa, kwa Marekani wao hawafichi siku yamkutekelezwa hukumu huwa inatangazwa na hata wale ndugu wa wahanga au mhang aliyeuawa na mtuhumiwa hualikwa kushuhudia hukumu hiyo ikitekelezwa, ambapo hutekelezwa kwa kuchomwa sindano ya sumu.
  Kwa kawaida hukumu ya kunyongwa hutekelezwa baada ya kupita miaka kadhaa na hiyo hutokana na labda mtuhumiwa amekata rufaa, au mpaka Govenor wa jimbo husika na jopo lake la washauri waridhike na hukumu hiyo na yeye ndio anaweka saini ya kutekelezwa kwa hukumu hiyo na hapo ndipo hutangazwa rasmi siku ya kunyongwa kwa mtuhumiwa......
  Kwa mfano:
  1. Timoth McVeigh aliyelipua bomu kule Oklahoma na kuua watu wapatao 168 alihukumiwa kunyongwa hapo mnamo Juni 1997 na hukumu yake ilitekelezwa June 2001
  2. Karla Faye Tucker alihukumiwa kunyongwa 1984 na hukumu ikatekelezwa Februari 1998.
  3. Gary Roland Welch alihukumiwa kunyongwa Agosti 1994 na hjukumu ilitekelezwa Januari 2012
  4. Jaffrey David Matthew alihukumiwa Julai 1997 na hukumu ilitekelezwa Januari 2011
  5. Troy David alihukumiwa mwaka 1991 na hukumu ilitekelezwa mwaka 2011
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 401
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 80
  Asante Mtambuzi kwa kesi hii ya kusisimua naamin nimejifunza mengi huwa najitahid kufuatilia kesi na visa mbalimbali unavyoviweka hapa....mimi ni kijana ninayesoma form five kwa kweli huwa navutiwa sana na visa mbalimbal unavovitoa kwa kuwa hunielimisha na kuniburudisha...naomba nikuulize swali tafadhal hivi gazet la Jitambue limepotelea wapi nilikuwa nalisoma kuanzia mwaka 2005 hadi lilipopotea kipind hicho npo darasa la tano...kama kuna mpango ningependa lirudishwe,hivi sijui na Munga Tehenan yupo wap..?
   
 11. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280
  Munga Tehenan Alishafariki tangu mwaka jana.
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Madame B Munga Tehenan ametimiza miaka mitano mwezi May mwaka huu wa 2012 tangu afariki dunia
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 401
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 80
  My God....!Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe....Rest in Peace Munga otherwise Asante Madame B kwa kunifahamisha hili keep it up....!
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  kamwendo, Gazeti la JItambue lilisimama kuchapishwa kwake miaka mitano iliyopita baada ya mhariri wake Munga Tehenan kufariki......................
  Nimekuwa nikiweka makala na vijimamabo vya Utambuzi hapa JF kila siku na kila Ijumaa naweka kesi kama hizi ili wadau wapate kujifunza
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu Mtambuzi kwa kunisahihisha.
  Nilinukuu vibaya.
  Na vp Gazeti la Jitambue Ndo Basi tena au,
  Maana yake lilikuwa linatupa Maisha ya Uhalisia ya Ukweli Mtupu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280

  kamwendo nimesahihishwa,
  Kafariki Miaka Mitano iliyopita.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 401
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 80
  My God....!Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe....Rest in Peace Munga otherwise Asante Mtambuzi na Madame B kwa kunifahamisha na kuliweka sawa hili keep it up....!
   
 18. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280
  Pouwa Mdogo wetu kamwendo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. h

  hamic mussa JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante mkuu na nlikuwa naomba untajie title ya kesi ya kisa cha mwanamke ziwani ili nayo niisearch coz iyo ckuisoma.
   
 20. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Jamani , kwa kweli inasikitisha sana, wale watu tunao waamini sana ndio wanaotufanyia ukatiri wa ajabu.

  Upendo na uaminifu wa hawa wazee kwa huyu mchungaji mwizi mpenda mali na muuaji mkubwa ndio uliowaponza,

  Eh mungu wapumzishe kwa amani na huyu mchungaji afie huko jera liwe fundisho kwa watu wengine.

  Thanks Mtambuzi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...