Kisa cha mbuzi wanaojichunga wenyewe Dar, mzee anayewamiliki asema ukiiwaiba utawarudisha tu

Massivve

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
274
368
Kama wewe ni mtembezi mzuri wa jiji la Dar es Salaam, bila shaka umewahi kukutana na kundi la mbuzi wanaokatiza barabarani wao wenyewe bila mtu anayewachunga.

Mbuzi hawa ni maarufu, huja mjini na kurudi wanakokaa bila kudhurika. Hakuna anayediriki kuwaiba wala kuwadhuru – waguse uone.

Mwandishi wa BBC Swahili, Humphrey Mgonja aliamua kuwafuatilia ili kubaini ukweli wa maisha yao, na aliyoyabaini, yatakuacha mdomo wazi.

“Wakifika barabarani hapo wanasimama kama vile binadamu, wanaangalia huku na huku wakiona gari hamna wanavuka, wana akili kuliko binadamu,” anasema mkazi mmoja wa Dar es Salaam.

“Wanavuka katikati ya zebra, mbuzi gani wa kuvuka katikati ya zebra kama binadamu?” Anahoji mwingine.

Kwa aliyewahi kutaka kuwafanyia hila mbuzi hao, cha moto alikiona.

“Aliwachukua Shoppers akawapeleka Vingunguti machinjioni, lakini kule hakufanikiwa hata kushika mbuzi mmoja, alichofanya ni kurudisha mbuzi hadi hapa Shoppers akainua gari lake, mbuzi wakaruka akaachana nao yeye akaamua kuondoka zake,” anasema Pascal Mshau aliyewahi kumshuhudia nduguye aliyejaribu kuwachukua.

Mwandishi Humphrey Mgonja aliwafuatilia mbuzi hao hadi usiku wa saa mbili walipoelekea kwenye makaburi ya Kinondoni ambako ndiko yalipo makazi yao. Mmiliki wa mbuzi hao, Mzee Omari amemwelezesha mwandishi huyo kuwa mbuzi wake hawaibiki.

“Hawa mbuzi huwa siwachungi, na wala huwa siwafungi, huwa nawaacha wanaenda kula wenyewe malishoni huko baada ya muda wanarudi wenyewe hapa nyumbani,” anasema mzee huyo.

“Sijawahi kuibiwa, na hata kama ataiba mtu, yeye mwenyewe atanirudishia tu, atarudisha mwenyewe,” anaongea kwa kujiamini.
 
Pale darajani ubungo upande wa mawasiliano kunakuwaga na mbuzi kadhaa saa kumi na moja asubuhi wamelala pembezoni mwa kingo za korongo, huwa suwaelewi hawa mbuzi pia maeneo fulani mbezi shule pale kibaoni kuna fungu la kama mbuzi 15 huwa wanazutura bila mchungaji siku nzima!
 
Kwa iyo huyo mwenye mbuzi hawachinji wala kuwakamua maziwa. Tiss wawachunguze hawa mbuzi wanaweza wakawa na faida kubwa.
Inaonyesha hawa domesticated animals are undergoing some evolution and adaptation in urban areas
 
Kumbe Wamasai hamna kitu! Yaani pamoja na kuwalisha watu magome ya miti pale Kariakoo lakini bado hawana maujanja ya Mzee Ommy ambayo yangewaondolea taabu ya kushinda machungani kila cku!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom