Habari ya Mujini
JF-Expert Member
- Dec 22, 2013
- 2,517
- 1,044
Naitwa Gerald Machange. Nilifunga ndoa mwaka 2009 na nimekuwa nikiishi na mke na familia yangu ya watoto wawili sasa. Nimeajiriwa na shirika la nyumba la taifa NHC.
Wakati nafunga ndoa, mke wangu hakuwa ameajiriwa kwa kuwa ndio kwanza alikuwa na miaka miwili tangu amalize elimu yake ya chuo. Tulikubaliana kuwa mara tu baada ya kufunga ndoa, zoezi la kutafuta ajira lianze mara moja.
Ahadi hii tukaanza kuifanyia kazi mapema baada ya ndoa na ingawa alikuwa mjamzito, tulitumia nguvu kubwa walau apate sehemu ya kupitisha siku.
Kwa kuwa nilikuwa na uzoefu kidogo katika mfumo, sikuchoka na kweli, baada ya miezi nane, mke wangu akapata ajira Wizara ya viwanda na akaanza kazi kama mhasibu msaidizi.
Maisha yetu yakazidi kuwa ya amani mpaka pale alipopata ujauzito wa pili. Mambo yakaanza kubadilika taratibu kwa kuwa, upendo uliokuwepo kati yetu ukaanza kupungua taratibu. Mara kwa mara alikuwa kimya muda mrefu na alipomaliza kazi zake, ungemkuta akiwa bize na simu yake ya mkononi na nilipojaribu kuwa naye karibu, hakunipa kabisa nafasi.
Roho ilikuwa ikiniuma sana lakini nikaamua kuvumilia. Kilichonipa moyo ni kuwa, nilihisi hali ile ilitokana na ujauzito aliokuwa nao na kuwa niliamini kuwa baada ya muda mambo yatakaa sawa.
Baada ya miezi tisa, akajifungua mtoto wa kiume ambaye nikimpa jina la Lameck.. Hata hivyo, baada ya siku tatu, mke wangu akasema mtoto yule hawezi kuitwa jina lile kwa kuwa halifanani naye, na akapendekeza kuwa aitwe Timothy. Nilishangaa sana kwa kuwa jina hilo jipya hatukuwahi hata kuliwaza, lakini hata hivyo nikaamua kuvumilia na kukubali.
Baada ya miezi kadhaa, siku moja nikiwa natoka kazini nilisikia mke wangu akiwa anaongea na simu ndani. Nilivutiwa na mazungumzo yale kwa kuwa alikuwa akimtaka rafiki yangu mkubwa sana ambaye pia yuko Wizara ya viwanda aitwaye Julius Bongi ingawa tulikuwa tukimwita Bongi J. Nikajibanza kusikiliza.
Sikuweza kuunganisha vema mazungumzo yale, lakini katika simu ile alikuwa akimsisitiza mtu fulani kitu huku akisema "Yani kila anavyozidi kukua anazidi kufanana na Bongi J.. Sijui nafanyaje...".. Moyo ukanipiga pah!!
Akili ikasimama ghafla. Ni kweli, mtoto yule alikuwa na haiba fulani kama ya rafiki na ndugu yangu wa karibu Julius Bongi. Nikaamua kufanya uchunguzi.
Sikuonesha tofauti yoyote. Baada ya muda wa kurudi kazini mke wangu, nikaanza upelelezi. Kwa miezi miwili nilikuwa nikifuatilia nyendo zao kwa ukaribu sana. Mara kwa mara, walikuwa wakitoka kwenda kwenda kunywa chai au chakula cha jioni pamoja. Ajabu zaidi ni kuwa, mara kadhaa mke wangu alikuwa akienda na mtoto kazini jambo ambalo kwa mazingira ya kazi nilijua sio la kawaida.
Siku moja nikaamua kuvunja ukimya na uvumilivu ambao nimeuonesha kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu. Nakumbuka ilikuwa siku ya ijumaa na mke wangu akaniaga kuwa, angekuwa na safari kwenda kwao Bagamoyo kupumzika. Nikamkubalia huku nikipanga kumfuatilia.
Alipotoka kazini, akanipigia simu kuwa ndio anaondoka. Wakati huo nilikuwa nimepaki gari kama mita mia nne hivi kutoka ofisini kwao, hivyo kabla hajatoka, lazma ningemwona. Kwa bahati mbaya wakati tunaongea, simu yangu ikazima ghafla. Nilijaribu kuiwasha bila mafanikio.
Nikashuka na kukimbia pembeni kwenye kibanda cha kuuzia simu nikiamini kuwa wanaweza kunisaidia kuichaji kidogo ili iwe rahisi kumfuatilia mke wangu.
Nilipoingia tu kwenye kibanda kile sikuamini kabisa macho yangu. Nilikutana na kijana mmoja ambaye alishawahi kunizulumu zaidi ya laki mbili na nusu. Nilijaribu kumkumbusha juu ya pesa yangu lakini hakuonesha dalili ya kulipa zaidi ya kuwa mbishi na kusema hakuwa na fedha kwa wakati ule.
Ndugu zangu, hebu nishaurini.. Huyu jamaa mi nimfanyaje ili anilipe hela yangu?