Kisa cha Kafulila kuvuliwa uongozi hiki hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisa cha Kafulila kuvuliwa uongozi hiki hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by April, Dec 13, 2011.

 1. April

  April Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] Wakati hali ikiwa tete katika Chama cha CUF, mzozo mwingine mkubwa ambao umeibuka ndani ya Chama cha NCCR- Mageuzi umefikia hatua mbaya, baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Samuel Ruhuza, kumvua madaraka ya Ukatibu Mwenezi Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.


  Akizungumza na gazeti hili jana jioni kwa njia ya simu, Kafulila alikiri kupokea barua ya kuvuliwa wadhifa huo kutoka kwa Ruhuza, akisema ameambiwa kuwa hayo ni mamlaka ambayo anaweze kupewa na kuondolewa.

  “Ni kweli nimepokea barua lakini mimi sijaona tatizo lolote kwani sikuomba nafasi hiyo bali niliomba ubunge. Ujue hadhi ya ubunge ni kubwa kuliko katibu mwenezi, hivyo nimejulikana na kuheshimika kwa wadhifa wa ubunge,” alisema.
  Alifafanua kuwa ana uhakika shinikizo la kuondolewa kwake limetoka kwa Mbatia, kwani ameonesha wazi kuwa hamtaki yeye pamoja na Mbunge wa Mhambwe, Felix Mkosamali, kutokana na kutofautia naye.

  “Mbatia hata yeye ubunge anajua una hadhi kuliko hata uenyekiti wake, ndiyo maana aliomba kura Jimbo la Kawe lakini akashindwa. Ila anajua hali ni ngumu na anaweza kuangushwa kwenye NEC ijayo, hivyo anadhani mchawi wake ni mimi na Mkosamali,” alisema Kafulila.

  Alisema Mbatia hana jambo la kukwepa kuhusu kutumiwa na CCM bali anachotakiwa kufanya ni kuhamia huko ili akafanye kazi vizuri na kuiacha NCCR mikononi mwa watu wenye malengo ya mageuzi.
  “Juzi nilihojiwa kuhusu wapinzani kukutana na Rais Jakaya Kikwete, nikatoa msimamo wangu kuwa sina imani na serikali ya CCM na nikasema NCCR-Mageuzi hatutakwenda Ikulu kuonana naye kwani hatuwezi kupangiwa ajenda na CCM. CHADEMA walikaa kwenye vikao wakaibuka na ajenda yao,” alisema.
  Mwanasiasa huyo aliongeza kuwa baada ya kutoa msimamo huo, Katibu Mkuu wao, Ruhuza, alimpigia simu na kumlalamikia kuwa aliisema vibaya CCM na kuwahi kutoa msimamo wa kutokwenda Ikulu, hatua aliyoiona kuwa viongozi hao wana ajenda ya siri.

  Kafulila ni miongoni mwa wanachama na viongozi wengi wa chama hicho wanaomshinikiza Mwenyekiti wao, James Mbatia, ajiuzulu nafasi hiyo kwa madai kuwa amekuwa akifanya kazi kama kibaraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuvihujumu vyama vya upinzani, kikiwamo NCCR-Mageuzi.

  Halmashauri Kuu ya chama hicho iliyoketi Novemba 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea malalamiko ya wajumbe hao ilimpa Mbatia siku 21 za kutoa utetezi wake kwa maandishi ili mkutano ujao Februari 3, mwakani uweze kutoa uamuzi ama wa kumuengua au la.

  Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa Mbatia anataka kuwafukuza wajumbe wote wa NEC aliowateua halafu wanampinga ili kuweka mazingira mazuri ya kutoenguliwa katika mkutano wa Februari.
  Lakini kuhusu hilo, Kafulila alisema kuwa anajidanganya kwa mpango huo, kwani licha ya kumuondoa kwenye ukatibu mwenezi bado anabakia kuwa mjumbe wa NEC kwa wadhifa wake kama mwenyekiti wa wabunge wa chama hicho.

  Source: Tanzania Daima  Kazi ipo!!  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  “Mbatia hata yeye ubunge anajua una hadhi kuliko hata uenyekiti wake, ndiyo maana aliomba kura Jimbo la Kawe lakini akashindwa. Ila anajua hali ni ngumu na anaweza kuangushwa kwenye NEC ijayo, hivyo anadhani mchawi wake ni mimi na Mkosamali,” alisema Kafulila.

  Kafulila wewe ni Mkale, yaani unamchana live mwenyekiti wako bila Chenga?
   
 3. josefast

  josefast JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  kaz ni kwenu kama vp mrud CDM
   
 4. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kafulila's end is looming.
   
 5. W

  Wakurogwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawezi kurudi alishaambiwa yeye ni Sisimizi ndani ya chadema.
   
 6. W

  Wakurogwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawezi kurudi alishaambiwa yeye ni Sisimizi ndani ya chadema.
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Njaa na tamaa ya madaraka ni kama saratani!
   
 8. zululima

  zululima Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapana wasione aibu, wao warud nyumbani wazungumze na makamanda wenzao wa ukweli . Kafulila na mkosamali mmekulia cdm. hilo mamluki limekulia ccm b(bara) hawatamuweza pale. Nawasihi vijana rudini nyumbani kwa pamoja tukimbize magamba.
   
 9. CHIETH

  CHIETH Senior Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vitha ni vitha Mra.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sisimizi kawa tembo ss arudi chadema
   
 11. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Aseme tu samahani Chadema, then atapokelewa aongeze nguvu kwa makamanda! Lakini kama Mbatia ni kibaraka atakuwa anafanya usaliti sana kwa Taifa hili.
   
 12. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Huyo dogo naona ubunge unamchanganya. Asubiri 2015 hatma yake.
   
 13. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe, wanaweza kurudi, na sas watakuwa wamekomaaaaa
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sisimizi unakonda nini ..hahayayaaa sikulagi kwenuuu
   
 15. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ndio njia aliyoichaagua hiyo,
  Hey K pambana na hatima yako kiasa, nadhani bado una mengi ya kukumbana nayo katika hicho chama chako!
   
 16. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera CHADEMA kwa kutokuungana na vyama hivi (CUF and NCCR Mageuzi) kuunda kambi rasmi kwani vingetuletea matatizo.
   
 17. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kafulila na mkosamali wakirudi chadema nani ataomba msamaha? slaa kwao au wao kwa slaa? strictly kwa wenye jibu tu.
   
 18. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyo kafulila sasa nimeamini hana nidham kabisa. Inaonekana ni mbinafsi na anadhani anjua sana. Hawezi kuwa mwanasiasa mzuri make anayetofautiana naye kimawazo ni adui. Asipojirekebisha atakufa kisiasa. Maana hakuna chama kitamfaa labda awe mgombea binafsi.
   
 19. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwani siasa ni lazima? Hawa watu si waje uraiani au wanaogopa watapoteza pos....? Kuna mtaalamu mmoja wa masuala ya kisiasa aliwahi kusema 'yapo maisha nje ya siasa' nawasihi nyie mabwana wadogo Kafu na mwenzio Mali, nyie bado mna nguvu na vijana wadogo acheni kubweteka na porojo hizo, njooni kitaa mbona byeeeee tu. Siasa ni hatari bana, kama vipi walipeni hao maccm b, c na d then msepe....
   
 20. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kafulila ni sawa na lusifa, anapenda sana madaraka, hata kwa magamba watamfukuza
   
Loading...