Kisa cha Bob Marley kumpiga Risasi Sheriff John Brown vs Mkulima Mwamwindi na Dr Kleruu

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
ilikuwa siku kama siku nyingine katika maisha ya Bob Marley akiwa katika mizunguko yake. jioni hiyo akitembea taratibu na mara ghafla yake akamwona Sheriff John Brown akiwa anakatiza mtaani na kuingia kwenye kichochoro flani. Bob Marley alisogea kuelekea kwenye hicho kichochoro kilichokuwa na giza kiasi flani na kuchomoa bastola yake.akajibanza pembeni ya ukuta na kufyatua risasi ambazo zilienda moja kwa moja kumpiga sheriff john brown kifuani akaanguka.sheriff alijaribu kuamka lakini hakuweza ,akashikilia kifua chake kwa maumivu damu zikimtoka mdomoni na kujilaza tena chini akiwa amezama kwenye dimbwi la damu... akakata roho kwa maumivu makubwa sana.

ilikuaje mpaka bob marley kumuua sheriff john brown?

Bob Marley anasema alipotunga wimbo huu wa i shot the sheriff kiuhalisia alitaka kusema i shot the police. kwa nini Bob Marley atake kumpiga Risasi Polisi?
Bob M anazungumzia polisi ambao wamekuwa corrupt. wala rushwa ambao wamekuwa wakiwanyanyasa raia na kuwatendea isivyo stahili.unyanyasaji huu na mwingine pia ukawa unamfanya afuge chuki, ukifuga sana chuki hufikia hatua inajenga kisasi dhidi ya uumchukiaye. anasema lengo lake lilikuwa ni kuwachana polisi kutokana na maovu yao dhidi ya wananchi ila akahofu kuwa wimbo ungeingia kwenye mgogoro na serikali. ndo maana akaamua kuubadilisha iwe i shot the sheriff badala ya i shot the police.

sheriff john brown alikuwa siku zote aki mharass bob marley. akifanya ubabe na kumnyanyasa kitu ambacho kilimfanya afikie hatua ya kuchoka kutokana na yale manyanyaso. aliamua kuchukua sheria mkononi.kumuua sheriff john brown.

bob marley anakataa anasema hakumuua msaidizi wa sheriff. inaonekana kama sababu ya kukosekana kwa ushahidi wa yeye kumuua sheriff john brown wakaamua kumuua sheriff ili waweze msingizia Bob Marley. yeye anasema kuwa ni siku nyingi walikuwa wakimtafuta ili waweze mframe kutokana na kifo cha deputy.anakataa hakumuua Deputy.hicho kifo anasema hakuhusika kabisa ila alimuua sheriff katika hali ya kujihami.bila shaka inaonekana kuwa sheriff john brown alikuwa na nia ya kumdhuru BM.

Maana yake nini?
kuna kipindi watu hufikia hatua na kuchoka. huchoka kutokana na mambo ambayo hutendewa kinyume na haki. hapo huamua kuchukua hatua mkononi.jambo hili linatufunza siku zote tujitahidi kutenda haki.kuna kipindi watu huamua kufanya maamuzi magumu.binadamu tumeumbwa na kiasi. kama walivyo wanyama wengine wote. paka unaweza ukamnyanyasa sana.lakini hufikia hatua huchoka. wanasema paka anapofikia kuchoka hufanya maamuzi magumu.afe yeye ufe wewe.

kuna mengi ambayo watu wanazungumzia kuhusiana na wimbo huu likiwepo suala la birth control n.k lakini Bob M anasema ni hawa polisi waovu. inawezekana ikawa ni hawa viongozi waovu.hawa ndio ambao watu hufikia hatua na kuchukua maamuzi magumu.

Wito wangu kwa Serikali

Mnamkumbuka kisa cha Mkulima Mwamwindi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa dr kleruu tarehe 25-12-1971.Mwamwindi aliamua kum piga risasi Mkuu wa Mkoa na hakutaka kukimbia baada ya kitendo hicho. alibaki hapo hapo pengine akawa amewasha sigara anavuta kusubiria polisi waje mkamata.alikubali kuwa amemuua dr kleruu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyafanya kwao. tukio alilolifanya mwamwindi lilikuwa tukio ambalo watu hufanya wanapofikia katika point of no return. wapofikia kwenye ukingo wa thim. huamua kufanya jambo ambalo hawajutii kulifanya.

serikali iangalie watu wasifike hatua hiyo ambayo ni mbaya sana. yanayotokea afrika kusini yanaweza tokea tanzania kwa mfumo mwingine. si lazima wauawe wageni. inawezakana machafuko yakatoea dhidi ya tabaka flani. maybe watu flani na familia zao. hili linawezekana. hali ngumu waliyo nayo wananchi wanatafuta wapi waondolee stress zao na machungu waliyo nayo.

siku moja mtu atasimama na kusema I SHOT THE SHERIFF....Proudly kabisa with a smile on his/her face. then the person will handle his/her hands to be encuffed with no remorse.








wimbo huo aliuimba bob marley si kwamba alienda mshoot mtu.hii ni kazi ya fasihi.
 
Mkuu Gudume binafsi nimekuelewa vizuri sana nina Imani Wahusika Wakuu wanapita humu nao pia watakuwa wamekuelewa bila shaka ..






















Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
Mungu Ibariki Morogoro
 
Back
Top Bottom