Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,679
- 729,847
Ulishawahi kulitafakari jina lako au la mtu mwingine na ukalingalisha na maisha yake?je kuna mfanano wowote?
Kila jina liwe la biashara ama la mtu lina maana yake kubwa sana na katika ulimwengu wa roho huwa na kichokoo hasi ama chanya kwenye maisha ya mhusika
Kuna baadhi ya makabila huenda kuchagua jina kwa mtabiri na hii yote ni kutaka mtoto atakapokuwa mkubwa jina liwe na matokeo chanya na si hasi..kuna majina hutolewa kulingana na majira ya mwaka na nyakati zake
Huku kwetu Africa majina mengi ni ya kurithi vizazi na vizazi na ndio maana kwenye ile mada ya laana za ukoo jina pia lina nafasi yake kubwa tu
Kuna wakati jina linaweza lisiwe halisi! Yani unajipachika ama kupachikwa na wengine na kwa mshangao likaja kuwa sawasawa na tabia na hulka zako
Ni katika haya majina yetu yasipotuathiri sisi wenyewe mengine huwa na athari kwenye jamii! na kwakweli ni afadhali jina liwe na athari mbaya kwa mhusika kuliko jamii isiyo na kosa lolote
Tunazielewa fika tabia za makonda hata avae na kupendeza sana lakini hulka na tabia zake zitabebwa na jina lake. KONDA NI KONDA TUU.....
Tunaelewa kwa undani kabisa nini maana ya neno SHIDA ama TABU au SIKUZANI nknk...sasa kama mzazi unapompa mtoto wako jina kama hili unategemea nini?
Ninaweza kumshangaa mtu ambaye hajui kazi ya komeo ama kitasa...kazi ya ni kufunga...kwenye ulimwengu wa roho jina kama hili laweza funga vingi sana
Jina ni utambulisho wenye kuleta uhalisia katika maisha yetu furaha zetu shida zetu changamoto zetu mafanikio na hata anguko huathiriwa kwa kiasi kikubwa na kile tulichokitanguliza kama taa
Tunaishi kwenye kipindi kinachoathiriwa na utambulisho kwa sehemu kubwa tu...hivyo episodes hazitakoma
Kilichofungwa duniani na kwenye ulimwengu wa roho pia kimefungwa..kilichofunguliwa mbinguni na duniani pia kimefunguliwa