KIPINDUPINDU: Dalili, tiba na namna ya kujikinga

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,394
2,000
Kipindupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo husababishwa na aina ya bakteria aitwaye Vibrio cholerae, Ugonjwa huu ni wa kuambukizwa kwa njia ya viini vinavyoenezwa kupitia kwa kinyesi kutoka kwa wagonjwa wenye Kipindupindu.

Kipindupindu sana sana iwapo mahali hakuna maji ya mfereji au mabomba ya kupitisha maji machafu.

Mabomba ya kupitisha maji machafu yasiyofunikwa na matanki ya maji ya kunywa yasiyofunikwa huchangia katika kusababisha mkurupuko wa kipindupindu.

Kwa sababu hii, ugonjwa wa kipindupindu ni shida inayotokea sana sehemu za mashambani au vitongoji duni kwenye hakuna maji ya mfereji na mabomba ya maji machafu.

150709083228_cholera_bacteria_624x351_bbc_nocredit.jpg
Bakteria aenezaye ugonjwa wa Kipindupindu

Dalili

1. Dalili bainifu ya ugonjwa huwa ni kuharisha sana haja iliyo majimaji.

2. Mwili hushindwa kutumia maji na chakula hivyo basi kumfanya mgonjwa kudhoofika haraka kwa sababu ya kukosa maji mwilini.

3. Mgonjwa huhisi kiu kingi na uchovu mwingi, na hushindwa kutulia.

4. Ngozi ya nje na ndani itanyauka na macho yataingia ndani na watahisi kichefuchefu na kiharusi kisicho cha kawaida.

Vipimo
Madaktari huchukuwa choo cha mtu kuangalia iwapo ana kipindupindu, kwani viini vyake havipatikani kwa damu.

Matibabu


1. Mgonjwa hunyweshwa maji mengi, kwa sababu mwili wake hupoteza maji mengi anapougua maradhi haya.

2. Dawa zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone.

3. Chanjo za kuzuia Kipindipindu ambazo hutolewa katika baadhi za nchi.

Kuepukana na Kipindupindu
Kinga ni kama ifuatavyo:


 • Wakati wowote kunawa mikono kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo kama sahani, vikombe n.k.
 • Nawa mikono kabisa kwa sabuni – kiganja, upande wa nyuma wa mkono, katikati ya vidole na kucha kwa sekunde. Baada ya haja na kabla ya kula.
 • Kuwa na akiba ya maji yaliyochemshwa pasipo na maji safi ya bomba
 • Kupika chakula vizuri maana halijoto juu ya 75 °C (hadi 85 mlimani) inaua bakteria;
 • Kumenya matunda yote
 • Kufunika chakula maana nzi wanapitisha bakteria kwa miguu yao
 • Maji ya choo yanayotokamana na wagonjwa wa kipindupindu yanapasa kupitia mashimo ya choo yaliyohifadhiwa vizuri ili kuzuia usambazaji wa bakteria
 • Vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto
 • Mikono inayoshika wagonjwa au nguo zao inapaswa kunaniwa kwa sabuni
 • Mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia klorini
 • Tumia maji yaliyotibiwa pekee hasa ikiwa ni ya kunywa; yachemshe au utie matone 5 ya klorini kwa kila galoni 1 au utumie dawa ya kutakasa maji. Yaache maji yatulie kwa dakika 30 kabla ya kunywa.
 • Tumia choo kila mara – usiende haja karibu au ndani ya chanzo cha maji.

CHOLERA-6.jpg
Wagonjwa wa kipindupindu wakipata tiba.
 

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,073
1,250
UGONJWA wa kipindupindu umelipuka mkoani Morogoro na kuua watu wanne wakiwemo watatu wa familia moja katika Manispaa ya Morogoro na Wilaya ya Mvomero.

Akizungumza jana ofisini kwake, Ofisa Afya Mkoa wa Morogoro, Cares Lyimo alisema, ugonjwa huo ulilipuka Novemba 20 mwaka huu katika Kata ya Mgeta wilayani Mvomero na mpaka sasa watu 69 wameshaugua ugonjwa huo.

Alisema, katika Wilaya ya Mvomero, mtu mmoja alifariki dunia na wengine 58 waliugua ugonjwa huo na kutibiwa kabla ya kuruhusiwa kurejea makwao.

Lyimo alisema katika Manispaa ya Morogoro ugonjwa huo ulilipuka tangu Novemba 25 mwaka huu katika Kata ya Lukobe na umeshaua watu watatu wa familia moja akiwemo mama na watoto wake wawili.

Chanzo cha ugonjwa huo kwa mujibu wa ofisa huyo, ni uhaba wa maji katika Mkoa wa Morogoro ambao umesababisha watu wengi kutumia maji hasa ya kununua kwenye magari, bila kujua maji hayo yanachotwa wapi na yana usalama kiasi gani.

Aliwaasa wakazi wa mkoa huu kujilinda kwa kutumia maji safi na salama muda wote na kuzingatia kanuni za afya na kuhakikisha mazingira yanayowazunguka yanakuwa safi muda wote.

Ofisa Afya Manispaa ya Morogoro, William Lema alisema uongozi wa manispaa hiyo unakusudia kufungua kituo cha matibabu katika Shule ya Msingi Azimio iliyopo katika Kata ya Lukobe, Manispaa ya Morogoro, ili kusaidia wagonjwa wanaotoka katika eneo hilo kupata matibabu kwa haraka.

Lema aliwaasa wananchi wa Manispaa ya Morogoro kufuata kanuni za usafi kwa kula vyakula vya moto, kunawa mikono kabla na baada ya kula, kuchemsha maji ya kunywa na kuosha matunda kabla ya kula.

Alisitisha shughuli zote za upishi wa pombe za kienyeji kwa wakazi wa manispaa hiyo kutokana na utengenezaji wa pombe hizo wakati huu wa uhaba wa maji na kuwepo uwezekano wa watengenezaji kutumia maji yasiyo salama.

Aliwataka mama lishe kuwa makini katika utengenezaji wa chakula na walaji kujiridhisha kwa kuangalia maji yanayotumika kuoshea vyombo na ikibidi kujiepusha kula vyakula hivyo.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,859
2,000
Kipindupindu charejea kwa kasi Dar

WAGONJWA 17 wamelazwa kwenye kambi maalum zilizotengwa na Jiji la Dar es Salaam baada ya kuugua wa Kipindupindu.
Ugonjwa huo ulipotea Dar es Salaam baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kupiga marufuku uuzaji mchicha holela uliokuwa ukifanywa.

Akitoa takwimu kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Hawa Kawawa, Ofisa habari wa jiji hilo, Raphael Kilapilo, alisema idadi hiyo inatisha ikilinganishwa na juzi kulikuwa na wagonjwa 15 na imepanda hadi 17.

"Kutokana na ugonjwa huo kuanza baada ya mvua kunyesha, wagonjwa wapya 17 wamelazwa vituo maalum tulivyovitenga kutoa huduma," alisema Dk Kawawa.

Dk Kawawa alisema hakuna mgonjwa aliyefariki na kwamba, kulingana na taarifa za manispaa zote; Ilala, Temeke na Kinondoni wagonjwa wote wameruhusiwa kurudi nyumbani.

Alisema Manispaa ya Temeke inaongoza ikiwa na wagonjwa 15, ikifuatiwa na Ilala wawili, Kinondoni haina mgonjwa.
Aliwataka wananchi kuzingatia usafi maeneo yao na kuchemsha maji ya kunywa.

Alisema Dar es Salaam inakabiliwa na tatizo la kutokuwa na maji safi na salama.
Dk Kawawa alisema kwa kuzuia ugonjwa usiendelee, Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na wenyeviti wa serikali za mitaa wamejipanga kutoza faini watu watakaoonekana kutupa taka ovyo.

 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,859
2,000
Alisema Dar es Salaam inakabiliwa na tatizo la kutokuwa na maji safi na salama.
Dk Kawawa alisema kwa kuzuia ugonjwa usiendelee, Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na wenyeviti wa serikali za mitaa wamejipanga kutoza faini watu watakaoonekana kutupa taka ovyo.

Uchafu ni silika yetu kwa hiyo magonjwa nyemelezi kamwe hayatatutoka......................
 

Maalim Jumar

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
1,243
1,250
Rutashubanyuma!
Tufafanulie vzuri!
silka yetu wote waishio dar?
Naamini hao yawezekana si wazoefu katika jiji letu! Hivyo namna ya kukabiliana na uchafu inawashinda.
Kweli jiji maeneo mengi machafu hata mijengo na vyoo vinavyojengwa hatari tupu...maofisa wa afya hawakagui na kushauri kwa wadhifa zao..
Uchafu...vyooo vnajaa... Yaani hata nmechefuka!
 

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
10,782
2,000
Dar iko chini ya maji ya mafuriko tangu juzi. Kama inavyojulikana miundombinu ya Dar hususan ya maji machafu ni mibovu sana na maeneo yenye ujenzi holela kama Kigogo, Mkwajuni, Bonde la Msimbazi n.k miundombinu hiyo haipo kabisa.

Mvua zinaponyesha wakazi wa maeneo haya wamekuwa na desturi ya kuelekezea uchafu wa vyooni kwenye maji ya mkondo wa mvua kitu kinachoweka afya za wakazi wa jiji kwenye hatari kubwa ya magonjwa ya mlipuko.

Kwa jinsi mafuriko na kiasi cha maji ya mafuriko tulichoshuhudia ni wazi maji hayo yamefumua hata septic tank kwa wale wenye vyoo vya kutumia mifumo hiyo. Ni wazi kuwa maji yote ya mafuriko tunayoyaona Dar kwa sasa yako contaminated na uchafu wa chooni.

Maeneo mengi yaliyokumbwa na mafuriko mifumo yake ya maji masafi kwa kiasi kikubwa pia imeharibiwa vibaya hivyo watu hao hawana hata uhakika wa maji ya kunywa...

Serikali ichukue hatua za dharura sasa za kugawa maji na kutoa tahadhari kwa wakazi wa Dar juu ya magonjwa ya mlipuko ambayo ni wazi yatafuatia baada ya maji ya mafuriko kupungua.

Tunaomba serikali ijiandae sasa kukabiliana na changamoto za baada ya mafuriko ili kunusuru maisha ya wakazi wa Dar maana majuto ni mjukuu.
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,394
2,000
Cholera is among one of the serious infections of intestine. In cholera the lower part of the small bowel gets infections and this is mostly seen during raining season. This disease is mainly seen among kids belonging to

places like South East, India and Mid East Asia. The kids in the age group of one year to three years are the main targets of cholera disease. It is life-threatening disease, due to the heavy fluid loss that happens during this

disease and hence the patient should get urgent medical help. Though there are some

home remedies for cholera
that will prove effective in fighting with the cholera bacteria


Home remedies for Cholera: • Limejuice - This juice should be given to the patient daily. The limejuice will keep the body well hydrated and also kill the cholera bacilli, which is the root cause of cholera.
 • Bitter Gourd Juice - Add half glass of onion juice to half glass of bitter gourd juice and put few drops of lemon juice in it. Drinking this mixture of juices is also effective way to treating the cholera.
 • Mint Juice - Drinking mint juice on a daily basis will provide relief from the symptoms of cholera, like vomiting and nausea.
 • Onion Juice - Grind some onions with seven black peppers and prepare an infusion form it. Consume it two to three times in a day.
 • Cloves - Boil drinking water by putting some cloves in it. Always drink this boiled water and follow this remedy during the rainy season every year.
 • Coconut Water - Cholera patients always feel thirsty and for this reason it is best to give them coconut water whenever they want water. You can also mix coconut water with juice prepared from cucumber leaves.
 • Onion and Lemon - Both onion and lemon are good for cholera patients and hence you can either include these two while preparing food or make a juice of these two and give it to the patient.
 • Asfoetida - Add powder of asfoetida to a cup of onion juice and take this drink on a daily a basis.
 • Clove Oil - To improve the poor conditions of the immune system, add some sugar in clove oil and have it at least once in a day.
 • Buttermilk - Take one glass of buttermilk and add one teaspoon of cumin seeds powder and some rock slat. Drinking this glass of buttermilk is one of the very effective home remedies for cholera .
 • Avoid Junk Food - During rainy season at least take care not to it outside food. Advice your kids not to eat any outside oily stuff or not to drink outside water. This will prevent the cholera disease form happening.
 • Rice Water - In case of diarrhea, which is the most common thing to happen during cholera, drinking one bowl of rice water is very good.
 • Eat Yogurt - Eating yogurt with every meal has plenty of benefits and is also very effective in cholera.
 • Diet should be Light - The food of the cholera patient should be very light so that it doesn't put extra pressure on the already infected intestine.

Cholera1.jpg

 

Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
3,228
2,000
Kwa hivi sasa kuna ongezeko la “nzii”, tumejiandaaje kuepuka kipindupindu, sehemu za mighahawa wametanda, si ajabu ufunguapo kinywa kumeza mlo nae akaja akajichanganya hapo ukamtafuna…kwa wapendao chipya mayai "ZEGE" ulapo ule kwa makini..wakati unywapo soda wanaingia bila wewe kujua... litakapolipuka tutamudu kulizuia??
 

leipzig

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
2,771
2,000
Katika pitapita yangu maeneo mbalimbali ya jiji nimeona marundo ya takataka kwa tani na tani ndipo nikauliza kulikoni ?waketeketwa wa siasa chafu na uongozi hovyo wakaniambia serikali haina pesa za kuwalipa wazoa takataka,pesa nyingi zimetumika katika sherehe za muungano kiasi cha Tsh 8.6 bln.
Sasa najiuliza hizi mvua zinazoendelea na mlundikano wa takataka tutapona kipindupindu?
Ama kweli kupanga ni kuchagua !
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
49,294
2,000
Maisha ni kupanga, na kupanga ni kuchagua.

Sherehe ni kipaumbele cha serikali
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,589
2,000
Utawala dhaifu usiokuwa na vipaumbele! Nasi tumelala mno kiasi kwamba hatuhji matumizi ya hovyo ya kodi zetu na kuchukua hatua pale tusiporidhika na matumizi. Tunawaogopa wezi wa fedha za umma kuliko shetani! Amkeni mlikolala.
 

Kobello

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
7,066
2,000
Katika pitapita yangu maeneo mbalimbali ya jiji nimeona marundo ya takataka kwa tani na tani ndipo nikauliza kulikoni ?waketeketwa wa siasa chafu na uongozi hovyo wakaniambia serikali haina pesa za kuwalipa wazoa takataka,pesa nyingi zimetumika katika sherehe za muungano kiasi cha Tsh 8.6 bln.
Sasa najiuliza hizi mvua zinazoendelea na mlundikano wa takataka tutapona kipindupindu?
Ama kweli kupanga ni kuchagua !
Samahani mkuu naomba nikuulize.
Serikali ipi isiyokuwa na hela ya kuwalipa wazoa taka?
 

LOOOK

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,390
1,225
Sio hapo tu sasa hivi ni mikoa mingi tu takataka hazizolewi.
 

Magnificient

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,148
2,000
Tanzaniaa tanzaniaa.. Nakupenda kwa moyo wote... Nchi yangu tanzania....

Tanzania raha sana jamani, mtu yeyote anaweza kupewa uongozi na kuongoza; bora awe na hela na aweze kuroga!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom