Kipindi Maalum Cha Lowassa Channel Ten

Kipindi Maalum Cha Lowassa Channel Ten

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Itakapo timu saa tatu kamili usiku kutakuwa na kipindi maalum chanel ten cha safari ya matumaini.
Watarusha toka mzee Lowassa atangaze nia pale arusha na sehemu zote alizopita kusaka wadhamini bara na visiwani mpaka hatua ya kurudisha fomu dodoma.
 
Naona anaamua kuonesha jinsi kampeni zake zilivyokuwa
 
Amehangaika sana Lowasa, kwa nini hataki kufuata utaratibu Kampeni za nini?
 
Ama kwali Lowasa anania na Urais.!
 
Matumizi makubwa ya pesa kafanya akiwa rais ndo itakuwa balaaa.
Namimi nakula limao
 
Amehangaika sana Lowasa, kwa nini hataki kufuata utaratibu Kampeni za nini?

taratibu haziruhusu yeye kurusha hizo sehemu.mbona huwaga kwenye taarifa ya habari wanawekaga vipande vya sehem walipopita
 
CCM hebu angalieni jinsi LOWASSA kwa makusudi ameamua kuanza kampeni wakati chama hakijaruhusu
 
Sasa huu ni uvunjaji wa wazi kabisa wa ''kanuni za CCM''. CC haitopata shida kumg'oa huyu muheshimiwa sana
 
Lowasa kama una sifa unaangaika nini mzee? nani hajapita uko kutafuta wadhamini bona wengi tu wewe nini kinachokufanya uangaike hivyo ,kweli washahili walisema KIZURI CHA JIUZA KIBAYA CHA JITEMBEZA,
 
Itakapo timu saa tatu kamili usiku kutakuwa na kipindi maalum chanel ten cha safari ya matumaini.
Watarusha toka mzee Lowassa atangaze nia pale arusha na sehemu zote alizopita kusaka wadhamini bara na visiwani mpaka hatua ya kurudisha fomu dodoma.
Sasa hivi saa tatu dakika 12 hamna dalili ya Lowasa kurushwa, au sio saa tatu ya leo.
 
Sasa huu ni uvunjaji wa wazi kabisa wa ''kanuni za CCM''. CC haitopata shida kumg'oa huyu muheshimiwa sana

mkuu tatizo ni nini unajua?
1, lowasa mwenyewe hana akili za kujiongoza
2,mshauri wake kingunge unatengemea nini hapo?
3,washauri wake wanamuigiza choo cha kike nae anakubali kukaa,na kwa kuwa anabaka siasa nae anakurupuka siasa hazijui.
 
lowasa anavunja kanuni waziwazi na hakuna anayevhukua hatua. ccm hii ya sasa ni hatari..
 
Bavicha mnajifanya nyie ni ccm tumewagundua,lowasa ndio mgombea pekee atayewatoa jasho Ukawa yote,jifarijini
 
Zamani vijana wa CCM walikuwa imara sana kukijenga chama,nasema zamani enzi chama cha wakulima na Wafanyakazi,walijali na kuzifuata kanuni za chama chao wakaweka taratibu zote,leo wenyechama hawapo tena si wakulima na wafanyakazi hataa ni matajiri na viongozi wa serikali,vijana hawapo wanalumbana kwa ushabiki wa watoa nia na si mustakabali wa Taifa wazee wa CCM nao kushney haya yanatokea wameweka mikono nyuma tuu,aibu kubwa ccm kwa haya yanayotokea...ndani ya miaka 10 uongozi wa ccm ulianguka mara kadhaa akibaki mwenyekiti pekee,na hata yeye aliponea kiduchu kutunguliwa nafasi hiyo,ni aibu kwa chama hiki kilicholeta ukombozi wa baadhi ya nchi za Afrika,leo ushabiki,Rushwa ufisadi kuvunja sheria na kutofuata kanuni ni jambo la kawaida kabisa kwa ccm,miradi yote ya chama hiki haikinufaishi chama hata mgombea wa nafasi ya njumba kumi kumi lazima avunje kanuni,amini nawaambia CCM kwa mwendo huu mtatuletea machafuko makubwa na hayata koma.Vijana wa CCM mko wapi angalieni Tanzania kwa Jicho la mbali zaidi.
 
Itakapo timu saa tatu kamili usiku kutakuwa na kipindi maalum chanel ten cha safari ya matumaini.
Watarusha toka mzee Lowassa atangaze nia pale arusha na sehemu zote alizopita kusaka wadhamini bara na visiwani mpaka hatua ya kurudisha fomu dodoma.

huyu fisadi ana jeuri kweli
 
Sasa hivi saa tatu dakika 12 hamna dalili ya Lowasa kurushwa, au sio saa tatu ya leo.

Kuna kitu wameshtuka si bure!!! Kama kweli walikuwa na mpango wa kufanya hivyo basi naona washauri wake wamepania kumpa enough rope vile.....
 
Back
Top Bottom