Kipindi cha talaka/divorce

pole sana mkuu
kumove on inategemea na wewe mwenyewe ila uwahi uchelewe litapita tu mtegemee Mungu na usali sana natumai hutochukua muda kuendelea na maisha yako.
Asante sana sana
 
Sawa asante
 
Bless you [emoji122]
 
Kaomba talaka au ww ndio unatoa?!

Ni vizuri kama mmeamua kupeana talaka basi ukawa unaishi mbali naye itakusaidia kuzoea hali ya kuishi mwnyw mpaka ikifikia mida talaka imeshakuwa official inakuwa ni kugawana mali tu


Kuhusu mida gani inachukua inategemea inategemea kama mnapeana mahakamani au bakwata kama ni muislam kujadiliana mgawanyo wa mali ndio kunapoletaga matatizo lakini km unaamua kukubaliana na anavyotaka process inakuwa fupi tu.


Pole sana.
 
Tatizo kwa jamii zetu za kaifrika hizi ni jambo geni kwahiyo kama utatalikiana na mumeo na kwa bahati mbaya sana maisha yakakulazimisha uwe yegemezi aiseeeee utajuta kuzaliwa , sio mitusi aliokuwa anatukanwa dada yangu ile duuuuh hadi alitamani dunia ipasuke adumbukie na kupotea kbs. Baada ya mwaka na nusu ikabidi aende chuo akaja kuwa na maisha yake ya kujitegemea mwenyewe kidogo ikampa unafuu. Jambo la ajabu sana ana mimba na fununu zinasema ni mimba ya yule yule alietalikiana nae yapata miaka nane kumi iliyopita
 
Jiulize swali;
Kwa nini napewa/naitaka hii talaka?? Kama mtu wako kakuchoka, angalia pia kilichomfanya kakuchoka. Penzi halizeeki bali hukua kila siku. Ilitokea nini?? Habari za kuvumilia ati hili nalo litapita tu sio kweli. Hatuvumilii kwenye penzi bali huwa tunalidai penzi letu. Ukifika pale mahakamani kataa hiyo talaka kuwa kama yeye kakuchoka, wewe hujamchoka.
Hizo dhiki unazoziona sasa ndio zitakuja kuwa msingi wa raha, furaha na amani baadaye. Kitu pekee cha kuchunga ni kuwa, isijekuwa pendo lako limeingiliwa na vijimambo vya nje. Hakuna ugomvi usio na suluhu. Mahakama itawapeni muda wa kujitathmini. Huo ndio muda wako wa kujitathmini. Kama jamaa amezamia kwa nyumba ndogo, wala usimpigie kelele. Mpe haki yake siku huko nyumba ndogo kuna matope tena kwa ufundi mkubwa bila kelele na kebehi. Wanawake wengi midomo yenu ndio inawaponza.
Mwisho jiulize; Labda alikukuta bado msichana, akakutoa usichana wako, amesha kukutotoa toto 2, 3, 4. Leo umesha kongoroka na ukichanganya na unayosema mateso kama ukiingia bafuni huwa unahofu kujianglia. Sasa unataka kwenda wapi?? Nasema; Komaa naye hadi bp imuue kwani akienda kazini akirudi akukute na bonge la tabasam na sifa kem kem kuwa hakuna dume ka wewe uliyenitoa usichana wangu. Imba hadi sikio lake liizoee sauti yako. Hakuna talaka kwa mkristo
 
Kwanza inabidi hizo tofauti zenu ziwe zimefika kwa wasimamizi, wakashindwa kutatua, wazazi nao wawe wameshirikishwa wakashindwa kusuluhisha. Baada ya hapo unaenda ngazi ya wazee wa kata (afisa mtendaji) mtaitwa na kusuluhishwa, ikishindikana mnapelekwa kwny baraza la usuluhishi nao wakishindwa ndo mnaenda mahakamani.

Mdai talaka anapeleka shauri mahakamani, alafu anapewa barua/taarifa kumpelekea mtalikiwa ya kuitwa mahakamani. Siku ya mahakama kusikiliza kesi yenu, mnaulizwa maswali mengi tu ikiwemo kwa nini mna talikiana/kwa nn mdai talaka anataka talaka, alafu wazee wa usuluhishi pale mahakamani wanatoa maoni yao..

Kama mna watoto mnaulizwa mtawatunzaje/ wanaenda kuishi na nani kati yenu. Mnaulizwa mali mlizochuma pamoja na jinsi ya kugawana then mkishakubaliana hukumu inatoka siku hiyo hiyo na talaka inatoka. Ila wengi wanachukua muda mrefu kutokana na mgawanyo wa mali maana wengi hawako tayari kugawana.

Khs kumove on, hapa inategemea na wote wawili, je mmejiandaa na kutengana? Kama unashindwa ku move on inabidi mtengane kwa kipindi chote cha process, mpeane nafasi. Hii itasaidia kuzoea hali ya utengano.
 
Mtaalam... husitumie akil nying kwenye mambo madogo....
Hapo kinachokupa shida ni ile hali ya kujihisi hupendwii... hvyo una kiu kikubwa cha kupendwa...
Chakufanya:
Mtafute kijana aliyekuwa anaonyesha anakupenda saaaana... hata kama ww humpend... hlf ingia kwenye mahusiano nae....
Amin husiamin atakusaidia sana kukuvusha kwenye hlo daraja...
Akimaliza kazi yake.. mteme.
 
Hapo ndo ukute ndugu ndo mlikuwa kiherehere wakati wanatalikiana,hapo lazima mtafutane kwa tochi
 
Ushauri mzuri sana,Mungu akulinde
 
divorce kama divorce kwa mtoaji (MDAIJI) yeye anakuwa amejiandaa ki psychology so haitamsumbua sana. kwa wewe unayepokea kuna changamoto zake nyingi....mara nyingi anayetoa/dai maana yake ana utayari wa ku move on either alone au kuna mtu ambaye yupo japo si kwa watu wote.
talaka sio mwisho wa maisha .cha msingi cha kwanza kukubali yaliyotokea ili ukubaliane na kila kitakachofuatia baada ya hapo. ila uki resist any thing at that moment nguvu yako ya kusonga itakuwa ndogo mno.
cha msingi kukubali matokeo .
 
Mwombee ushauri mchepuko wako EM
 
Fikiria furaha yako kwanza cha muhimu usiwe na roho ya chuki na kinyongo hutoweza ku move on epuka migogoro isiyo na tija usigombee vitu visivyo na tija wengi hugombeamali hasa nyumba kumbuka unapewa talaka hujakatwa mikono amani yako ni muhimu sana go kanisani or msikitin jichanganye na watu usipende kuliongelea swala la talaka yako kwan hutolisahau kirahis jitahid kufanya activitieszinazokufurahisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…