Kipindi cha Take One cha Clouds Tv chafungiwa miezi mitatu

Kipindi cha Take One cha Clouds Tv chafungiwa miezi mitatu

vantz

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2016
Posts
1,107
Reaction score
570
Take one.jpg


Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia kwa miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo hicho.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

“Clouds tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema Mapunda.

Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00
 
Hiki kituo kinasifiwa sana na wakubwa zetu, inakuwaje mara kwa mara kinafungiwa?
Wote ni wale wale tu, nawashauri TCRA waachane na hiyo station maana anayehusika ataishia kutumbuliwa tu
 
Zamaradi tena.Alipokosolewa kwa kumuhoji Kaoge alitoa maneno ya kukera.Sasa kakosolewa tena.Kumbe yeye ndo tatizo.
 
Zamaradi kwa vile kazaa na Ruge anajihisi hamna wa kumpangia maisha pale klauz anatukana wafanyakazi wenzie, anajisifia Ruge kamuweka mkononi ndo mana hata Joe Kusaga hawezi kumfukuza kazi.
 
me nadhani wangebadilisha muda wa hicho kipindi ili ajimwaye mwaye
 
Back
Top Bottom