Kipindi cha Redio: Mafanikio ni moyo. Soma hapa liz

Radio Producer

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
724
295
KIPINDI: MAFANIKIO NI MOYO​

Script

Sing tune:_fade up_______fade down and then fade out 00:20
Karibu tena ndugu msikilizaji; katika kipindi chako cha mafanikio ni moyo ambacho huandaliwa na kuletwa kwako nami Radio Producer. Daima kila binadamu awaye yeyote katika dunia hii, awe maskini au tajiri neno mafanikio huwa halikosi kuimba ndani ya moyo wake, hasa anapokuwa na akili timamu! Wengine wanashindwa kuelewa maana halisi ya mafanikio, wengine wanadhani mafanikio ni kupata pesa nyingi na kuzitumia kwa anasa wapendazo. Ukweli halisi tutauona ndani ya kipindi hiki ambao utatuelekeza sehemu muhimu tunayohitaji kuielewa katika mafanikio. Kama kawaida ya kipindi chetu, kwa sasa tuanze ka kusikiliza wimbo mfupi kabisa kabla ya kuingia katika kipengele kingine, nakusihi twende pamoja.

WIMBO: MTAJI WA MASKINI BY MWIJUMA MUMINI 02:00

Ama kweli mtaji wa maskini unatoka katika nguvu zake mwenyewe! Ni wimbo mzuri kweli kweli unaoweza kutupa mwanga mpana wa jinsi ambavyo tunaweza kupata mtaji. Mafanikio ni neno linalojumuisha mambo mbalimbali, kufanikiwa ni pamoja na kuishi kwa amani, upendo na ushirikiano na jamii kwa ujumla. Hata hivyo tabia ya mtu ni chanzo kikubwa cha mafanikio yake. Izingatiwe kuwa mafanikio siyo tu kama wengine wanavyofikiri kuwa ni kuishi maisha ya raha na starehe bila kukumbana na matatizo mbalimbali ya kimaisha. Wataalamu wengi wanasema ukishindwa sana katika mafanikio utakuja kufanikiwa sana. Kila unapoanguka unajifunza, kwanini nilianguka! Itakusaidia mara nyingine kujichunga usianguke! Ndugu msikilizaji inawezekana umeanzisha biashara nyingi sana, lakini hujafanikiwa umekuwa ni mtu wa kushindwa, usikate tamaa kwani hakuna mafanikio yasiyo na vipingamizi.
Hapa studioni katika siku ya leo tunaye mtu mgeni ambaye atajitambulisha jina lake na sisi
tumsikilize mwanzo mpaka mwisho, yeye yuko wapi katika suala la mafanikio na tutajifunza nini kwake!

BREAK INSTRUMENTAL: FADE OUT AFTER 20 SECONDS.

Mgeni: Kwa jina naitwa Maamzi Mafanikio, ni mzaliwa wa mkoa wa Shinyanga, kijiji cha Mahembe na sasa naishi jijini Da es salaam. Asante ndugu mtangazaji wa kunipa fursa hii kuwaeleza wasikilizaji jinsi ambavyo mimi niliweza kujikwamua kimaisha na hatimaye kufanikiwa!

Kwanza kabisa nikiwa kijijini miaka ya 1996 nilikuwa nikiishi na wazazi wangu, tulikuwa na maisha mabaya sana ambayo hata leo nikiyakumbuka machozi huwa yananidodoka! Familia yetu ilikuwa ya watu watatu tu. Mimi baba na mama. lakini usingeamini maisha mabaya tuliyoishi. Kulala kwetu wote kulikuwa kwa shida, ngozi za ng'ombe ndiyo tulilia. Hili lilinipa shida sana kuwaza kichwani mwangu! Wakati huo mwisho mwaka huo wakati nilipokuwa na umri wa miaka 18, niliamua kuondoka nyumbani na kwenda kufanya kazi za uchimbaji madini kwenye machimbo yaliyoko Mwakitolyo mkoani Shinyanga. Hata hivyo nilitoka kwa nguvu kwani wazazi hawakuwa tayari kuniruhusu. Ilinilazimu kufanya hivyo kulingana na msukumo wa moyo wangu wa kujitafutia. Nilipofika machimboni nilijituma sana na kuweza kufanikiwa kupata pesa kiasi cha laki 5 kwa muda wa miezi mitatu. Nilifurahi sana nikatamani nirudi nyumbani ili nikanunue ng'ombe na kuwa mfugaji. Usiku wa mwisho kulala machimboni ghafla nilisikia mlango umevunjwa katika nyumba niliyokuwa naishi. Watu watatu waliingia na kunitaka nitoe hizo pesa haraka sana. Nilijaribu kukataa lakini nilipata kipigo kibaya sana. Ilibidi niwape lakini hali yangu ya afya sasa ilikuwa mbaya mno kwani nilikatwa panga kiganja chote cha mkono wangu. Sikuwa na msaada wakati huo, ila nilikaa kama mwanaume nikachemsha maji na kuyaweka chumvi baadae nikauosha mkono wangu na kujifunga kanga, hadi kesho yake nilipoenda hospitali kwa matibabu! Matibabu hayakua mazuri sana kwani sikua na pesa, ila nikwambie msikilizaji kama Mungu bado anakulinda hata kama utumbo utoke nje wote hakika hautakufa.
Ilinichukua miezi mitano kupona kisawasawa lakini sasa sikuwa na ujanja kwani kono wa kushoto ulikua butu. Niliamua kwenda mjini Shinyanga na kuwa mtu wa mitaani. nilijaribu omba omba ikanishinda. Siku moja nikiwa nimelala niliijiwa na wazo baya sana la kuiba! Usiku huo huo niliamua kwenda kijiji jirani kwenda kuvunja duka. Bahati haikuwa yangu nilikamatwa na kupigwa vibaya sana, cha ajabu wakati wanachi wameamua kunimalizia kwa kunichoma moto, walikosa mafuta ya taa wakaamua kukusanya karatasi na majani wakanirundikia na kupiga moto. Ghafla milio ya bunduki ilisikika wakakimbia wote. na mimi nikainuka kwa shida na kukimbia. lakini nilienda kuanguka kwenye shimo moja nikaumia vibaya sana! Maisha haya, nililia sana nikawakumbuka wazazi wangu na jinsi mawazo mabaya yalivyonijia. Sasa nimebahatika kupona, madonda tele, makovu mengi nimepigwa vibaya. Nilienda kwenye familia moja nikaomba chumvi kidogo wakanipa nikaendwa kwenye bwawa moja nikaoga na kujipaka chumvi hiyo, sijawahi kusikia maumivu makali kama hayo. Jaman dunia hii! Baada ya hapo nilifikiria sana, nakujisemea sitaiba tena. Nilipopata nguvu niliamua kwenda mbugani maeneo ya Busia Shinyanga huko kulikuwa na matango mengi sana yakujiotea. Nilienda na mfuko nikafanikia kuchuma debe mbili ambazo nilizibeba kichwani. Nilipofika mijini Shinyanga nilifanikiwa kuuza mzigo wote na kupata Tshs 1,000. Hii ilikuwa kazi yangu kila siku hadi siku matango yaliisha mbugani, nilijikuta nina Tshs 10,000/=.. cha ajabu sikuzigusa kabisa niliendelea kulala mtaani, kula matango na kubahatisha ninapokuwa nimeenda kijijini. Nashukru Mungu ka sababu tabia yangu ilibadilika na kuwa nzuri. Baadae nilianza biashara ya kufuata matunda kijijini na kuuza mjini kwa usafiri wa daladala. Hadi msimu wa kilimo unafika mwaka 1999, nilijikuta nikiwa na Tshs 50,000/= mfukoni na kwenda hyumbani kwa ajili ya kilimo. Hali ilikuwa mbaya sana nyumbani, njaa niliwapa nusu ya pesa wakanunua chakula nyingine nikalima ekari 5 za mahindi. Wakati wa mavuno Mungu alisaidia nikapata gunia 20, nikauza wakati wa msimu wa mauzo na kupata laki 2. Kwa kuwa msimu ulikuwa umekaribia nililima tena ekari 20 kwa hiyo hela kuja kpata magunia 100. Niliuza na kuapa milioni moja na nusu. Nikanunua mashine mbili za kusaga. Ndugu yangu baraka zilifunguka. Nikaendelea na kilimo ambapo mpaka sasa mimi ni mkulima nalimia shinyanga, nina ekari 100 mbugani na kila mwaka navuna zaidi ya magunia 500. Nimefungua kiwanda cha kutengeneza mbao porini. Makadirio ya chini pato langu la mwezi ni milioni 50. Nimejenga nyumba kwa wazazi wangu nzuri sana, solar nimweka, mwenyewe nina nyumba nzuri sana hapa dar. natarajia kujenga hoteli kubwa ya kitalii Arusha. ni mengi sana mtangazaji ila leo nikomee hapa.

Ndugu msikilizaji muda wetu umetutpa mkono, nina imani umejifunza chochote. Kwa maoni na ushauri weka maoni yako hapo chini. Asanteni.
 
Kipindi ni kizuri mno na naahidi nitakuwa nakisikiliza kwa umakini sana ili niweze kujifunza kama nilivyojifunza hapa ya kwamba hatutakiwi kukata tamaa.je? Kipindi kinurushwa kila cku ipi ili niweze kukisikiliza.
 
Usijali ndugu yangu, ratiba utaipata kamili tunakiandaakikae fresh!
 
Back
Top Bottom