Elections 2010 Kipindi cha Dk Slaa kilichokuwa kirudiwe chaahirishwa

emmathy

Senior Member
Sep 22, 2010
147
25
Nimekuwa nikisubiria marudio ya mdahalo wa Dr slaa kupitia ITV usiku huu ila nimekutana na tangazo kuwa hayatakuwepo, badala yake naona mieleka
 
Hawa Itv vipi?Siku nzima wamekuwa wakitudanganya wasikilizaji wao kuwa watarudia mdahalo saa 4.45 usiku.Sasa wanaomba radhi ati mdahalo hautarudiwa leo,bila hata ya kutoa sababu na bila hata ya kueleza ni lini watarudia kama walivyosema awali.

Nina wasiwasi mkubwa na kinachoendelea hapa,there's somethin fishy.It's not a technical issue,It's a political stake.
Kina makamba wamefanya juhudi zote kitu kisirudiwe maana wanajua moto wake!
Kitaeleweka tu,...No turning back!
 
walisema wataonyesha saa nne na dkk 45 ilipofika wakaweka mieleka.....sijui wamepigwa mkwana na jk
 
Mafisadi wameshawapa mshiko itv wasionyeshe marudio ya mdahalo wa Rais Dk Slaa. Nimeumwa na mbu bure kungojea kipindi.
 
Wameamua kutuburudisha na akina John Cena. Lakini ujumbe uwekwisha enea kama moto utavunavyo nyasi kavu. Kwa hili linalofanyika linawatia hamasa waloshindwa kushuhudia yale mahojiano kuwa na kiu ya kutaka kusimulia zaidi na kilichojili; na kwa hamu hiyo inawafanya wawe na hasira ya kinachoendelea. Lakini haya yote yana mwisho wake.
 
ITV acheni u**********, nimeacha shughulizangu halafu mnaniwekea mieleka
 
dk.slaa slow down u killin'em...yani mwaka huu hawatousahau hawa genge la majambawazi wa thithiemu!? HAT DOWN,I BOW TO U DR., U REALLY GOT EM THIS TIME AROUND
 
Taarifa zilizotoka katika chumba cha utangazaji cha ITV zinasema Mda mchache uliopita wamepigiwa simu Joyce Mwavile kuwa wasitishe kukirusha kipindi hicho.

Baada ya kudadisi asubuhi nimeambiwa asubuhi Riziwani alitinga katika ofisi za ITV na kukutana na watu kadhaa. Alipotafutwa Steven Chuwa ambaye alikuwa amelala nakumuuliza habari hizo akajibu kuwa watu hawa wamefanya usanii flani japo hakutaka kuwa wazi.

Baada ya kupiga chumba cha utangazaji wao walikuwa wamepitisha taarifa ya kuomba radhi, Tanzania hii lazima tuikomboe.

Taarifa nyingine muhimu ni kuwa Kikwete anatarajiwa kuwa Live kesho asubuhi Star TV katika jiji la Mwanza kuanzia saa 1:30 kwa kipindi kama alichofanya Dk Slaa. Hizi habari zimekuwa za kificho na tayari amewaamuru watangazaji wa Star TV kutoruhusu maswali magumu, Mtu huyu amekuwa anapanga mpango huu kwa kutokuwa wazi mpaka sasa haijulikani kama itakuwa hivyo.

Ndugu wana JF tujiandae......
 
uuuwi mbona huyu jambawazi anatapatapa sana?......anyway mwisho wake ni jumapili
 
Wapuuzi kweli hawa ITV, wamenifanya nikae kusubiri huo mdaharo na hawauonyeshi, pumbavu zao kitaeleweka 2 mwaka huu
 
Duh, poleni. Hakuna kulala wala kukata tamaa. Hii ni vita dhibi ya Mafisadi na umma waTZ. Sikilizia hiyo wanaahirisha matatizo. Hiyo nguvu ya umma huwezi kuizuia.
 
Hawa Itv vipi?Siku nzima wamekuwa wakitudanganya wasikilizaji wao kuwa watarudia mdahalo saa 4.45 usiku.Sasa wanaomba radhi ati mdahalo hautarudiwa leo,bila hata ya kutoa sababu na bila hata ya kueleza ni lini watarudia kama walivyosema awali.

Nina wasiwasi mkubwa na kinachoendelea hapa,there's somethin fishy.It's not a technical issue,It's a political stake.
Kina makamba wamefanya juhudi zote kitu kisirudiwe maana wanajua moto wake!
Kitaeleweka tu,...No turning back!

Kwani wao hawajipendi hadi waseme ni nani aliyekataza mahojiano na Rais Mtarajiwa kutorudiwa? Inajulikana wazi ni nani, hao ITV wameshatishiwa labda wanaweza kunyang'anywa leseni yao kama wakiyarudia.Tuwape kazi nzito ya kuiba kura kwa kuwapigia wabunge wa chadema na Rais Mtarajiwa kwa kishindo
 
ITV, tujulisheni marudio yatakuwa lini? ile Jmosi tuliwapa big-up sana, msituangushe sasa. Hivyo ndio vipindi vyenye soko, mtuambie na kuadvertise kabisa, lini mtafanya marudio.
 
Kwani wao hawajipendi hadi waseme ni nani aliyekataza mahojiano na Rais Mtarajiwa kutorudiwa? Inajulikana wazi ni nani, hao ITV wameshatishiwa labda wanaweza kunyang'anywa leseni yao kama wakiyarudia.Tuwape kazi nzito ya kuiba kura kwa kuwapigia wabunge wa chadema na Rais Mtarajiwa kwa kishindo
wanaogopa bure hawa itv! hawawezi kunyang'anywa leseni na chama cha upinzani....chichiem kitakuwa chama pinzani kuanzia 01112010. chama tawala i mean CHADEMA watasimamia haki na uadilifu hivyo mtu anayetenda haki na anatangaza matangazo yake kwa haki hatafungiwa na chombo chochote chini ya serikali mpya.......
kama wanasaidiana kuiangusha mission hii ya KiMungu watashindwa na nataka tu wajue kuwa nchi nzima wameahirisha kulala wanasubiri kipindi hiki ambacho kimeahirishwa bila kutaja sbb, for sure unaongeza idadi ya maadui, kura za ccm zinapungua kila siku....kuna watu waliokiacha chama hicho kwa issue ya shibuda na sasa wanaongezeka.
 
nai nmeshangazwa kwani nilikimbilia home nkjua mambo shwari leo ntalisten kwa utulivu ghafla John Ceana anatawala, well haitutishi hata kidogo haya yana mwiso, JK yeye kaamua kurushwa na dialo wake mz, well haitomsaidia, watz tuchange irushwe hata cnn,bbc, why hakuna coverage from those media?inaskitisha sana!
 
Back
Top Bottom