Kipindi cha dakika 45 ITV ni jukwaa la kisiasa?!

babangweta

Member
May 20, 2011
11
1
Kipindi cha dakika 45 pale ITV ni kama jukwaa la kisiasa la wanasiasa kutangaza sera zao kwa sababu mtangazaji hana uelewa wa maswali anayouliza hivyo kuwaacha jamaa wanajimwaga tu na majibu ya uongo. Mfano wa karibu ni jana ambapo Mh. Kasimu Majaliwa alipokuwa anadanganya kuwa wanasimamia Halmashauri wasihamishe vifungu vya matumizi wakati ni mwaka jana tu vifungu vilibadilishwa kwa agizo la waziri mkuu la kila halmashauri lazima inunue powertiller 50 wakati mpango haupo kwenye bajeti. Vilevile Idara ya elimu msingi imelazimishwa kupeleka watoto kwenye mashindano ya kitaifa ya UMISHUMTA kwa agizo la TAMISEMI wakati mpango haupo kwenye bajeti iliyopitishwa.
 
Ni kweli hicho kipindi mimi hua sikiangalii kabisa baada ya kugundua uwezo mdogo aliyonayo mtangazaji wa kipindi katika kuwauliza washiriki maswali,wakati mwingine kama vile anaogopa kitu fulani,uongozi wa ITV umbadilishe.
 
Back
Top Bottom