Kipindi cha Dakika 45 ITV: Wakati umefikia sasa kuruhusu maswali kwa wageni waalikwa

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
10,441
12,862
Wanajanvi.

Hiki ni kipindi kizuri sana. Ni kipindi cha muda mrefu na maarufu hapo ITV.

Wanaalikwa watu wazito wenye maslahi kwa umma! Mwandaaji wa kipindi bi Farhia anajitahidi sana kauliza maswali fikirishi kwa wageni wake.

Hata hivyo kipindi kinakosa mvuto. Ni cha upande mmoja. Muulizwa maswali anabaki akitamba peke yake bila kuulizwa maswali chokonozi.

Yaweza kuwa anapewa maswali au hata kuandaa maswali ya kuulizwa! Hatujui.

Wakati umefika sasa kuruhusu hadhira iulize maswali kwa njia mbalimbali ili kuleta tija zaidi.

Itapendeza zaidi kwa jina la jamhuri!

Alamsiki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom