Kipindi cha CHEREKO kupitia TBC1

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,985
Reaction score
25,374
TBC1 ni televisheni ya Taifa, hivyo tunatarajia vipindi vyenye manufaa kwa Taifa la Tanzania kuonyeshwa kwenye 'televisheni ya Taifa'.

Kuna kipindi kimoja kinaitwa CHEREKO ambacho kimekuwa kikirushwa kupitia TBC1 kwa muda sasa. Hivi kipindi hiki kinaifundisha nini jamii hasa? Ni kina nani walengwa wa kipindi hiki?--maana sijawahi kumuona wife wala babysitter akitazama hiki kipindi. Hata mtoto wangu wa kindergaten sijawahi kumuona akitazama kipindi husika.

Kwa sababu elimu ya watoto wetu iko taabani, nashauri kipindi hiki kifutwe, kwa kuwa hakina tija kwa taifa, badala yake vipindi vinavyohusu taaluma (kama vile vinavyoandaliwa na kuonyeshwa Star TV) vichukue nafasi yake.
Nawaza tu.
 
mkuu kumbe unakereka na hii program kama mimi pia!!

Mimi sishauri wakiondoe bali wakiweke usiku wa manane na kipindi cha elimu kiongezwe kwenye schedule yao!!
 
Huwezi kuchukia ww kitu na wenzako iwe hivyo kina washabiki wengi tuu mbona
 
Uwiii!!! kwetu hiko kipindi kina mashabiki sema kimedorora siku hizi kidogo ila sema tu hapo kwako na wachache wa aina yako hawakipendi.....ukisema kifuttwe unakosea sababu kila mtu na taste yake....Nimemaliza swahiba.
 
kwa hiyo wife wako na beki 3 wako ndo wanawakilisha watanzania wote? kwanza ulijuaje kuna hicho kipindi na kwamba hawaangalii kama wewe huangalii! hawaangalii kwa sababu muda huo unakuwepo ..beki tatu gani atakaa kwenye tv na boss wake jamani..wanacheki marudio alhamis
 
Walengwa wakuu wanakipenda kipindi hicho, binafsi sina muda kabisa wa kukaa eti naangalia Chereko ila Mamushka yeye anapenda.Ukiona mpaka watu wanalipia airtime na kuongeza kipato cha shirika basi tukubaliane kuheshimu uhuru wa kuchagua kwani kwa upande mwingine wapo wanaokerwa na kipindi cha- "This Week In Perspective". Kwa upande mwingine TV ya taifa si lazima ielimishe bali burudani pia.Mimi wakirusha mechi ya Mbeya City ninapenda sana but mwenzangu hataki kabisa mambo ya mipira.Out of that, nakushauri uwe flexible kama mie kwani mpaka niangalie TBC 1 ujue ni mpira au kipindi educative vinginevyo mpaka nasahau kama tuna TV ya taifa!
 
Uwiii!!! kwetu hiko kipindi kina mashabiki sema kimedorora siku hizi kidogo ila sema tu hapo kwako na wachache wa aina yako hawakipendi.....ukisema kifuttwe unakosea sababu kila mtu na taste yake....Nimemaliza swahiba.
ni kizuri wanarudia sana harusi ndo tatizo ila kinafaa wadau tupo
 
Bora alivyokuwa akitangaza angela ila shamim ananiboa na kurudia harusi mwanzoni ilikuwa sikosi ila now sina mzuka nacho
 
Mm binafsi ni mshabiki wa hki kipindi lakini now days kinaboa sio kama mwanzo alipokuwa anakiendesha yule dada mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…