Kipimo cha CT-scan chaharibika muhimbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipimo cha CT-scan chaharibika muhimbili

Discussion in 'JF Doctor' started by mgomba101, Oct 30, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kipimo cha ‘CT-Scan’ katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kimeharibika na kusababisha usumbufu mkubwa kwa baadhi ya wagonjwa wanaoandikiwa kwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyika kipimo hicho.

  Kutokana na hali hiyo, NIPASHE ilishuhudia jana wagonjwa mbalimbali wa MNH pamoja na wale wanaotoka nje ya hospitali hiyo walioandikiwa kupimwa kwa kutumia kipimo hicho, wakishauriwa kwenda katika hospitali nyingine.

  Pia NIPASHE ilifika kwenye jengo linalotumiwa kwa ajili ya kipimo hicho na kumkuta mfanyakazi mmoja aliyekuwa mapokezi, ambaye licha ya kukataa kutaja jina lake, alijibu kwa kifupi kuwa kipimo hicho kimeharibika kwa muda mrefu sasa.

  Afisa Habari wa MNH, Aminieli Algaesha, hakupatikana ofisini kwake na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi, iliita bila ya kupokelewa.

  Mkurugenzi Mkuu wa MNH, Dk. Merina Njelekela, alipotafutwa kwa njia ya simu, na kuulizwa kuhusu kuharibika kwa kipimo hicho, hakukiri wala kukataa, badala yake, aliomba apigiwe baada ya muda mfupi. Hata hivyo, alipopigiwa simu yake haikuwa na majibu.

  CT-Scan iliharibika mwishoni mwa mwaka jana na kutengenezwa katikati ya mwaka huu, ambapo katika mgomo wa madaktari, wa Februari na Juni mwaka huu, moja kati ya madai yao, ilikuwa ni kutengenezwa kwa kipimo hicho.

  Madaktari hao pia waliitaka serikali kukifanyia kipimo hicho matengenezo ya haraka na kudai gharama yake ni sawa na gari moja la kifahari linalotumiwa na mbunge.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wana JF naomba tujadili kuhusu hospitali yetu ya muhimbili kukosa hiki kifaa! Dhaifu na genge lake wao wakiumwa hao india,sisi walalahoi tunateseka hapahapa bongo.
  Kuna mabilioni yetu yako huko bank za uswisi,tushinikize zirudishwe nchini zisaidie sekta ya afya na elimu.
   
 3. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kwani CT-Scan imeharibika leo??..while at MNH huwa ni 100,000/=Tshs it's almost 390,000/=Tshs at other centres (Private hospitals).

  Anyway, tufanyeje sasa ndio tumeridhika wenyewe..pole kwa wagonjwa.
   
 4. Mavindozii

  Mavindozii JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 20, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 60
  Hapa USA ni $3000
   
 5. Mavindozii

  Mavindozii JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 20, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 60
  MRI ni $4000
   
 6. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Halafu mkuu, ukisema wafanyie jirani, utaambiwa eti tuna wapeleka katika hospitali zetu...ukiwambia waihimize serikali kununua CT-Scan na MRI machines hawataki!!
  Na hii ndiyo Tanzania yetu tuipendayo.
   
 7. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Hizo za usa sio sawa na za bongo za kwetu ni kuu kuu model ya zamani kama gari ni pijot au land rover za kizaman zile,, but za huko usa ni modern machines... Si unatujua wabongo kwa kununua used and expired product kama mweli za mv skagit
   
 8. s

  sawabho JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Nashindwa kushangaa Serikali ambayo ndio mmiliki wa rasilimali za nchi ikiwa ni pamoja na mapato yake yote, inakosa kipimo hicho ilhali hospitali za binafsi kinapiga kazi siku 3651/4 !!!!
   
 9. F

  Fofader JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Je ni mambo ya kutotulia kwa umeme wetu? Maana umeme ni tatizo kubwa kwa equipment kama hizi ambazo ziko precise sana. Au ni mambo yetu ya kutofanya preventive maintenance? CT scan hoi, rada hoi, ndege zinashindwa kuruka n.k. Angalau subway inafanya kazi ingawa kwenye ile safari ya kwanza injini ilizimika kwa kuingia upepo!
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  mkuu sawabho hakuna Serikali kuna jina tu la Serikali huyu Waziri wa Afya anafanya kazi gani huko? Rais kamteuwa waziri feki wa afya hashughulikii hilo tatizo la kuharibika kwa hiyo Mashine ya CT-scan ohhhhhhh nchi haina viongozi wabovu nchi yenyewe ni mbovu basi nchi inakwenda kama behewa la Treni lililo kosea njia .
   
 11. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kataka hali ya sasa hivi hospitali bila ya CT-Scan,MRI ni janga kubwa na kiukweli inakua haija kamilika. Huwa na jiuliza maranyingi sana nijinsigani wagonjwa wengi tuna wapoteza kwa kukosa vipimo hivi. Nina uhakika uki fanya utafiti mkubwa tutagundua wagonjwa wengi wanakuwa misdiagnosed na kupata either way matibabu yasio sahihi au yaliyo pungufu.
  Kuna umuhimu wa madaktari kujipanga vyema na kwa pamoja na kulipigia kelele hili. Wananchi wa kawaida hawajui nini thamani ya CT katika afya zao na wamekuwa mashabiki wa siasa tu na kushabikia rushwa za hapa na pale ilihali baadae wanakuja kuambulia patupu. Waandishi wa habari mnaangaika kumuhoji mkurugenzi mara mtumishi mnashindwa kwenda na kumuhoji mwinyi. Hawa watendaje mtawaonea bure. Sera mbovu za serikali na mis-allocation of funds ndio chanzo kikubwa cha janga hapo TZ
   
Loading...