Tumezoea kuwa wanafiki, unaamini hivi kinywani mwako unaongea vinginevyo. Namuheshimu Tindu Lissu kwa sababu anakisema kile anachokiamini, mimi binafsi sikuyapenda sana maneno ya Lisu ya kumkashifu Mwalimu lakini hivyo ndivyo Lisu anavyoamini na anasema anachokianmini tofauti na wengi wa viongozi wetu wengi wanaojifanya ni waumini wa Mwalimu wakati hawaishi yale aliyoyaamini Mwalimu, ni wezi, walafi, wabinafsi, mafisadi, wanyonyaji kama walivyo wajumbe wa bunge la katiba kule Dodoma. Najua angekuwepo Mwalimu leo lile bunge la katiba lingekuwa limesha sambaratishwa kwa sababu ule ni mradi wa kufisidi kodi za wavuja jasho wa nchi hii ulioratibiwa na Ikulu yenyewe - hakika ni wizi mtupu - shame upon you.