Kipi nyuma ya siku ya kuzaliwa


MLALUKO JR

MLALUKO JR

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2015
Messages
970
Likes
280
Points
80
MLALUKO JR

MLALUKO JR

JF-Expert Member
Joined May 3, 2015
970 280 80
Habarini wanaJf
Poleni kwa wote mliokumbwa na matatizo na mikasa mbalimbali mfano;kutumbuliwa na kufukuzwa km machinga!

Pia niwapongeze wale wote walio/wanaozidi kufanikisha ndoto zao ktk maisha,"Ni jambo la kumshukuru Muumba"!

Kutokana na mada husika napenda kujua,kuna usahihi gani kusherehekea Birthday ingawaje hatujui siku hiyo ilikuwaje na wala hatujui kilitokea nini, Je tunakumbuka nini?

Na je,kipi tunachokifurahia siku hiyo either kuja duniani au kuendelea kuishi na kupunguza siku zetu?

Je, nani au jamii gani iliyoanzisha suala hilo na kuturithisha?

Tujuzane wadau!
 
corasco

corasco

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2016
Messages
2,735
Likes
2,073
Points
280
Age
49
corasco

corasco

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2016
2,735 2,073 280
Binafsi sina upuuzi wa kusherekea hivyo vitu
 
Mhusika mkuu

Mhusika mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2013
Messages
273
Likes
148
Points
60
Mhusika mkuu

Mhusika mkuu

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2013
273 148 60
Sikukuu ya Kuzaliwa

Maana: Siku ya kuzaliwa kwa mtu au ukumbusho wa siku hiyo. Katika sehemu mbalimbali sikukuu ya kuzaliwa kwa mtu, hasa kule kwa mtoto, husherehekewa kwa kufanya karamu na kutolewa kwa zawadi. Hilo si zoea la Kibiblia.

Je, Biblia inapotaja kuhusu sherehe za sikukuu ya kuzaliwa, inaonyesha kwamba zinafaa? Biblia inataja sherehe mbili tu za aina hiyo:

Mwa. 40:20-22: “Basi siku ya tatu ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawafanyia karamu . . . Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji kwenye cheo chake cha kunywesha . . . Lakini akamtundika mkuu wa waokaji.”

Mt. 14:6-10: “Sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode ilipokuwa ikisherehekewa binti ya Herodia alicheza dansi na kumpendeza sana Herode hivi kwamba akaahidi kwa kiapo kumpa chochote kile ambacho angeomba. Ndipo yeye, chini ya mwelekezo wa mama yake, akasema: ‘Nipe hapa juu ya sahani kichwa cha Yohana Mbatizaji.’ . . . Akatuma watu wakamkate Yohana kichwa huko gerezani.”

Kila jambo katika Biblia limo humo kwa sababu fulani. (2 Tim. 3:16, 17). Wakristo wa kweli huepuka sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kwa kuwa wanafahamu kwamba Neno la Mungu hutaja mambo yasiyofaa kuhusiana na sikukuu hizo.

Wakristo wa kwanza na Wayahudi wa nyakati za Biblia walionaje sherehe za sikukuu ya kuzaliwa?

“Kwa ujumla Wakristo wa kipindi hicho hawakuwa wakisherehekea sikukuu ya kuzaliwa.”—The History of the Christian Religion and Church, During the Three First Centuries (New York, 1848), Augustus Neander (kilichotafsiriwa na Henry John Rose), uku. 190.

“Waebrania wa baadaye waliziona sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kuwa sehemu ya ibada ya sanamu, jambo ambalo lilithibitishwa kabisa na yale waliyoona katika sherehe zilizopendwa ambazo zilihusianishwa na sikukuu hizo.”—The Imperial Bible-Dictionary (London, 1874), kilichohaririwa na Patrick Fairbairn, Buku la 1, uku. 225.

Desturi zinazopendwa na wengi zinazohusiana na sherehe za sikukuu ya kuzaliwa zilitoka wapi?

“Desturi mbalimbali ambazo watu leo hutumia kusherehekea sikukuu zao za kuzaliwa ni za tangu zamani. Zilitokana na uchawi na dini. Desturi za kutoa pongezi, zawadi na kusherehekea—pamoja na mishumaa iliyowashwa—nyakati za kale zilikusudiwa kumlinda anayesherehekea sikukuu ya kuzaliwa asiumizwe na roho waovu na kuhakikisha usalama wake mwaka ujao. . . . Kufikia karne ya nne Wakristo walikataa kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa kuwa ni desturi ya kipagani.”—Schwäbische Zeitung (nyongeza ya gazeti Zeit und Welt), Aprili 3/4, 1981, uku. 4.

“Wagiriki waliamini kwamba kila mtu alikuwa na roho au daemon mwenye kumlinda aliyekuwapo wakati wa kuzaliwa kwake na kumlinda maishani. Roho huyo alikuwa na uhusiano wa kifumbo pamoja na mungu ambaye mtu huyo alizaliwa katika sikukuu yake ya kuzaliwa. Waroma pia waliunga mkono wazo hilo. . . . Wazo hilo liliendelezwa katika imani ya binadamu na linaonekana katika malaika mlinzi, mama wa ubatizo na mtakatifu mlezi. . . . Desturi ya kuwasha mishumaa juu ya keki ilianzishwa na Wagiriki. . . . Keki za asali za mviringo kama mwezi na zenye kuwashwa kwa mishumaa midogo ziliwekwa juu ya madhabahu za hekalu la [Artemi]. . . . Mishumaa ya sikukuu za kuzaliwa, katika hekaya za watu, ina uwezo wa pekee wa kuwapa watu yale wanayotamani. . . . Mishumaa midogo iliyowashwa na mioto ya dhabihu imekuwa na maana ya pekee ya kifumbo tangu mwanadamu alipoisimamishia miungu yake madhabahu mara ya kwanza. Kwa hiyo mishumaa ya sikukuu ya kuzaliwa ni heshima na sifa kwa mtoto wa sikukuu hiyo ya kuzaliwa na huleta bahati njema. . . . Salamu za sikukuu ya kuzaliwa na heri njema ni sehemu muhimu ya sikukuu hiyo. . . . Mwanzoni wazo hilo lilianzia katika uchawi. . . . Salamu za sikukuu ya kuzaliwa zinaweza kuleta mema au mabaya kwa sababu mtu huwa karibu zaidi na ulimwengu wa roho katika siku hiyo.”—The Lore of Birthdays (New York, 1952), Ralph na Adelin Linton, uku. 8, 18-20.
 
CHARMILTON

CHARMILTON

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Messages
6,306
Likes
9,066
Points
280
CHARMILTON

CHARMILTON

JF-Expert Member
Joined May 30, 2015
6,306 9,066 280
Birthday yangu ndio mwaka mpya kwangu, ile January 1 ni theoretical point of time na haina uhusiano wowote na mimi.
Kila inapofika birthday yangu, naitizama ile siku kwa mapana zaidi sababu kiuhalisia ndio siku nilipozaliwa.
Jua, nyota na mwezi vinakuwa kwenye position moja kama ile siku niliyozaliwa.Ni siku ambapo dunia inakamilisha mizunguko kadhaa ya kuzunguka jua tangu nizaliwe.
Kwangu birthday siyo siku ya kufanya party bali ni siku ya kutathimini mwaka ulioisha na kupanga mipango na mikakati ya mwaka mpya ninaouanza.

NB Mimi siamini kwenye Astrology, sifungamanishi tarehe ya kuzaliwa na matukio ya maisha yangu.
 
lulula

lulula

Member
Joined
Nov 20, 2016
Messages
80
Likes
43
Points
25
Age
48
lulula

lulula

Member
Joined Nov 20, 2016
80 43 25
Sikukuu ya kuzaliwa ni moja yaishara iliyowekwa na utatu mtakatifu ambao ni baba mwana Na roho mtakatifu ili kukuendeleza kumbukumbu hata mtiririko wa matukio katika maisha ya binadamu katika uwepo wetu duniani,.Kumbe basi siku ya kuzaliwa nimhimu kwa kutumaini afya njema Na hata Na mwendelezo wa kutenda Yale yanayo mpendeza Mungu
Kidogo sijanukuu lakini pata eleweka
 

Forum statistics

Threads 1,273,084
Members 490,268
Posts 30,470,668