Kipi ni Kipaumbele cha Serikali yetu kwa wananchi wake kati ya AFYA ya wananchi na POSHO? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipi ni Kipaumbele cha Serikali yetu kwa wananchi wake kati ya AFYA ya wananchi na POSHO?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mariavictima, Jul 14, 2011.

 1. m

  mariavictima Senior Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hamjambo wana jamii forums. Nadhani wengi wenu mmekuwa mkiona baadhi ya picha na maelezo ya watanzania wenzetu wenye shida ambao mara nyingi huwa wanatumia vyombo vya habari katika kuomba msaada. Naamini pia kati yetu, wengi tumeona au kusikia habari ya kijana Abbas Abdallah mkazi wa kijiji cha Kiru ndogo, Wilaya ya Babati Mkoani Manyara ambaye amevimba mguu kiasi cha kushindwa kutembea. Habari ya kijana huyu ni ya kusikitisha sana kutokana na yeye mwenyewe au familia yake kukosa kabisa uwezo wa kulipia gharama za matibabu na hivyo kumfanya alale tu nyumbani bila kujua cha kufanya. Pia naamini mmeona na kusikia habari nyingine ya kusikitisha ya mtoto Cecilia Edward (14) mwenye matatizo ya moyo yaliyopelekea kuvimba tumbo na kuwa kubwa la kutisha. Hawa ni baadhi tu ya watanzania wenzetu wanaoteseka kwa kukosa uwezo wa kugharamia matibabu yao iwe ni hapa nchini au hata nje ya nchi.
  Naamini pia viongozi wetu wa nchi huwa wanasoma magazeti yenye habari kama hizo. Ninachojiuliza mimi na ambacho kinaniumiza roho ni Je, inakuwaje Viongozi wetu wanashindwa kuwa na huruma kwa watu wenye shida na wanaohitaji msaada kama hawa, lakini wanakuwa na huruma ya kutetea posho wanazolipwa wabunge, mawaziri etc, eti kwa kigezo cha kuwagawia wananchi wanaowaomba majimboni kwao??? Mbona si9jawahi kusikia hata siku moja Mbunge yeyote amewasaidia wagonjwa kama hawa wanaoomba msaada kupitia magazeti au vyombo vingine vya habari? Ina maana Serikali haina uwezo wa kusaidia kugharamia matibabu ya watanzania wasio na uwezo? Inakuwaje iwe na uwezo wa kugawa kodi ya mtanzania kiholela kama posho?
  Wnajamii wenzangu, hebu tulijadili hili kwa uchungu. Najua viongozi wengi wamo humu jamii forums. Tulizungumze ili angalau ujumbe uwafikie na waone kama wanayofanya ni haki mbele ya Mungu.
  Naambatanisha picha za hawa watanzania wenzetu wanaoteseka. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   

  Attached Files:

Loading...