Kipi kitatokea endapo nitamuoa mpenzi wa rafiki yangu?

sakwano

JF-Expert Member
Sep 15, 2021
304
827
Moja kwa moja naomba nijikite kwenye mada, miezi kadhaa iliyopita nilipata kufahamiana na jamaa mmoja ambae aligeuka kuwa rafiki yangu mpenzi(best friend). Rafiki huyo alikua akiishi kwa raha na furaha pamoja na demu wake..(hajamuoa).Alikuwa akimsifia sana na pia kujihakikishia mbele yangu na hata baadhi ya marafiki wengine kuwa haitatokea akamuacha.

Kwa upande wangu niiliipenda hii familia ya best yangu na mara kadhaa nilienda kuwatembelea kama ndugu zangu..

Binafsi:
Mimi siku ya kwanza kumuona huyu demu wa jamaa nilimpenda sabb ni wife material, lakini nilijisemea tu moyoni na moyo ulikataa kufanya wizi wala ushawishi wowowte wa kumla kimasihara nilimuheshimu na maisha yakaendelea.

Miezi kadhaa kupita jamaa akapata demu mwingine,hii kitu ilipelekea mahusiano kuvunjika sabb jamaa Alikuwa akimcheat demu wake pasipo na umakini wowote hatimae kusababisha kuporomoka kwa mahusiano yao.

Demu:
Upande wa demu mahusiano kwake yakawa ni jeraha pamoja na majuto..ukizingatia alimpenda sana jamaa yake. Baada ya hayo yote mimi nikageuka kuwa mfariji na mrudisha mahusiano.Hali hii ya kuwa karibu na demu wa jamaa ilitupelekea kuanzisha mahusiano ya kimapenzi.

Ilikuwa ni rahisi sana kwa sabb toka watengane yule binti alihamia kwangu mm nikawa namficha nyumbni kwangu hata ikitokea jamaa kaja kunitembelea mimi nilikuwa nikimfungia chumbani kabla hajaonekana. Nilifahamu fika jamaa angejua angeniletea noma kubwa sana kwa sabb jamaa ni mkorofi..namfahamu vizuri.

Ndoa:
Baada ya kuhofia changamoto za huyu jamaa mimi nilimrudisha binti kwao,nikawa naishi mwenyewe kama ilivyokuwa nikiishi mwanzo,..

Kwa ufupi tu mimi nataka nimuoe huyu binti kwa sababu nimejirizisha ananifaa ...je?jamaa akijua itakuwaje?na kwenye harusi nimpe mualiko ama vipi?...angalizo ni kuwa jamaa hajui kama mimi na mahusiano na Aliekuwa mpenzi wake,

Niko njiapanda wakuu naombeni ushauri wenu...mtanisamehe kwa uwandishi mbaya ila imani yangu nimeeleweka.

Ahsanteni sana poleni na majukumu.
 
Kwa kuwa ni rafiki yako na hajui kama upo naye. Mtege kama utani umuulizie yule shemeji yupo wapi? Najua atajikosha jifanye kama unamuomba namba zake na umetokea kumpenda uone atasemaje.
Ila kumbuka lako ni moja tu kumoa tu.
Jamaa hajamuoa, hajawahi kumtolea mahari kwahiyo hana haki miliki. Kama umemuelewa oa tu, maisha lazima yaendelee. Mwambie ukweli tu hata kama akichukia
Kwahio mkuu nisimpe taarifa yoyote ya kuwa natarajia kuoa?
 
Tatizo Ni kwamba kwa mazingira yoyote utakayofanya kua nae na jamii ikajua,

Watajua umeanza nae tangu zaman, na Wewe ndio chanzo Cha mahusiano Yao kuvunjika.

Hata Kama ulikuta tayar walishaachana,

Cha kukushauri,
Wee Kama Ni kumla wee mle TU kimya kimya, kuruhusu jamaa ajue Ni hatar kwako, kwa rafiki yako na watu wengine wa karibu kwako.Washkaji watakutenga.
 
Back
Top Bottom