Kipi kilitokea mpaka Pepsi ikaizidi kete Coca Cola!!

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
13,136
27,083
Wadau ili halina ubishi kwamba soda inayouza sana kwa sasa hapa nchini ni Pepsi, Kumkuta mtu anakunywa Coca ni nadra sana!
Je pepsi walifanya jitihada gani kuipiku Coca cola..je ni mbinu za kawaida kibiashara au kuna hujuma ndani yake?
 
Uko idara ya Sales Pepsi sio?..
Tupe takwimu km unataka tuamini hilo
Mkuu hata wewe unaweza ukafanya observation...kuanzia mtaani mpaka kwenye mabaa..soda inayouzwa ni pepsi tu..coca wana hali mbaya sana!!
 
Pepsi wanaizidi coca cola kwa dar tuu kwingine anakungutwa tuu. Awamu zote za sikukuu kampuni ya Pepsi huwa inadorora kutoa huduma depot unakuta hamna soda kitu ambacho kinakera sana na wasipobadilika watapigwa nao tena kwa dar
 
Ila kusema hapa dar pepsi anatisha coz maeneo ninapoish maduka huwa hawauzag coca
 
Huku kanda ya ziwa Coca-Cola walileta vichupa vya mil 300 eti kwa sh 500/=

Tukawaama tukaenda Pepsi wao Mil 350 kwa sh 500....

Na sisi wabongo tunavyopendaga ujazo ...
Ndio basi tena harudi kwenye Coca-Cola hata kama sasa hivi wameongeza ujazo..
 
Wadau ili halina ubishi kwamba soda inayouza sana kwa sasa hapa nchini ni Pepsi, Kumkuta mtu anakunywa Coca ni nadra sana!
Je pepsi walifanya jitihada gani kuipiku Coca cola..je ni mbinu za kawaida kibiashara au kuna hujuma ndani yake?
Mimi mwenyewe nikiwa na kiu ya soda pepsi ndio hukata kiu yangu
 
Pepsi wamerudi sokoni na kuwa sawa au kuikaribia au kuipita koka kwa bei tu ,kunakipindi nao walipandisha ikawa mia 6 kwa huku Arusha wakapoteza wateja wakarudisha mia 5 ikarudi kwenye chart ,watu mambo ya chenchi hawataki kabisa ,ila kuna mitaa ukienda ni koka tu haswa ya wamasai na kuna mitaa haswa ya vijijini ukienda ni pepsi tu so kushusha bei imeirudisha pepsi sokoni
 
Mwaka 2013 mwezi 8-9 nilikuwa MBR (marketing representative body) wa SBL kampuni inayosambaza soda za pepsi wa muda.Nilizunguka duka hadi duka, grocery hadi grocery, bar hadi bar, hotel hadi hotel nikipita kila mahala wanapouza kinywaji chochote kat ya bidhaa za pepsi,coca,au maji ili kufanya tathmini ya biashara ya vinywaji baridi.Wakati huo Cocacola kampita pepsi licha ya kuwa zote zilikuwa zinalingana bei kwa mlaji wa mwisho yaani ya chupa ngumu 600@1, na take away 1000@1.Lakini katika maghala bei ya bidhaa za Coca zilizidi kidogo zile za pepsi.
Mwisho wa research yangu nilikuja na ripoti ambayo ilitumwa makao makuu.Kwenye sehemu ya mapendekezo nilipendekeza mambo kama 6 hivi,mojawapo ni kwamba pepsi ujazo wa ml.350 iuzwe sh.500.
Kazi hii niliifanyia manispaa ya Lindi wakati huo nilikuwa katika hali ngumu,walinilipa kiasi kidogo sana, kwa kazi mzuri kampuni ikawa radhi kuniajiri kama afisa masoko wa mkoa fulani ila meneja wa kanda hiyo akanizibia kwa kumleta rafiki yake toka Dar es saalam.
 
Pepsi wanaizidi coca cola kwa dar tuu kwingine anakungutwa tuu. Awamu zote za sikukuu kampuni ya Pepsi huwa inadorora kutoa huduma depot unakuta hamna soda kitu ambacho kinakera sana na wasipobadilika watapigwa nao tena kwa dar
Depot unakosa soda kwakuwa zimenunuliwa sana. Hujafikiria hilo
 
Sio mara ya kwanza. Miaka ya 80 pepsi ndio ilikuwa inatamba katika soko la Tanzania. Baadae miaka ya 90 coca wakachukua uongozi wa soko. Kama hayo unayosema ni kweli, basi hiyo ndio biashara kutesa kwa zamu
 
Kwa Utafiti wangu

>>>Pepsi anakimbiza kwa Dar, Moro

Cocacola anakimbiza Kaskazini.

Sijui sababu zake.
 
Kwa Utafiti wangu

>>>Pepsi anakimbiza kwa Dar, Moro

Cocacola anakimbiza Kaskazini.

Sijui sababu zake.
Pengine upo sahihi..huku kusini pepsi inakimbiza vibaya!
 
Back
Top Bottom