Kipi chao.... Kipi chetu!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipi chao.... Kipi chetu!?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kigarama, Oct 10, 2011.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kila jamii ina taratibu zake na mifumo yake ya jinsi ya kuishi. Haya yafuatayo ni mambo ambayo nadhani kwamba yanagawanyika katika jamii ni yepi ya kufanywa na wanaume au wanawake na yepi ni majukumu ya nani kwenye familia na ni zipi ni haki za nani kwenye familia. Tupe mawazo yako kwako yamekaaje.

  1. Kumiliki mali za familia ni haki ya nani?

  2. Kutoa na kuosha vyombo baada ya kula ni wajibu wa nani?

  3. Kubadilisha na kufua nepi za mtoto ni kazi ya nani?

  4. Kutandika Kitanda ni shughuli ya nani?

  5. Kufagia chumba/Nyumba nani afanye?

  6. Kulipia bili mbali mbali kama za maji na Umeme yupi atoe hela yake?

  7. Kulipia karo za watoto shuleni pamoja na matumizi yao ni nani awajibike?

  8. Kufua nguo za wawili (Wenza) nani hasa anahusika?

  9. Haki ya kutoa talaka kila mmoja anayo au ni ya jinsia moja tuu?

  10. Watoto majina ya ukoo wachukue kwa nani, baba au mama?

  11. Kanuni za jinsi ya kuishi ndani ya nyumba ziwekwe na nani? Mume au mke, ama wote wawili?

  Haya ni mambo yanayotofautiana kati ya watu na watu na jamii na jamii lakini sisi kama wana MMU tunayaonaje?
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  maswali bila kutusaidia baadhi hata ya majibu unatuacha kwenye mataa.......
   
 3. JICHO LA 3

  JICHO LA 3 JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  in red aweke mke ndo inapendeza
   
Loading...