kipi bora kusoma bachelor home na kwenda kusoma nje ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kipi bora kusoma bachelor home na kwenda kusoma nje ya nchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 4, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nalimwaga hili sababu kuna Afisa mmoja wa serikali kanitisha sana Kuna anaosema kwamba elimu ya nchi za nje haifai kwasababu kuna utofauti mkubwa wa mitaala na ufundishaji kwamba wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu hapa bongo wanapiga msuli sana hasa UDSM na waalimu pia wa kibongo quality yao ipo juu sana tofauti na waalimu wa nje ya nchi pia kuna nchi inabidi ujifunze lugha yao mwaka mzima au miaka 2 then uanze bachelor kwa kutumia lugha yao ama kiingereza pia system ya nje masomo ni mengi sana kama shule za msingi ukilinganisha na bongo sasa nimeomba kujua kipi bora kati ya kusoma nje ya nchi au nibaki hapahapa bongo maana nimepata offer ya kwenda kusoma bachelor nje ya nchi ila huko natakiwa nijifunze lugha yao mwaka mzima then ndipo nianze bachelor miaka 4 so kuna Afisa mmoja wa serikari ananishauri kama ni uchumi bora nisome vyuo vya hapahapa bongo!waungawana naombeni ushauri.hasa kwa mliopo vyuo nje ya nchi hasa nchi za Europe.
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Mr Kilimasera kwangu mimi nioanavo inategema nchi na nchi.kama umepata offer ya kwenda nje nadhani mitala yake imeanishwa ktk website ya chuo hicho ww binasfi angalia ni masomo mangapi wanafundisha kwa semister na kama wanafundisha kiingereza ni poa zaidi usiiache hiyo offer hata kama utasoma lugha yao kwa mwaka mzima,kama ukijituma na kujiibiisha hakuna lisilowezekana.Asikutishe mtu kwa hilo.Lau pia kama umepata adm ya UDSM kusoma bcom sikushauri sana pale tumepiga msuli sana tatizo ni kuwa walimu wanafurahia kukamata badala ya kufurahia wanafunzi kufaulu huu ni ujinga wa walimu wetu wa kibongo.kama umepata chuo kinachotambulika we nenda wala usihofu utapata upeo wa kujifunza mengi zaidi kutoka kwa watu mbalimbali.Cha muhimu ni bidii ktk masomo basi.Wengi wanasema ni vema kusoma digree ya kwana bongo lakini kama umepata nje kwa nn usiende? kazi kwako.Wengi tumesoma bongo kwa kuwa hatukuwa na altenative ya chuo kingine ila kwa wewe ndugu nenda fasta.
   
 3. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  huyo bosi wako amewahi kusoma nje? Au anaongelea kutokana na masimulizi aliyoyasikia kwa watu?
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Dec 4, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Usiiache hiyo nafasi ya kwenda kusoma nje ikapita bure tu yangu.............achana na vyuo vya bongo kama umepata chuo nje ya nchi, nenda ukasome!
   
 5. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,124
  Likes Received: 23,724
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa mimi ningeenda kusoma kwa hao waalimu vilaza, kama kweli ni vilaza wa nje ya nchi!.
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Dec 4, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu mi nadhani inategemea mambo mengi,
  aina ya chuo, nchi kilipo chuo, mdhamini nk.
  Kwa maoni yangu bora uende nje kama chuo ni cha uhakika,
  tatizo la tz ni kweli watu wanakamua sana lakini sio kuelewa bali kuepuka kukamatwa mashati na malectures wanao ona raha ukifeli.
  Mfumo wa vyuo bongo upo kupasi zaidi wakati wenzetu kuelewa kwanza ndio uta pasi.
   
 7. Kisima

  Kisima JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 3,768
  Likes Received: 2,222
  Trophy Points: 280
  Nenda nje kijana achana na vyuo vya kibongo mi mwenyewe km kakayako nimesoma chuo kikuu bongo hamna lolote zaidi ya kuepuka suprementary ya malecturer kasome hulo uweze kujitegemea. Wengi wetu tuliosoma Bongo tunategemea zaidi ajira eventuary tunapigwa jua siku nzima tukitafta ajira.
   
 8. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2010
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Kama umepata scholarship au una uhakika wa kupata msaada financially hasa mwaka wa mwanzo bora uende nje. Inategemea ni nchi gani kama wengi walivyokushauri kuna mambo mengi yanatofautiana ungekuwa specific ni nchi gani hasa umepata nafasi nadhani pia ungepata ushauri wa uhakika zaidi.
   
 9. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  huyu bosi yeye kasoma advance diploma ya maendeleo ya jamii pale Tengeru CDTI nahisi nae alikuwa anasikia kwa watu tu maana scholarship nimepata ya nchi ya Russia so akasema kwamba huko watu wanaosoma huko wanakuwa walevi sana na shule ya huko inawafaa watu wa science tu!
   
 10. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nawashukuru sana kwa ushauri wenu niliona niulize hapa sababu nilijua wengi hapa ni watu wenye uelewa mpana juu ya maisha na mambo ya nje na kuna wengine wanaishi huko so wanajua the real situation
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  bongo utapiga photocopy vitabu mpaka semester inaisha.hakuna lolote hapa labda kwa kozi ya medicine kwa kua utakumbana na tropical diseases ambazo nchi zingine hakuna!
   
 12. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nikuambie ndugu,huyo mshauri wako sio kosa lake kwa vile hajuhi alisemalo.Tofauti ya mitaala sio ishu.Na kama anakwambia ati elimu ya bongo ni nzuri kuliko nchi zingine,em muulize elimu hiyo nzuri ya bongo imeweza kutranslate vipi kwenye maendeleo ya nchi,mbona bongo ni masikini wa kutupwa na hiyo elimu wanayojidahi nayo.Facts ni hizi hapa,elimu ya bongo ni mbovu mbovu mno.Waalimu wa bongo hawako serious,mimi nakumbuka kuna ndugu yangu alikuwa mzumbe ananiambia sometimes kaenda class mwalimu hajafika ati ana safari nk nk.Chuo kikuu? what?..vitu kama hivyo havitokei kwenye nchi zingine watu wako serious na elimu yao,muhula ilivyopangwa ndivyo inavyoisha,mwalimu akitokea asiwepo lazima awe replaced.Elimu ya Urusi,China,India,Malaysia,Japan,Korea,Europe and North America n.k ni nzuri mara kibao kulinganisha na ya Tanzania.Huku watu wameendelea sababu ya elimu,ukifanikiwa kupata scholarship ya kutoka bongo,kimbia fasta toka nduki we kimbia!..utajifunza mengi sana nje ya nchi,utajua dunia ilivyo.Mimi nilipata B.COM udsm na Scholarship zote kwa pamoja nikapiga chini B.COM,today am proud of my decision.
   
 13. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  thank you very much!
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ina maana ukibaki bongo ndo huwezi kua mlevi ukitaka???Huo ni uamuzi wa mtu na sio sehemu.Newayz nna watu wanasoma Russia wala hawalalamiki sana......sema baridi ni kali alafu wakati mwingine wazawa wanakua wakorofi kwa wageni....ila sijaskia mtu akilalamika shule sio nzuri!Tumia hiyo nafasi usije ukaitamani baadae ikishapita!
   
 15. BWANYEENYE

  BWANYEENYE Member

  #15
  Dec 4, 2010
  Joined: Jun 2, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bro labda kwa reason nyengine ila kwa ulevi ni ww mwenyewe kama utaendekeza pombe ht bongo unaweza kuwa mlevi sisi tupo huku wala pombe haijawahi karibia kinywa.........
   
Loading...