Kipenzi Changu Gazeti La Rai

A

AG

Member
72
125
Kipenzi changu gazeti la rai, nimekukosea nini? Kiboko cha makala zilizo jaa ukosoaji, leo umejikunyata mkia, vipi? Rai ya Jenerali Ulimwengu, Rai ya Johnson Mbwambo Kidee, kulikoni siku hizi mbona umekengeuka njia? Yaani gazeti limekosa ridhim kabisa, ama kweli hujafa hujaumbika. Nisaidieni; kipenzi changu kala sumu gani? Hizi hoja motomoto rai wewe unazipoza; ahh my friend what is wrong?
 
K

Kimbembe

Senior Member
122
0
Baada ya kukubali kuuza hisa kwa Mu Iran na kupokea mshiko wa pembeni kila baada ya muda na hata kuahidiwa mazuri lazima mtu mzima mwenye akili zake awe mwendawazimu na kupotosha ukweli .Lakini Rai inakufa na kunazaliwa mengine yenye nguvu kama MwanaHalisi,Tanzania Daima na linakuja gazeti la Raia Mwema.
 
G

Game Theory

JF-Expert Member
8,561

Nadhani its time watu waka move on na kuachana na Print media za Tanzania

M

Mtanzania

JF-Expert Member
4,818
1,225
.Lakini Rai inakufa na kunazaliwa mengine yenye nguvu kama MwanaHalisi,Tanzania Daima na linakuja gazeti la Raia Mwema.
Hivi Tanzania Daima lina tofauti na RAI?

Ni sawa kuhusu Mwanahalisi na pia mwananchi pamoja na magazeti mengine kama thisday lakini Tanzania Daima hawana tofauti na RAI.

Gazeti likimilikiwa na wanasiasa usitegemee ukweli kutoka gazeti kama hilo.
 
L

lageneral

Member
61
0
Raia mwema litakuwa lini mitaani na ninani wamiliki?Natafuta partner wakuanzisha naye gazeti huko nyumbani Tanzania,gazeti litakalo kuwa huru na kichocheo cha kuiletea maendeleo nchi yetu.Mtu yeyote ambaye atapenda kushirikiana katika biasha hii anijibu kupitia forum halafu baadaye tatafutane
 
Forum statistics

Threads
1,424,857

Messages
35,074,128

Members
538,128
Top Bottom