Tangu mwezi wa 11 mwaka Jana, Serikali ilituambia kuwa kipaumbele chake cha kwanza ni viwanda. Leo ni mwaka unaelekea kuisha, sioni hata dalili ya hicho kiwanda.sasa hivi wamekuja tena na mpya. Mnaniambia ni kuhamia Dodoma. As I know fedha za kuhamia Dodoma ni nyingi kuliko ambazo zinahitajika kufufua viwanda vyetu.
Hali za maisha za watu mitaani ni mbaya sana. Mzunguko wa pesa ni mdogo haijawahi kutokea tangu Mwinyi. Ni dhahiri kuwa wananchi hawana furaha kabisa. Kila mtu analalamika. Tajiri analalamika. Masikini ndiyo kabisa anahisi bora asingezaliwa.
Nataka kujua seriously. Nini hasa kipaumbele chenu?. Kesho hatujui mtatuambia kituko gani tena kipya. Mimi nafikiri mngetekeleza kwanza la viwanda halafu hayo mengine yaje taratibu. Hatuna haraka ya kuhama kiasi hiki, Serikali kuweni na huruma na mnaowangoza. Rekebisheni kwanza hali zao za uchumi. Hali zao ni mbaya mno huko mitaani.