Mifuko iliyotolewa ni ghari haiendani na Uwezo wa wauzaji wadogo wadogo.
Watoa matamko wawatolee pia wazalishaji waipack kama ile ile iliyokuwepo na iwe bei ndogo.
Mfano ile Mifuko ya plastick midogo ilikuwa inafungwa pakti moja ndani mifuko50 kwa sh 550-700 sawa na kafuko kamoja kwa almost Sh 14 which is simple kwa muuza ndizi kununua na kuwafungia Wateja wake bure.
But hii ya mbadala mfuko wa saizi kama hiyo niliyoizungumza hapo juu inauzwa kwa piece/mmoja mmoja sh 90-100.
Sasa ukija kwa mama muuza ndizi kama alikuwa anaweza only kutumia pakti moja ya Sh 700 kwa sasa idadi ile ile ya Mifuko 50 itamgharimu Sh 5000 kwa Mifuko 50 tu. Sasa kama alikuwa anatumia pakti 4 ujue tayari imeshagonga elfu 20.
Kwahiyo watoa matamko tunawaomba wawalazimishe wazalishaji waipack kama hiyo iliyokuwepo na bei zikaribiane mno na iliyokuwepo