Kipaji / kipawa ni nini?

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habarini mabestito!

Sio kwamba sijui ninachotaka kukijua bali nataka wengine wafunguke
zaidi katika kujua kile ukijuacho best wangu

nataka kufahamu maana ya maneno haya KIPAJI / KARAMA / KIPAWA.
mana wengi wetu tumekuwa tukichanganya maneno haya na kusema
kuwa ni mamoja na kumbe yako tofauti kabisa.

Kwa uelewa wako rafiki yangu Je Kipaji/Karama/Kipawa ni nini?
Hebu shiriki hapa kuelezea ili wale wengine wasioelewa waelewe.

Karibuni mezani kwa uchangiaji wako naomba msijoke tu tunafundishana
hapa.
 
asante ladyfurahia naomba niwe wa kwanza kushangia, KIPAJI, KIPAWA NA KARAMA ni vitu vinavyofanana lakini vikitofautiana katika hali fulani fulani, vyote vina maana kuwa na uwezo wa ziada kuzidi uwezo wa kawaida wa binadamu, mfano kipaji cha mpira, uchoraji nk lakini kipaji kikihusika zaidi na akili na mambo ya kimwili. KIPAWA NA KARAMA vinahusika zaidi na mambo ya kiroho mfano karama au kipawa cha uponyaji, kuhubiri nk
 
naomba niongezee tena, sio kiherehere bali ni hamu ya kushare!!! kuna vitu sio kipaji kipawa wala karama ni tabia mbaya tu, mfano ulevi, umalaya umbea, uongo, uzushi, utapeli, roho mbaya nk!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…