Parata
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 3,090
- 693
Kwa ufupi...
Kutoa ahadi ni rahisi lakini kutimiza
ahadi ndio tatizo! Nice, binti mrembo
mtoto kigogo wa benki kuu tawi la
Mwanza, anampa ahadi mpenziwe
Robert ya kuwa atampenda milele,
haijalishi ni katika mazingira gani.
Robert anatoka katika familia ya
maisha ya kati na analelewa na baba
yake mdogo baada ya baba yake
mzazi kufariki. Lakini ahadi ya Nice
inaingia dosari baada ya uhusiano
wao kupata upinzani mkali toka kwa
wazazi wa pande zote mbili...
SEHEMU YA KWANZA:
"happy birthday to you, happy
birthday to you, happy birthday,
happy birthday, happy birthday to
you." sauti za furaha zilikuwa
zikiimba na kufuatiwa na vigelegele,
nderemo na vifijo kumpongeza binti
mwenye sifa zote za kumfanya
mwanaume amgeukie mara mbili
mbili, Nice Mbawala! Kila mtu ama
alimpa mkono, alimkumbatia ama
alimbusu shavuni kuonesha
kumpongeza! Kila mtu alionesha
furaha!
Katika kona moja alisimama kijana
alievalia nadhifu, suruali nyeusi,
shati la pinki na tai nyeusi ya
kipepeo, mkononi alikuwa na glasi ya
wine, usoni hakuonesha kuwa na
raha!
Wakati ukumbi unalipuka kwa vifijo,
yeye alikuwa kimya kabisa kasimama
tuli! Akaitua glasi iliyokuwa na nusu
mvinyo na kutoka nje ya ukumbi huo,
akaelekea katika bustani na kuketi juu
ya bembea akionekana mwingi wa
mawazo!
Baada ya muda Nice alitokea mlango
na kuangaza nje, alipomuona kijana
yule akaelekea alipo, "mbona
umekimbia sherehe yangu jamani?"
akalala akiketi katika bembea
pembeni yake. Kijana akatoa
tabasamu hafifu bila kujibu kitu. Nice
akamtazama na kumuonea huruma,
akapeleka mkono na kumshika bega,
"Robert usiwaze sana, ni mipango ya
Mungu, sote tunapita!"
Robert au Roby kama Nice mwenyewe
alivyopenda kumwita, alijikuta chozi
likimdondoka! Hakuwa hata na zaidi
ya miezi tangu amzike baba yake
mpendwa! Machungu bado yalikuwa
moyoni mwake! Nice akainuka na
kumkumbatia rafiki yake huyo, akalia
nae!
***
Kipindi hiki cha likizo kiliwakutanisha
mara kwa mara Nice na Roby, kwa
kuwa walikuwa majirani, mara nyingi
Roby alienda kwao Nice wakaketi
kibarazani na kuongea mambo ya
shule, kwa kuwa wote walikuwa
wanasoma mchepuo mmoja, walikuwa
na mengi ya kuongea. Jioni hii Nice
alikuwa akimsindikiza Roby, walikuwa
wakitembea taratibu huku wakiongea,
mara Nice akamshika mkono Roby
ambae mwili ulimsisimka si kidogo,
walienda mbele kidogo na mara Nice
akageuka na kumkumbatia, busu
murua mdomoni na kumwachia mara!
Roby alibaki na mchecheto alitamani
liendelee, akapeleka mkono mdomoni
huku Nice akitabasamu, kisha
akageuza kurudi kwao! Roby
alisimama pale kwa muda asijielewe
elewe! Badala ya kwenda nyumbani
akaelekea kwa rafiki yake Zuberi,
"hey, mbona leo una furaha sana!"
kilikuwa kitu cha kwanza kwa Zuberi
kusema baada ya Roby kuingia akiwa
ana uso wa furaha! Roby hakujibu
kitu zaidi ya kujirusha kitandani!
Zuberi akacheka na kutania, "au
umeonana na Sigfrida, ha ha haaa!"
akatia utani kidogo! Roby akacheka,
Sigfrida alikuwa girlfriend wa Roby
wakiwa sekondari Mwenge!
"umenikumbusha mbali sana! Kuna
kitu kingine mshkaji wangu!"
Zuberi akaketi kwenye pembe ya
kitanda na kumsikiliza Roby, "Nice
kani kiss!" Roby akasema kwa furaha
huku akiigiza jinsi Nice alivyomkiss!
Zuberi akabaki na mshangao, "acha
bwana! Serious?!"
"yeah, serious like Hell!"
Zuberi akacheka kwa furaha na
kuuliza, "mmeanza lini tena?"
Roby akainuka pale kitandani na
kujaribia tena jinsi Nice alivyombusu!
***
Baada ya mlo wa usiku, Roby
alijifungia chumbani kwake
akiitazama na kuishika simu akiwaza
ampigie Nice ama vipi? Hakuwa
akijiamini kama kweli Nice amefanya
vile kwa kuwa anampenda kimapenzi
au kama rafiki tu? Au kutokana na
matatizo yaliyompata, anajaribu kuwa
karibu nae kumfariji? Hakuwa na
uhakika! Nice alikuwa mzuri wa sura,
umbo na tabia pia! Vijana wengi
shuleni kwao walimpenda, hata
walimu pia wapo waliojaribu
kumrubuni wampate, lakini hakuna
aliefanikiwa! Ucheshi wa Nice
uligeuka shubiri kwa yeyote
aliemtongoza! Wakati anafikiri hayo,
simu yake ikaita, akakurupuka,
alikuwa Nice.....
Kutoa ahadi ni rahisi lakini kutimiza
ahadi ndio tatizo! Nice, binti mrembo
mtoto kigogo wa benki kuu tawi la
Mwanza, anampa ahadi mpenziwe
Robert ya kuwa atampenda milele,
haijalishi ni katika mazingira gani.
Robert anatoka katika familia ya
maisha ya kati na analelewa na baba
yake mdogo baada ya baba yake
mzazi kufariki. Lakini ahadi ya Nice
inaingia dosari baada ya uhusiano
wao kupata upinzani mkali toka kwa
wazazi wa pande zote mbili...
SEHEMU YA KWANZA:
"happy birthday to you, happy
birthday to you, happy birthday,
happy birthday, happy birthday to
you." sauti za furaha zilikuwa
zikiimba na kufuatiwa na vigelegele,
nderemo na vifijo kumpongeza binti
mwenye sifa zote za kumfanya
mwanaume amgeukie mara mbili
mbili, Nice Mbawala! Kila mtu ama
alimpa mkono, alimkumbatia ama
alimbusu shavuni kuonesha
kumpongeza! Kila mtu alionesha
furaha!
Katika kona moja alisimama kijana
alievalia nadhifu, suruali nyeusi,
shati la pinki na tai nyeusi ya
kipepeo, mkononi alikuwa na glasi ya
wine, usoni hakuonesha kuwa na
raha!
Wakati ukumbi unalipuka kwa vifijo,
yeye alikuwa kimya kabisa kasimama
tuli! Akaitua glasi iliyokuwa na nusu
mvinyo na kutoka nje ya ukumbi huo,
akaelekea katika bustani na kuketi juu
ya bembea akionekana mwingi wa
mawazo!
Baada ya muda Nice alitokea mlango
na kuangaza nje, alipomuona kijana
yule akaelekea alipo, "mbona
umekimbia sherehe yangu jamani?"
akalala akiketi katika bembea
pembeni yake. Kijana akatoa
tabasamu hafifu bila kujibu kitu. Nice
akamtazama na kumuonea huruma,
akapeleka mkono na kumshika bega,
"Robert usiwaze sana, ni mipango ya
Mungu, sote tunapita!"
Robert au Roby kama Nice mwenyewe
alivyopenda kumwita, alijikuta chozi
likimdondoka! Hakuwa hata na zaidi
ya miezi tangu amzike baba yake
mpendwa! Machungu bado yalikuwa
moyoni mwake! Nice akainuka na
kumkumbatia rafiki yake huyo, akalia
nae!
***
Kipindi hiki cha likizo kiliwakutanisha
mara kwa mara Nice na Roby, kwa
kuwa walikuwa majirani, mara nyingi
Roby alienda kwao Nice wakaketi
kibarazani na kuongea mambo ya
shule, kwa kuwa wote walikuwa
wanasoma mchepuo mmoja, walikuwa
na mengi ya kuongea. Jioni hii Nice
alikuwa akimsindikiza Roby, walikuwa
wakitembea taratibu huku wakiongea,
mara Nice akamshika mkono Roby
ambae mwili ulimsisimka si kidogo,
walienda mbele kidogo na mara Nice
akageuka na kumkumbatia, busu
murua mdomoni na kumwachia mara!
Roby alibaki na mchecheto alitamani
liendelee, akapeleka mkono mdomoni
huku Nice akitabasamu, kisha
akageuza kurudi kwao! Roby
alisimama pale kwa muda asijielewe
elewe! Badala ya kwenda nyumbani
akaelekea kwa rafiki yake Zuberi,
"hey, mbona leo una furaha sana!"
kilikuwa kitu cha kwanza kwa Zuberi
kusema baada ya Roby kuingia akiwa
ana uso wa furaha! Roby hakujibu
kitu zaidi ya kujirusha kitandani!
Zuberi akacheka na kutania, "au
umeonana na Sigfrida, ha ha haaa!"
akatia utani kidogo! Roby akacheka,
Sigfrida alikuwa girlfriend wa Roby
wakiwa sekondari Mwenge!
"umenikumbusha mbali sana! Kuna
kitu kingine mshkaji wangu!"
Zuberi akaketi kwenye pembe ya
kitanda na kumsikiliza Roby, "Nice
kani kiss!" Roby akasema kwa furaha
huku akiigiza jinsi Nice alivyomkiss!
Zuberi akabaki na mshangao, "acha
bwana! Serious?!"
"yeah, serious like Hell!"
Zuberi akacheka kwa furaha na
kuuliza, "mmeanza lini tena?"
Roby akainuka pale kitandani na
kujaribia tena jinsi Nice alivyombusu!
***
Baada ya mlo wa usiku, Roby
alijifungia chumbani kwake
akiitazama na kuishika simu akiwaza
ampigie Nice ama vipi? Hakuwa
akijiamini kama kweli Nice amefanya
vile kwa kuwa anampenda kimapenzi
au kama rafiki tu? Au kutokana na
matatizo yaliyompata, anajaribu kuwa
karibu nae kumfariji? Hakuwa na
uhakika! Nice alikuwa mzuri wa sura,
umbo na tabia pia! Vijana wengi
shuleni kwao walimpenda, hata
walimu pia wapo waliojaribu
kumrubuni wampate, lakini hakuna
aliefanikiwa! Ucheshi wa Nice
uligeuka shubiri kwa yeyote
aliemtongoza! Wakati anafikiri hayo,
simu yake ikaita, akakurupuka,
alikuwa Nice.....