Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,755
Kwani mkuu wewe hili hauliangalii kwa mboni za kisiasa?...Hauoni kama uliyoaandika kwenye bandiko hili ni siasa tupu....Bandiko la kisiasa lazima lijadiliwe kwa mtazamo wa kisiasa Chifu...Sijui ni kwanini watu wanaangalia kila jambo kwa mboni za kisiasa badala ya masilahi mapana ya nchi.
Jambo zuri rekodi zipo hivyo wengine tunapozungumza tuna uhakika
Hatuhitaji kufanya makosa yale yale kwasababu tu wapo wanaofanya makosa hayo hayo
Hii ni dhana mbovu sana
Huyu bwana alisimama kupinga ukuu wa Wilaya, leo anarudi kuwaambia watu wale wale, taswira yake kama kiongozi inakuwa wapi?
Lakini pia lazima tujifunze kwa viongozi wetu waliotangulia. Wapo walioacha masialhi yao binafsi kutetea nchi. Hata kama ni wachache, hatupaswi kuishi kwa historia yao tu, ni wakati tujenge historia ya kizazi hiki. Je, haya ndiyo tunatarajia kwa vijana kama hawa?
Lakini pia mteule alienda mbali, si kwa ukuu wa Wilaya, alifikia mahali anapotosha umma, anazungumza uongo usiohitaji certificate.
Leo kazawadiwa kwasababu hiyo tu! Tunajenga nchi kweli?
Tukianza kutetea haya, ipo siku watu watateua wajomba zao, nao watasema wanaweza kufanya nao kazi vizuri, kuna shida gani!!
Hebu tuangalie nchi kwa upana wake. Nipo katika rekodi nikipinga nafasi za ukuu wa wilaya. Ninapoona ukuu huo unatolewa kwasababu tu fulani anapepeta sana , inatia shaka
Kiongozi anateuliwa kwasababu alimtwanga mzee fulani katika kongamano!
Ndio tunahitaji hayao?
Halafu tukisema lipo tatizo, wapo wanaosema mbona Mrema naye alitwangwa kule Tanga? ina make sense kweli