Kiongozi wa Kikundi cha Ugaidi cha Islamic Jihad auawa na Israel

Watakutanishwa vipi wakati wanaendelea kurushiana vifaa?
Pili,kuna mkubwa wa UN jana alisema hivyo vita visitishwe kwa pande zote mbili as soon as possible, Nani amemsikiliza na bado vitu vinatumwa hewani tu!?
Wanakutanishwa viongozi hata kama wapiganaji wao wanaendelea kupingana.Hayo yalishafanyika nyuma kidogo tena nakumbuka ni Misti iliwakutanisha, baada ya mazungumzo wakasitisha vita.UN ni zaidi ya Misti.
 
Hawawezi kutanishwa sababu Hamas anajulikana kama Gaidi
Hapo naona ndio tatizo linakwamisha kutatua huu mzozo. Hadi leo jumuiya ya kimataifa hawataki kuitambua hamasi Kama mtawala, Ila wamemtambua Abas kama Rais wa palestina. Abas hana mamlaka huko Gaza. Hii ni changamoto. Lakini naona Misri anaheshimiana na pande zote, anaweza shika usukani wa kusuluisha
 
Kiukweli tujifunze kitu hapo hawa mashehe wanaoacha kufundisha uislamu badala yake wanafundisha kuhusu wakristo kuwa makafili ,,, Unazani hata kule palestina hawapo mashehe kama hao? kwahio achene makafili wafanye ukafili mnaouzungumza kuwahusu simnaupenda? basi vumilieni hamuwawezi wale makafili na watawaacha hadi mkijitambua kinachowapasa kufundisha katika imani zenu.
 
Kiongozi wa Kikundi cha Kigaini cha Islamic Jihad Kamanda Hussam Abu Arbeed ameuawa na majeshi ya Israel kwenye shambulizi la Anga

Kamanda Hassam amekuwa akisakwa kwa muda mrefu na amehusika na mashambulizi mengi ya ugaidi dhidi ya Israel kwa muda wa miaka 15 akiongoza divisheni ya kaskazini ya Gaza.
==
Israeli iliipiga Gaza City kwa mashambulizi ya anga Jumatatu, na kumuua kamanda mwandamizi wa wanamgambo wa Palestina, nao wanamgambo wa Palestina walifanya mashambulizi ya roketi dhidi kwa Israeli wakati ghasia katika eneo hilo zilipoingia wiki ya pili.

Tangu mapigano yalipoanza Mei 10, Wapalestina wasiopungua 200 wameuawa, wakiwemo watoto wasiopungua 59 na wanawake 35, kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza. Waisraeli wasiopungua 10 wameuawa katika mashambulizi ya roketi, pamoja na mtoto wa miaka 6.

Jeshi la Israeli lilisema liliharibu mahandaki ya kilomita zipatazo 15 huko Gaza yaliyotumiwa na Hamas, pamoja na jengo la orofa tano ambalo lilikuwa na wizara ya Maswala ya Kidini inayoendeshwa na Hamas, na kumuua kamanda wa Jihad wa Kiislam wa kaskazini mwa Gaza, Hussam Abu Harbeed.

Ikijibu mashambulizi, kundi la Jihad lilifyatua roketi katika mji wa pwani wa Israel wa Ashdod na watu saba wamejeruhiwa kwa mujibu wa maafisa.
watu wapumbavu.
israel akiua kimakusudi haitwi gaidi ila wanaompinga israel wanaitwa magaidi.
 
Back
Top Bottom