Kiongozi wa Kikundi cha Ugaidi cha Islamic Jihad auawa na Israel

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,204
4,695
Kiongozi wa Kikundi cha Kigaini cha Islamic Jihad Kamanda Hussam Abu Arbeed ameuawa na majeshi ya Israel kwenye shambulizi la Anga

Kamanda Hassam amekuwa akisakwa kwa muda mrefu na amehusika na mashambulizi mengi ya ugaidi dhidi ya Israel kwa muda wa miaka 15 akiongoza divisheni ya kaskazini ya Gaza.
==
Israeli iliipiga Gaza City kwa mashambulizi ya anga Jumatatu, na kumuua kamanda mwandamizi wa wanamgambo wa Palestina, nao wanamgambo wa Palestina walifanya mashambulizi ya roketi dhidi kwa Israeli wakati ghasia katika eneo hilo zilipoingia wiki ya pili.

Tangu mapigano yalipoanza Mei 10, Wapalestina wasiopungua 200 wameuawa, wakiwemo watoto wasiopungua 59 na wanawake 35, kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza. Waisraeli wasiopungua 10 wameuawa katika mashambulizi ya roketi, pamoja na mtoto wa miaka 6.

Jeshi la Israeli lilisema liliharibu mahandaki ya kilomita zipatazo 15 huko Gaza yaliyotumiwa na Hamas, pamoja na jengo la orofa tano ambalo lilikuwa na wizara ya Maswala ya Kidini inayoendeshwa na Hamas, na kumuua kamanda wa Jihad wa Kiislam wa kaskazini mwa Gaza, Hussam Abu Harbeed.

Ikijibu mashambulizi, kundi la Jihad lilifyatua roketi katika mji wa pwani wa Israel wa Ashdod na watu saba wamejeruhiwa kwa mujibu wa maafisa.
 
Kiongozi wa Kikundi cha Kigaini cha Islamic Jihad Kamanda Hussam Abu Arbeed ameuawa na majeshi ya Israel kwenye shambulizi la Anga

Kamanda Hassam amekuwa akisakwa kwa muda mrefu na amehusika na mashambulizi mengi ya ugaidi dhidi ya Israel kwa muda wa miaka 15 akiongoza divisheni ya kaskazini ya Gaza
Peponi kwa mujibu wao.
 
Hii vita ya Israel na wapalestina ni ngumu sana kuitolea maamuzi, kwa maana inagusa imani, kama kuanza ilianza tangu enzi za mitume na adi leo bado inasumbua.

Waisrael wanadai Mwenyezi Mungu aliwaambia wakiue kizazi chote cha wapalestina na waarab walio wakuta ndani ya ‘nchi ya ahadi/ Israel’ lakini huruma yao ya kuto wamaliza ndiyo inayo wapinza adi leo.
 
Hii vita ya Israel na wapalestina ni ngumu sana kuitolea maamuzi, kwa maana inagusa imani, kama kuanza ilianza tangu enzi za mitume na adi leo bado inasumbua, Waisrael wanadai Mwenyezi Mungu aliwaambia wakiue kizazi chote cha wapalestina na waarab walio wakuta ndani ya ‘nchi ya ahadi/ Israel’ lakini huruma yao ya kuto wamaliza ndiyo inayo wapinza adi leo........
Huo si utakua ni unyama tu kama wa Kipagani.
 
Kiongozi wa Kikundi cha Kigaini cha Islamic Jihad Kamanda Hussam Abu Arbeed ameuawa na majeshi ya Israel kwenye shambulizi la Anga

Kamanda Hassam amekuwa akisakwa kwa muda mrefu na amehusika na mashambulizi mengi ya ugaidi dhidi ya Israel kwa muda wa miaka 15 akiongoza divisheni ya kaskazini ya Gaza
Free PalestineView attachment 1788681
Screenshot_20210515-125416.jpg
 
Kiongozi wa Kikundi cha Kigaini cha Islamic Jihad Kamanda Hussam Abu Arbeed ameuawa na majeshi ya Israel kwenye shambulizi la Anga

Kamanda Hassam amekuwa akisakwa kwa muda mrefu na amehusika na mashambulizi mengi ya ugaidi dhidi ya Israel kwa muda wa miaka 15 akiongoza divisheni ya kaskazini ya Gaza
Marekani kimya wakati jengo refu lililokuwa likitumika na Aljazeera media lilishushwa na boma lakini hakuna taifa lolote la magharibi limelaani tukio hilo.
 
Back
Top Bottom