Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,798
- 31,811
Utangulizi
Wapenzi wasomaji nimekuta ujumbe huu katika group moja katika Whatsapp na nimeupenda. Nimeona niuweke hapa kwa faida yetu sote. Ndani ya ujumbe huu kuna mengi ya kuzingatia na pia kushukuru kuwa leo tunaweza tukawakumbuka masultani waliotawala Zanzibar kwa kheri na kisha tukawaombe dua kwa Allah.
Maziko ya Sultan Sayyid Khalifa bin Haroub
Haya ni mazishi ya Mfalme wa Zanzibar Sayyid Khalifa bin Haroub Albusaidy aliyefariki 1960 alitawala muda wa miaka 49 ilibakia mwaka mmoja tu afanyiwe Diamond Jubilee.
Alikuwa Mfalme mpole mwenye huruma akiwapenda sana wananchi wake akiwatembelea kwa miguu na akiwahi kuwaamkia kabla yeye hajaamkiwa akipita pahala watu wote husimama kwa kumlahiki kwa furaha kubwa wakati anasalimiana nao.
Alipokuwa Uingereza aliulizwa, "Je nchini kwako kuna siasa za vyama vingi vinavyoshindana si huenda wale wakagombana wasiwafikiane?
Akajibu, "Habana hawa ni ndugu hawagombani wanazungumza tu maendeleo ya nchi yao watawafikiana."
Alikuwa hapendi ugomvi wala mivutano, alipenda kuona watu wake wanaishi kwa raha.
Siku za Maulidi ya Mtume SAW watu wa Maulidi ya Home na dhikri wa mashamba wakifika Forodhani Sultan Palace wakimsomea maulidi na dhikri na yeye akiwapikia biriani nzuri sana na sharbati ikisha akishuka na marashi akitia marashi kwa mkono wake kisha akiwatunza pesa na Ahli dhikri na Ahlul Maulidi wakifurahi kwa taadhima na heshima hiyo kubwa wanayopewa na Sayyid Sultan.
Allah amuweke peponi pamoja na Mtume wetu Muhammad SAW na Allah atupe baraka zake na madad yake na Allah aijalie Zanzibar iwe nchi ya amani upendo huruma na mshikamano baina ya wananchi wake na viongozi wao Amin Amin.