Wapo wengi ila wanatofautiana kwa jambo moja au jingine na nyerere lakini wanaweza wasiwe kwenye nafasi za kisiasa kwa sasa kwa sababu nyingi kwani hata Nyerere angeikuta TZ kama ilivyo leo angeweza asijihangaishe na siasa bali angefanya mambo mengine research au kuwa mwanaharakati Fulani et.c. kati ya makundi hayo ndiyo mtafuteni Nyerere wa leo siyo kule kwenye vyama, labda chama kimoja tu ingawa hatuna uhakika kama ni maneno tu au hata moyoni ndiyo walivyo lakini wafuatao wanafanana fanana naye kwa vitu kimoja au viwili lakini siyo fully yaani, intellect, integrity, patriotism, courage, selflessness et.c. . Tundu Lisu, Zito, Deo Kibamba, Issa Shivji, Jenerali Ulimwengu, Juma Mwapachu Slaa, Mbatia, na watu Fulani Fulani huwa wanaongea Star TV kuna mwalimu anaitwa Chacha Ngaisery, Lwaitama n.k sehemu kubwa naamini wako kati ya watafiti, waandishi na wanaharakati ila hawajulikani na hawajikwezi sawa na yeye alivyokuwa. Kumbukeni Pugu watu wa TAA walimfuata hakujipeleka, ila wa siku hizi sijui labda ndiyo wito. Ila wako wanaofana naye kwa rangi ya nywele na ngozi wengine alivyokuwa kijana wengine alivyokuwa mtu mzima hao hatuwahitaji wanafanana kama ajali tu.