Kiongozi lazima akaze sauti vitani

prucho

Member
Jul 22, 2016
39
94
LAZIMA KIONGOZI AKAZE SAUTI KWENYE MAPAMBANO.

HONGERA RAIS JPM.

Na,Mwl.Pasaka O. Rucho.
AFISA MTENDAJI KATA YA TAI RORYA.

Leo tarehe 03/05/2020 nilikuwa nafatilia hotuba bora kabisa wakati huu wa janga hili la CORONA iliyotolewa na mh.Rais Magufuli akiwa anamwapisha Comrade Mwigulu Lameck Nchemba kuwa waziri wa katiba na sheria.
Hotuba hii kwa watu wanaofikiria vizuri ndio hotuba inayotolewa na majemedari wengi wanapokuwa vitani, (never give up in a battle field).

Rais wewe ni Jiwe kweli ukikisoma kitabu cha THE CONCISE 48 LAWS OF POWER kilichoandikwa na Robert Green.
Sheria ya 15 miongoni mwa hizo 48 inasema "Crush your enemy totally".

Sheria hii haituhitaji kufanya mjadala na adui yetu na kumpa nguvu kubwa ya kutumiliki sisi, ukishakuwa Kiongozi lazima uongeze juhudi ya kupambana na adui yako.

(Leo hii adui yetu ni CORONA) Je ni sahihi nchi yote tukajifungia ndani,tumuache nani nje asiye na damu( kwani polisi, manesi, madaktari na viongozi wengine wa serikali )wenyewe hawana damu???.

Kuna wabunge ambao tena ni wakilishi wetu wamejifungia kwenye vyumba vyao kwa lugha ya kujiweka carantin kwa siku 14, huu ni uzembe kazini, nchi yote tukiwa lock down nani atamuhudumia mwingine.

Chadema 2016 mlitoka bungeni mmefunga BARAKOA, Kkwanini msizitumie tena kwa kipindi hiki pale bungeni?

Robert Green anasema....all great leaders since moses have known that a feared enemy must be crushed completely(sometimes they have learned this in hard way).

Lazima wote tuingie vitani na kutoa kauli za kijasiri za kututia moyo kama alizozitoa leo mh.Rais.

Tukizubaaa Robert Greene anasema the enemy will recovery and will seek revenge, crush him not only in body but in spirit.

Mtu yeyote anayeonekana kuonesha kututisha sana katika janga hili ni adui yetu lazima tumnyime kodi zetu anazotaka kuchukua kama mishahara na posho zake.

Mh.Rais hawa maadui walimsumbua hata MUSA na Harun, kipindi aliwatuma kwenda kuangalia nchi kaanani, majibu waliyoyarudisha yalikuwa ni mabaya na kuvunja moyo (huko kuna majitu makubwa na ya ajabu)

Ila Yoshua alikuja akawatuliza watu na kuwaambia ile ndo nchi ya ahadi.
Mh.Rais hiki alichokifanya Yoshua ndicho ulichokifanya leo kama mfariji mkuu umetoa trend ya ugonjwa na kusisitiza kuwa upo ila TUSITISHANE, Wanaandika mambo mengi ya kutuogopesha lakini lazima tukubali kusimama pamoja na imara zaidi kuungana kupambana na adui yetu huyu.

Kwa maombi na sala nyingi.
Mitandao imeonesha kuwa nchi nyingi zimeanza kukataa vile vipimo ambavyo vimepata Korona kwenye papai, ila kuna baadhi ya maadui zetu hawajaelewa

Nitumie tuu wino huu kipindi naelekea Mwisho kumpongeza Rais kwa ujasiri mkubwa usiyo na mawaa wala hofu katika kipindi hiki.

Chapa kazi, na hatutakuangusha.

Tuendelee kumwomba Mungu kwa imani zetu CORONA lazima iendeeeeee.
 
Hivi ukienda ocean road ukamuambia mgonjwa wa kansa dah huu ugonjwa ni hatari na hauponi, hapa ni kifo.. unakuwa umemsaidia au ndio unazidi kummaliza kinga yake?

Ukiangalia wanaoongea sana kwenye covid19 na kutoa vitisho ni vijana wa chadema chini ya viongozi wao na dada yao mange.

Viongozi wanaoona mbali wanaangalia namna bora ya kuwafanya watu waishi na hili gonjwa katika njia salama. Maana halijulikani litaisha lini. Hata ukifungia watu ndani siku ukiwaachia wataambukizana tena. Tena kwa kiwango kikubwa maana watajihisi wote ni wazima wakati wengine ni cariers.

Lakini ukitoka utakuta na waajiri hawapo, wakulima hawapo, madaktari nao walijiweka lockdown, askari hawapo.

Tutaanza kulilia njaa na ajira.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom