Kiongozi gani wa juu muongo kupitiliza? Wangu ni huyu...

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,115
Sisi binadamu kwa asili ni waongo!! Na kwa mwenyezi Mungu uongo ni dhambi. Tunapaswa kuishinda hii dhambi ya uongo! Lakini mara nying watu husema uongo kwa mtu mmoja mmoja na sio kwa jamii nzima. Na uongo uliozoeleka kwa sasa ni kudanganya ulipo kwa mtu aliye mbali nawe. Tuombe Mungu kwa hili atuepushie tulishinde.

Lakn katika maisha ya kawaida katika jamii tuna watu ambao husifika kwa uongo! Ina maana hao huongea uongo uliopitiliza. Mfano kuna rafiki yangu mmoja alikua mwongo hadi alikua anaboa. Sasa safari hii alikua anamdanganya mchumba wake wa kike had wakaachana.alikua na mchumba msom aliye amua kuwa hakimu. Sasa jamaa wakati anamdet alijitangaza kwamba naye ni msomi wa kiwango cha juu mpaka amefikia ngazi ya uhandisi. Huku aliishia la saba, (sio dhambi kuishia la saba). Na masomo yake mengine kasomea nchi za ng'ambo ikiwemo china. Huku kusafiri kwame koooooote kaishia kongo huku akiwa kondacta wa roli!!!.

Sasa alikua anamshangaza sana mchumba wake kwa kumkataza pale anaponogesha maongez yao kwa kuchomekea kizungu. Jamaa alikua mkali kweli kwa mchumba wake asitumie kizungu maana kati yao hakuna mzungu kwanini achanganye kizungu wakati hamna mzungu!. Huku akimpiga mkwala mchumba wake kwamba yeye ni bingwa wa kichina, vip na yeye akiamua kunogesha na maneno ya kichina?? Lakn mkwala huo ilikua ni kuogopa kuumbuka pale na yeye atakapotaka kuchanganya na lugha ya malkia atajikuta ni mwendo wa kiswangilishi! Sasa akipiga mkwala anatupia maneno ya uongo na ukweli ya kichina feki . Si unajua kichina ni rais kuongea kwa mtu asiye kijua ili mrad unamalizia na ng. Ching chong pyong yong n.k. Waliishia kuachana maana karibia kila kitu jamaa alikua anamdanganya mwanamke.

Sasa twende kwa viongoz wetu waliopita na waliopo. Wawe wa upinzani au chama tawala. Huwa wanatudanganya sana . Ni wakati mwafaka kuwaweka hapa na kuweka maneno yao ya uongo. Hii itafanya wajue wananchi tunawafatilia kwa karibu sana matamshi yao, hivyo wanapaswa kuwa makini wanapotamka.

Kwangu mimi mtu pekee ambaye hunishangaza sana na aina ya uongoz wake na maneno yake ni rais wangu wa sasa. Aisee naweza kusema ni mwongo sijapata ona kiongoz mwongo kama huyu tangu nipate akili. Tena ni kwa muda mfupi sana: sijui akifikisha miaka mitano nitakua nimesikia kauli ngapi toka kwake zilizo jaa upotoshaji wa makusudi.

Naweka kauli zake chache zilizokua zimejaa uongo mkubwa ila aliongea huku akiwa na amani usoni ila sijui moyoni.

Hakuna serikali duniani iliyowahi kuwajengea waathirika wa maafa yeyote duniani. Na mimi serikali yangu haiwejengei! Huku anamalizia kwa kusema msema kweli mpenz wa Mungu. Je hili lina ukweli??

Ujenzi wa reli ya mwendokasi unajengwa kwa hela ya ndani na hela ipo . Baada ya siku mbili anaomba msaada na mikopo kwa viongoz waliomtembelea kwa ujenzi wa reli hiyo hiyo! Baadaye tena anaongea na wananchi wale wale kwa kulalamika . Wezi hawa wamesababisha tushindwe kujenga reli ya kwenda dodoma hadi tunaenda kukopa wakati tuna mahela mengi kwenye dhahabu.

Na hupenda walio chini yake waseme mambo makubwa makubwa ili kumkweza . Na hii tabia hutumika sana kwa mtu mpenda sifa zisizo na msingi. Yaan angetamani kila mtu amsifie. Kwangu mimi ndiye kiongozi pekee aliye na aina ya uongoz wenye kupenda sifa zisizo stahili ila huzilazimisha kwa kutumia hata lugha za uongo ili aonekane kiongoz bora kuwahi tokea tangu tupate uhuru.

Huyu ndio kiongoz mpotoshaji (mwongo) kupita wote niliowahi kuwasikia. Kwenye hotuba zake nyingi lazma umsikie akijikweza.

Yapo maneno meng sana kayaongea ila sina sababu ya kujifanya peke yangu ndio nimemsikia ni wakati wako na wewe kuweka kauli zake hapa. Au za wengine unaohisi kwako wewe ndio waongo kupitiliza.
 
Mkuu point yako inaeleweka toka kwenye kichwa cha habar. Tatzo umeandika mambo mengi na kuzunguka zunguka tu.
 
Muongo kweli katudanganya kafungua mladi wa maji sengerema toka aondoke hakuna cha maji
 
kuna mmoja huyo muongooo....lakini kuweka nomino yake hapa siwezii
 
Uongo ni UDHAIFU, sasa hapo unanichanganya maana wengi wanaamini huyu si dhaifu!!!!! Labda nitamuuliza yule mbunge anae tueleza nani na taasisi ipi ni dhaifu.
 
Hugo to a kipind cha kampeni wengine tulijua no a in a gani ya kiongozi...alipokuwa anataja raisi was Libya na Iraq...anapiga pushup hadharani...sema kwakuwa wapiga kura wengi ni mbumbumbu, walimchagua wakiamini no makosa madogo madogo na hii imekuwa Tabia ya watanzania wengi...ku-ignore vitu tukijiaminisha no mambo madogo madogo tu
 
Ghorofa moja Dsm milioni 500 Ghorofa moja la TRA chato milioni moja na nusu
 
Ajira mpya zitatolewa baada ya uhakiki! Sijui ni nani alitoa hiyo kauli!
 
Tunasubiri kila mtu Noah yake zitakazo nunuliwa na dhahabu iliyojaa Fuso za tani saba saba zaidi ya hamsini


Ingawa saa nyingine sio uongo wake bali ni ushamba uliopitliza ( wa kuropoka asichokijua)
 
Mapema Mh. Rais alipoanza kazi aliwavutia watanzania wengi pamoja na mimi kwa hotuba zake zenye kuonesha ana nia ya kweli ya kuwasaidia watz wanyonge.


Kwasababu nina desturi ya kutoamini maneno ila ninaamini katika historia na matendo ya mtu, nilichelea kumsifia niliona nisubiri nione angalau utendaji wake hata kidogo; nilichoshangaa ni kuwa anachosema mara nyingi kinakuwa sio.


Kwa mifano michache:


> Aliwatumbua wafanyakazi wa Bandarini kwa ufisadi ila kesi ilivyoenda mahakamani walishinda kesi; je,walionewa?


> Uhakiki wa watumishi alisema utafanyika kwa miezi miwili tu ila ulifanyika kwa miaka miwili, je, aliongea bila uhakika?


> Alisema alipoingia madarakani sukari ilikuwa inauzwa 5000/= ukweli ilikuwa inauzwa chini ya 2500/= je, alidanganywa na wasaidizi wake?


> Alisema hostel za UDSM zimejengwa kwa bil.10 tu ila ukaguzi wa CAG umeonesha imetumika bil.54. Je, ulimi uliteleza?

> Alisema tunaidai Acacia trilioni 400 na wamesema watatulipa ila mpaka sasa ni kizungumkuti. je, alidanganywa na kamati ya madini?

Sitaki niamini haraka kuwa alisema uongo ila nina wasiwasi na wasaidizi wake kuwa wanamharibia Rais wetu mpendwa kwani yeye mwenyewe hawezi kupanga kutudanganya wananchi kwani anajua fika kuwa raia wa sasa wanafuatilia sana na wanachunguza sana kila kinachosemwa na viongozi wao.


NB: Imeandikwa kwenye biblia kuwa ' shetani ni baba wa uongo' na wahenga walisema " msema kweli ni mpenzi wa Mungu"

By: Seme
 
Back
Top Bottom