Scarlet Pimpernel
JF-Expert Member
- Feb 22, 2017
- 576
- 402
Kiongozi ana maono (vision). Anaona picha kubwa (bigger picture) na maamuzi yake huwa yanaendana na picha kubwa pamoja na maono. Meneja anaona picha finyu na maamuzi yake yanaendana na picha finyu ambayao wakati mwingine hiyo picha haiendani na picha kubwa. Yaani kwa kiingereza kiongozi fights wars and a manager fights battles. To win a battle is not to win a war. Sometimes, strategically, you can lose battles in order to win wars.
Kwa mfano umepewa kazi ya Ukurugenzi Mkuu wa kampuni ambayo inafanya kazi vizuri kisasi kwenye soko na mauzo sio mabaya sana ila kuna wizi sana wa sukari wakati wakunywa chai asubuhi, pamoja na mafuta ya magari ya ofisi, matumizi ya magari ya ofisi kwenye shughuli binafsi na wafanyakazi wengine wanachelewa ofisini nakufika saa tatu.
Sasa wewe Mkuregenzi mpya unaingia na mbwembwe unafuatilia wanywa chai asubuhi. Unawakamata kweli wano kunywa chai sana na kuiba sukari. Safi. Wachelewaji nao unawakomesha. Unawahi ofisini, unawavizia, unaamka usiku naku shika watumiaji magari wa kampuni kwenye ma-bar maarufu. Unatumia nguvu kweli. Unawafukuza kazi. Watu wanatia adabu. Unafanya kwa mbwembwe watu wanakushangilia ni mchapa kazi lakini unasahau "bigger picture". Kazi yako kubwa ni kuongeza mauzo ya bidhaa za kampuni - profits. Kupunguza matumizi ya shukari ni sawa, kuweka discipline kwenye matumizi ya magari ni sawa lakini yote hayo hayana maana kama mauzo yanapungua. Sasa kwa sababu umepoteza focus mauzo yanapungua lakini budget ya sukari na mafuta ya magari ni ndogo sana ukulinganisha na pesa zinazotoweka kwa kupungua kwa mauzo.
Unapandisha cheo wale wenye discipline ya unwaji chai na wasiotumia magari jumapili kumbe kuuza hawawezi. Kazi inawashinda na mauzo yanazidi kudidimia pamoja na kuwahi kwao ofisini na kunywa kikombe kimoja tu cha chai asubuhi. Wengine walikuwa wanapata mauzo au contracts huko bar. Sasa hawana usafiri na wengine umewatimua. Haukufanya uchunguzi wa kina. Ulikurupuka. Labda kuruhusu magari yatumike weekend ilikuwa na faida yake. Better to lose that battle but win the war (sales). Unaendesha zoezi kwa kibabe na wafanyakazi wazuri wengine nao wanahama kampuni, hawataki fedhea na mauzo yanazidi kushuka.
Sasa ni kweli kazi yako umefanya lakini umefanya sehemu ndogo sana ya kazi yako. Kiukwelli ni kwamba umefanya kazi ya meneja wako wa utawala na meneja wako wa usafirishaji. Ume-micromanage. Umekosa vison. Wewe umekuwa meneja na sio kiongozi.
Bodi ya wakurugenzi itakapo kupiga chini, utabaki unasema "this is a thankless job".