fakhbros
JF-Expert Member
- Sep 14, 2013
- 388
- 666
Pesa zilizotolewa kama Sadaka kwa waheshimiwa na Brother Ruge naamini kuna sehemu zilisaidia. Pesa hizo japo Leo mamlaka inadai zile ni pesa za haramu lakini mamlaka haisemi uharamu wa mshiko huo unatokana na kitu gani kama mahakama ndio ilimpatia umiliki halali brother Ruge baada yakuwepo mgongano kati ya kampuni yake na TANESCO na mahakama kumuona kuwa yeye ndie anaestahili kupatiwa kiasi hicho cha pesa kutoka katika ACOUNT ya Escrow.
Je mamlaka zimejipanga vipi endapo brother Ruge mahakama itamkuta hana hatia kwa kupewa umiliki wa pesa hizo kutoka katika ACCOUNT hiyo?
Je nikweli brother Ruge ni mtuhumiwa katika uso wa sheria au ni mtuhumiwa katika uso wa mamlaka?
Nimejitahidi kusoma magazeti yalioandika kuhusu Brother Ruge katika kipindi hiki anachotuhumiwa ni magazeti hayo hayo yalio muandika brother Ruge kwa kumsifia kipindi cha 2014.
Watanzania tumekuwa washabiki katika kila jambo linalo tokea ndani ya nchi yetu pasina kutafakari na kurejea matukio kwa mtazamo chanya.
Serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha inapambana na ufisadi tumeanza kuona matukio mengi yakifanywa na mamlaka katika mfumo wa tamthilia ambazo hazifiki mwisho na hata mtazamaji ambae ni mtanzania akiangalia hizi tamthiria anaona jinsi gani mamlaka inavyo jichongea kinyago kitakachogeuka Malikia pindi watuhumiwa watakapoishinda serikali mahakamani.
Natabiri kushindwa kwa serikali na brother Ruge
Natabiri ushindi kwa Yusuphu Maji
Natabiri ushindi kwa ACACIA hivi ni vinyango vitakavyo geuka Malikia pale nchi itakapo lazimika kuwalipa wahusika baada ya kesi zao kukosa ushahidi wenye kijitosheleza kuwatia katika hatia husika.