Kinshasa:Chimbuko la virusi vya HIV

Kinshasa:Chimbuko la virusi vya HIV

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,572
Reaction score
53,588
141003131746_hiv_kinshasa.jpg

Kinshasa mwaka 1955, janga la HIV lilikuwa linatesa mjini humu na kote nchini DRC hasa mkoa wa Katanga

Ugonjwa wa ukimwi uligunduliwa miaka ya 1920 mjini Kinshasa, nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo. Wanasayansi wameeleza.

Wanasayansi wa kimataifa wanasema ongezeko la watu,vitendo vya kukutana kimwili na shughuli za usafirishaji kwa njia ya reli zilifanya virusi vya ukimwi kuenea.

Ripoti inasema kuwa biashara ya ngono, ongezeko kubwa la watu na vitu vyenye ncha kali kama sindano kwenye zahanati huenda kulichangia kusambaa kwa ugonjwa huo DRC.

Wakati huo huo reli ilikuwa ina watu takriban milioni moja waliokuwa wakiingia na kutoka kwa wingi jijini Kinshasa kwa mwaka,wakisambaza virusi kwenda kwenye miji mingine.

Takriban watu milioni moja walikua wakitumia reli ya Kinshasa mwishoni mwa mwaka 1940.

Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga.

141003131747_chimp.jpg

Inaarifiwa virusi vya HIV ni sawa na virusi vya Sinium vinavyopatikana katika Sokwe

Ukimwi ulitambulika kuwa janga kimataifa mwaka 1980 na uliathiri takriban watu milioni 75.

Ugonjwa huu una historia ndefu barani Afrika , lakini ulipotokea ugonjwa huu bado ni mjadala mrefu.
Timu ya wanasayansi kutoka chuo cha Oxford na chuo cha Leuven, nchini ubelgiji walitafiti chanzo cha ugonjwa wa ukimwi wakisema kuwa ulianzia kwa Sokwe.

Virusi vya HIV ni sawa na virusi vinavyopatikana kwa Sokwe ambavyo vinajulilkana kama Simian ambavyo vinadhaniwa vilitoka kwa Sokwe na kuambukizwa binadamu kupitia kwa damu wakati wakitafuta nyama ya wanyamapori.

Virusi hivyo vilikuwa na muundo tofauti na muundo huo ulikuwa unabadilika kila wakati. Virusi vya kwanza viliwaathiri maelfu ya watu nchini Cameroon.

Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga.

141003131747_hiv.gif

Virusi vya HIV

Idadi kubwa ya wanaume waliokuwa wanafanya kazi mijini na idadi ya wanaume ndio ilikuwa kubwa kuliko wanawake na hivyo biashara ya ngono ikawa kubwa sana.

Mmoja wa watafiti Profesa Pybus anasema kuwa mambo mawili yanesaidia kupunguza maambukizi. Kwanza hamasisho la serikali kuwatibu wagonjwa kwa maradhi tegemezi.

Jambo la pili ingekuwa mfumo wa usafiri ambao uliwawezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine huku ugonjwa ukienezwa zaidi.

Takriban watu milioni moja walikua wakitumia reli ya Kinshasa mwishoni mwa mwaka 1940.

Virusi vielendelera kuenezwa kwa nchi jirani ya Brazzaville na mkoa wenye madini wa Katanga ambao ulikuwa kitovu cha ugonjwa huo.

Virusi havikukomea tu nchini Congo bali vilianza kuenezwa kote duniani

Source: BBC Swahili

Kinshasa:Chimbuko la virusi vya HIV - BBC Swahili

Sasa inakuwaje Kenya na Afrika ya Kusini zinaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wenye virusi vya HIV na nchi za Congo Brazaville na CONGO DRC zina wagonjwa pungufu sana ukiliganisha na nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika?

Inabidi Jamiiforums iwaulize maswali mgumu hawa BBC.
 
Swali lako hilo linakosa mantiki maana hata Ebola inawamaliza Liberia na ivory Coast wakati imewakuta tu juzi na sio chimbuko yake.
 
Viral diseases are self limiting, Congolese might have acquired immunity against the virus.
 
Tanzania yetu mkoani iringa na njombe hali inatisha sana. ukijikwaa tu umeumia, jambo la ajabu wanafunzi {wakike} wa vyuo kama TUMAINI, RUCO, MKWAWA,CDTI wakifika iringa kutoka mikoani wanafanya umalaya wa kutupwa, wanabeba gonjwa wanasambaza kwao.

jamani tujihadhari na vvu.
 
Huu ni utumwa wa akili,na ugonjwa mkubwa sana.Kila gonjwa bovu,mnasingizia Afrika,Njaa-Afrika,Vita-Afrika,Utapeli-Afrika,Uzembe-Afrika???Je humuoni kwamba hii ni vita vya adui kutuangamiza?Huyu nyani maskini ambaye naye ni Kama Afrika,kila ugonjwa anasingiziwa nyani,natamani sana angeweza kwenda mahakani akashtaki.Tunamuonea sana na tunamsingizia uongo mara zote.Wa-Afrka amkeni usingizini.Ugonjwa wa ukimwi ulipogundulika,walisingizia Nyani na kwamba umeanzia Afrika,lakini ukweli ni kwamba aliyetengeneza ni mwanasayansi Robert Gallo.Robert Gallo - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Hiki ndicho nilichofikiria niliposoma hii habari toka BBC wiki iliyopita. Huu ugonjwa umeanzia Marekani ila hawawezi kukubali hili janga wameleta wao. Kama nyani wana virusi ambavyo wanaweza kuvihimili, kwanini wasitafute dawa kutoka kwa nyani hao. Mimi sidhani kama kuna uhusiano wa virusi vya nyani na vvu bali ni namna tu ya kutaka kutafuta njia ya kulisingizia bara la Afrika. Kinachojuliakana ni kwamba ugonjwa ulianza kutambulika Marekani miaka ya 1980 na ulikuwa unawapata mashoga sana.
 
Swali lako hilo linakosa mantiki maana hata Ebola inawamaliza Liberia na ivory Coast wakati imewakuta tu juzi na sio chimbuko yake.

Mantiki inayo coz had iwe ivo kuna sabbbu znazofanya Kenya kuwa na idadi kubwa au Africa kusini sababu gan unappswa ujibu kama ujui tulia
 
Swali lako hilo linakosa mantiki maana hata Ebola inawamaliza Liberia na ivory Coast wakati imewakuta tu juzi na sio chimbuko yake.

[h=3]HIV prevalence in selected countries across sub-Saharan Africa in 2012[/h][TABLE="align: center"]
[TR]
[TH]Country[/TH]
[TH] [/TH]
[TH]HIV Prevalence (%)[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="class: row_title, colspan: 4"]Southern Africa:[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]South Africa[/TD]
[TD="colspan: 2"]17.9[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Botswana[/TD]
[TD="colspan: 2"]23[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Swaziland[/TD]
[TD="colspan: 2"]26.5[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: row_title, colspan: 4"]West Africa:[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Senegal[/TD]
[TD="colspan: 2"]0.5[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Cameroon[/TD]
[TD="colspan: 2"]4.5[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Nigeria[/TD]
[TD="colspan: 2"]3.1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: row_title, colspan: 4"]East Africa:[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Kenya[/TD]
[TD="colspan: 2"]6.1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Uganda[/TD]
[TD="colspan: 2"]7.2[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Tanzania[/TD]
[TD="colspan: 2"]5.1[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Our History of HIV and AIDS in Africa page details how HIV prevalence has changed over time.
- See more at: HIV and AIDS in sub-Saharan Africa | AVERT

Lawmaina,
Ikiwa HIV-AIDS imekuwako kuanza miaka hiyo ya 1950 huko Congo DRC na Congo Brazza lakini Afrika Mashariki, Magharbi na Kusini ni miaka ya 1980 , swali bado tujiulize ktk nchi tano zenye wagonjwa wengi mbona Congo hizo mbili hazipo?
 
Ni kampeni ya mashoga na watetezi wao na wapenda kuyatumia mashirika ya habari kama BBC nk.
MASHOGA WOTE WASHINDWEEE !!!
 
Hawa bbc kuweni nao makini sana,,,! maana ukweli kuhusu ni wapi ukimwi ulipoazia na ulipotengezwa wanaujua.
kwa sasa wanaendelea kutuletea porojo tu.
 
Huku ni kutuharibia uchumi kwa uongo wao ili tuendelee kuwa omba omba miaka yote.Kwani wanawaogopesha wawekezaji wa maana,wanawaogopesha watalii,wanaharibu mauzo ya bidhaa ya Afrika kwani watu wanaogopa kununua,na wanatutangazia mabaya.Tuweni macho.Angalia ebola soma hapa:
USA created Ebola virus as biological weapon? - English pravda.ru

mkuu hawa bbc, ukweli wanaujua kabsa kuwa ni wapi?? ukimwi ulitengenezwa.

nigekuwa nauwezo wa kuwa kiongozi wa east africa nigefunga kabsa matangazo yao bbc yasiwe yanaruka katka ukanda wetu.
 
Back
Top Bottom