Kinjekitile Ngombale Mwiru: Haiingii akilini kila mwenye tuhuma na kashfa akimbilie upinzani

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Mwanaharakati Kinje Ngombare Mwiru, amezungumza mtazamo wake kuhusiana na sakata zima la msanii Wema Sepetu kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Amesema kitendo cha CHADEMA kumpokea Wema kinaonyesha dhahiri kwamba Vyama vya Upinzani vimeanza kupoteza mwelekeo kisiasa na vinashindwa kupambana na Chama cha Mapinduzi(CCM) ambacho kinashughulika na mambo mbalimbali yanayowakabili wananchi

"Haiingii akilini kila mwenye tuhuma na kashfa akimbilie upinzani. Huo ni udhaifu mkubwa unaofanywa na viongozi wa vyama hivyo, wameshindwa hoja za msingi kupambana na CCM sasa wanajisifu na kujigamba kwa kuwakaribisha watu watuhumiwa", alisema Kinje

Aliongeza kwa kusema ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona hata alipoingia Edward Lowassa CHADEMA , Chama hicho kilikosa hoja na ndipo kilipoanza kupoteza mwelekeo na matokeo yake yanaonekana katika uchaguzi ambapo CCM ilipata ushindi mkubwa

Kitendo cha CHADEMA , kupokea wanachama wenye tuhuma mbaya ni dhahiri inaonesha chama hicho kimepoteza uelekeo na kukwamisha vyama vya upinzani

Alimaliza kwa kusema wananchi wanapatwa na wasiwasi juu wanasiasa ambao ni watuhumiwa wa dawa za kulevya kuwepo kwao kwenye siasa ni kama maficho ya uharifu.

Chanzo: Dar24
 
Mwanaharakati Kunje Ngombare Mwiru, amezungumza mtazamo wake kuhusiana na sakata zima la msanii Wema Sepetu kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Amesema kitendo cha CHADEMA kumpokea Wema kinaonyesha dhahiri kwamba Vyama vya Upinzani vimeanza kupoteza mwelekeo kisiasa na vinashindwa kupambana na Chama cha Mapinduzi(CCM) ambacho kinashughulika na mambo mbalimbali yanayowakabili wananchi

"Haiingii akilini kila mwenye tuhuma na kashfa akimbilie upinzani. Huo ni udhaifu mkubwa unaofanywa na viongozi wa vyama hivyo, wameshindwa hoja za msingi kupambana na CCM sasa wanajisifu na kujigamba kwa kuwakaribisha watu watuhumiwa", alisema Kunje

Aliongeza kwa kusema ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona hata alipoingia Edward Lowassa CHADEMA , Chama hicho kilikosa hoja na ndipo kilipoanza kupoteza mwelekeo na matokeo yake yanaonekana katika uchaguzi ambapo CCM ilipata ushindi mkubwa

Kitendo cha CHADEMA , kupokea wanachama wenye tuhuma mbaya ni dhahiri inaonesha chama hicho kimepoteza uelekeo na kukwamisha vyama vya upinzani

Alimaliza kwa kusema wananchi wanapatwa na wasiwasi juu wanasiasa ambao ni watuhumiwa wa dawa za kulevya kuwepo kwao kwenye siasa ni kama maficho ya uharifu.

Chanzo: Dar24
Soma sifa za kujiunga na chama ndo uandike kile ulichokiandika sio kukurupuka ili upendwe na CCM. Wenye macho na akili za kuelewa kinachoendelea ndani ya CCM walishaihacha long time.
 
Ndio siasa zetu hizo, kama comedy, eti tunaangalia mtu anawafuasi wangapi kutoka mitandao ya kijamii, haya kuweni makini hata kaoge ana followers na wafuasi kibao kwenye mitandao ya jamii.
 
Huyu ndo rafiki yake Daudi Bashite aliogopa kumtaja kuwa anahusika kuuza madawa ya kulevya kwa sababu mtu wake wa karibu.
Kuhusu tuhuma za madawa ya kulevya zinazomkabili Wema Sepetu hoja hii pia ni mufilisi kwa sababu tuhuma hazimfanyi mtu kuwa na hatia. Wema sio mtu wa kwanza kujiunga na Chadema akiwa na tuhuma mahakamani. Wapo wengi. DC Kimolo alipoamua kuacha ukuu wa wilaya na kujiunga Chadema alipewa tuhuma za kunyang'anya ardhi wananchi enzi za uDC wake, lakini bado tulimpokea. However viongozi karibu wote wa Chadema wana tuhuma mahakamani. Sasa je nao tuwanyang'anye uanachama hadi kesi zao ziishe?
 
Kuna watu vichaa. Nenda kwanza kasome katiba za vyama vya siasa, chama cha siasa kinaongozwa na katiba na si matakwa ya mtu kama anavyotaka huyo kije. Naomba aseme ni kifungu gani cha katiba hao uliowataja wamevunja kujiunga chadema.?
 
Chenji ya miamoja ni sh.kumi sasa tangu lini hii tisini ikamtenga sh.kumi wanaunga mkono kauli wao ndo sh.tisini ya makonda wanapinga kauli ndo sh. tisini ya chadema
 
Back
Top Bottom