Kingunge Ngombale nae amshukuru MUNGU

Kingunge Ngombale nae amshukuru MUNGU

Umeeleza uchawi ni nini ila bado sijaelewa nguvu ya uchawi hutoka wapi?

Uchawi ni maarifa mkuu, yeyote anaweza kujifunza na watu fulani huzaliwa na huo uwezo. Kutumia hizo nguvu kwa ubaya ndio uchawi haswaa, ni sawa na bunduki kuua na kulinda kwa wakati mmoja.

Nitakuwa nakosea nikisema uchawi hutoka kwa mungu?
 
Wala huhitaji kusoma vitabu. Unaweza kuona live kwa wanaozifuata dini hizo. Labda uniambie kuwa Wamasai sio Waafrika ama Wandorobo wao hawamo. Makundi haya kwa sehemu kubwa bado yanafuata dini za Kiafrika. Usitafute vitabu tena vya watu (maaskofu) ambao kwa maoni yako wameathiriwa na dini za Mashariki ya Kati wakati ambapo mwenyewe unaweza kuwaona wanaofuata dini hizo unazozisifu.

Wewe unaelezea ulichokisoma, wenzako tunakuambia tulichokifanya chini ya hizo dini za Kiafrika. Usipotoshe!

Nikupotoshe kwa faida ya nani, mimi ni Mwafrika na nimeishi maisha ya Kiimani miaka yangu yote. Uafrika si lazima uuishi katika mapori, kuna makabila huwa yanafanya ziara kwao kutambika, ni ibada kwa Mungu wao na mizimu, ambayo inatuangalia kwa niiaba ya Mungu na kutuweka sawa tunapokosea.

Nimetoa mifano ya maandiko kwa kuwa mwombaji anapotoshwa akasome kazi ya fasihi ili aelewe Uafrika, fasihi ambayo inapotosha Uafrika. Mbiti na Tempels ni wanafalsafa, licha ya kuwa ni maaskofu. Siwarejei kwa Uaskofu wao, bali kwa uanataaluma wao.
 
Uchawi ni maarifa mkuu, yeyote anaweza kujifunza na watu fulani huzaliwa na huo uwezo. Kutumia hizo nguvu kwa ubaya ndio uchawi haswaa, ni sawa na bunduki kuua na kulinda kwa wakati mmoja.

Nitakuwa nakosea nikisema uchawi hutoka kwa mungu?

Uchawi ni maarifa mkuu, yeyote anaweza kujifunza na watu fulani huzaliwa na huo uwezo. Kutumia hizo nguvu kwa ubaya ndio uchawi haswaa, ni sawa na bunduki kuua na kulinda kwa wakati mmoja.

Nitakuwa nakosea nikisema uchawi hutoka kwa mungu?

Unaposema kutumia hizo nguvu kwa ubaya ndiyo uchawi wenyewe haswa maana yake ni kwamba uchawi kama uchawi ni kitu kisichofaa.
 
kwani aliesema kuwa kingunge haamini mungu ni nani, yule mzee anaamini mungu ila sio kwanamna au jinsi ambayo nyinnyi mlio na dini zenu za kutoka nje mnaamini. Kingunge ni true African ambaye imani yake iko kiafrica zaidi, anaamini walichokuwa wakiamini baba zake, babu wa enzi hizo.

Hayo yalisemwa na aliye kuwa mjumbe wa Bunge maalumu la Katiba akiwakilisha upande wa dini Shekh Jongo.
"Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kasema kuwa kukamilika kwa mchakato wa katiba inayopendekezwa kwakweli ni suala la kumshukuru MUNGU"

Watu walicheka sana.
 
Mkuu unajichanganya sana,ila labda ibada za dini za afrika ni zipi?

Wapi nimejichanganya? Tatizo ni jinamizi lililo kichwani mwako kuwa uchawi ni ubaya tu. Mbinu za mganga mponyaji na mchawi zinafanana, tofauti ni malengo tu. Ndio maana nasema ile ni teknolojia ya kutenda yaso kawaida, matumizi ndio huamua ubaya.

Sherehe zetu zipo za aina nyingi, zipo za daily basis na zinazoendana na matukio. Za matukio ni kama matambiko, shughuli za jando, sherehe za 'passage' kama kumtoa mtoto nje, kuingia utu uzima na kadhalika.

Huwa zinatofautiana kulingana na jamii.
 
Unajichanganya unaposema miujiza ikitumika vibaya ndiyo uchawi,hebu rudia tafsiri ya neno uchawi uliyonipa mwanzo halafu linganisha na kauli hiyo ya miuji ikitumika vibaya ndiyo uchawi.

Nimeuliza ibada sio sherehe,halafu tofauti ya dini za kiafrika na tamaduni za kiafrika ni ipi?
 
Nilivyoelewa mimi ni kuwa mzee haamini katika Mungu na hana Dini lakini kuhusu katiba kamshukuru MUNGU
Huyu Mzee inasemekana alibatizwa kanisa Katoliki kwa jina la Kayetani, ubatizo haufutiki,
 
..kazi ipo!!

..amemshukuru MUNGU baada ya kufanikiwa kwa zoezi lao la kuchakachua kura za wa-Znz.
 
Unajichanganya unaposema miujiza ikitumika vibaya ndiyo uchawi,hebu rudia tafsiri ya neno uchawi uliyonipa mwanzo halafu linganisha na kauli hiyo ya miuji ikitumika vibaya ndiyo uchawi.

Nimeuliza ibada sio sherehe,halafu tofauti ya dini za kiafrika na tamaduni za kiafrika ni ipi?

Sikukaririshi, najaribu kukufanya uelewe. Kurudia tafsiri yangu ya awali kutafanya kazi yangu iwe ni kukukaririsha fasili. Uchawi ni uwezo wa kutenda yasiyo ya kawaida, ambayo nasikia hata Yesu alitenda. 'Uchawi' wa uchawi unaamuliwa na malengo yake, maana hapa ni kuwa, mwenye uwezo huo akiutumia kudhuru, ndio mchawi.

Ibada ni mawasiliano kati ya binadamu na Miungu, katika sherehe za Kiafrika huwa kuna sala/maombi. Mathalani sherehe ya kumsimika kijana huwa inaambatana na maombi kwa mizimu, ya kuwa imlinde huyo kijana kama ambavyo imekuwa ikimlinda siku zote za maisha yake. Tayari tuna mawasiliano ya kimungu na roho za Miungu na watangulizi wetu, yatosha kuitwa ibada hiyo, sio?

Utamaduni ni namna ya kuishi ya watu, dini ni kipengele kilicho ndani ya utamaduni. Vingine vikiwa ni desturi (kawaida za kila siku, mavazi, chakula), mila (mambo yasobadilika kama taratibu za ndoa, tunu za jamii) , lugha na teknolojia.
 
Huyu Mzee inasemekana alibatizwa kanisa Katoliki kwa jina la Kayetani, ubatizo haufutiki,

Mkuu, ubatizo ni uhuni... Sanaa ya kukufanya uwe mteja wa Kanisa siku zote, wewe na uzao wako. Usipumbazwe na vitisho kama hivyo!
 
Ushauri
Hawa miungu wa kiafrika wana uwezo mdogo sana ndio maana sitaki hata kuwasikia. Walishindwa kutuzuia tusipelekwe utumwani na waarabu na wazungu, zikashindwa kumzuia "Mungu wa wazungu" tukawa koloni, zimeshindwa kuzia wizi wa rasilimali zetu zaidi ndizo zinawachukua wezi kuwalaza makaburini na kuwapa uongozi wa nchi. Hizi hatuzitaki na mwaka huu ndio mwisho wa viongoz wenye chale makalioni kutuongoza.

Mkuu hii pointi sikuiona jana, Mungu wa Afrika alishindwa ndio, lakini sio wa kwanza kushindwa mbele ya miungu wengine. Kuna Mungu wa Isrrael, huyu alishindwa na kuacha kizazi chake kikakaa utumwani miaka mia nne, miaka mia mbili zaidi yetu.

Alimshindwa Hittler, matokeo yake akaruka na watu milioni sita wa Taifa lake pendwa, alishindwa kwa milki za Ugiriki, Media, Persi na Rumi zikawa zinapokezana kutawala taifa lake kadiri walivyoona. Leo ameshindwa na Kikundi cha Wanamgambo, hadi leo wanachapana huko Mashariki ya Kati na watu wa Mungu hawalali usingizi... Zaidi ameshindwa hadi na Mungu wa Mashoga na Wasagaji, leo hii mji wa Tel Aviv unaitwa Makao Makuu ya Ushoga ndani ya Mashariki ya Kati

Usiwakosee heshima viongozi wako, maana hata Bilblia inakuonya kuhusu kuitii Mamlaka halali.
 
Sikukaririshi, najaribu kukufanya uelewe. Kurudia tafsiri yangu ya awali kutafanya kazi yangu iwe ni kukukaririsha fasili. Uchawi ni uwezo wa kutenda yasiyo ya kawaida, ambayo nasikia hata Yesu alitenda. 'Uchawi' wa uchawi unaamuliwa na malengo yake, maana hapa ni kuwa, mwenye uwezo huo akiutumia kudhuru, ndio mchawi.

Ibada ni mawasiliano kati ya binadamu na Miungu, katika sherehe za Kiafrika huwa kuna sala/maombi. Mathalani sherehe ya kumsimika kijana huwa inaambatana na maombi kwa mizimu, ya kuwa imlinde huyo kijana kama ambavyo imekuwa ikimlinda siku zote za maisha yake. Tayari tuna mawasiliano ya kimungu na roho za Miungu na watangulizi wetu, yatosha kuitwa ibada hiyo, sio?

Utamaduni ni namna ya kuishi ya watu, dini ni kipengele kilicho ndani ya utamaduni. Vingine vikiwa ni desturi (kawaida za kila siku, mavazi, chakula), mila (mambo yasobadilika kama taratibu za ndoa, tunu za jamii) , lugha na teknolojia.

Nilikuelewa vizuri na ndiyo maana nameweza kuona jinsi ulivyojinganya..mkuu naona sasa unaongea vitu kwa kutumia hisia zako wewe kama wewe,swala la kusema mchawi ni mtu mwenye kufanya uchawi wa kudhuru kwa maana ya kwamba mwenye kufanya uchawi usio dhuru sio mchawi hapa pananitatiza.
 
Hayo yalisemwa na aliye kuwa mjumbe wa Bunge maalumu la Katiba akiwakilisha upande wa dini Shekh Jongo.
"Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kasema kuwa kukamilika kwa mchakato wa katiba inayopendekezwa kwakweli ni suala la kumshukuru MUNGU"

Watu walicheka sana.

Kwi! Kweli huyu mmatumbi anachekesha. Si alikuwa 'Atheist' (Asiye Muumini) huyu mmatumbi, tena baada ya kuukana ukatoliki (kristo) uliomkuza na hata kuamua kubadili na jina juu dezaini staili ya Mabutu Seseko aliyekuwa Rais wa Zaire (DRC). Leo kilichombadilisha ni kipi? Hebu tujuzeni zaidi? Au Uzee ameona anaanza kuelekea kule ambako watu wakienda hawarudi🙂 teh teh
 
Nilikuelewa vizuri na ndiyo maana nameweza kuona jinsi ulivyojinganya..mkuu naona sasa unaongea vitu kwa kutumia hisia zako wewe kama wewe,swala la kusema mchawi ni mtu mwenye kufanya uchawi wa kudhuru kwa maana ya kwamba mwenye kufanya uchawi usio dhuru sio mchawi hapa pananitatiza.

Ulitaka nitumie hisia za nani, Wagiriki wa Karne ya kwanza walioandika Biblia au Warumi waliorasimisha ibada zao kua Ukristo, au za Waarabu ambao walianzisha Uislam ili kushinda ubabe wa Wazayuni waliokuwa wameteka falsafa za dini kwa wakati huo?

Mimi naona tutumie neno 'miujiza' ili tuwekane sawa. Huu ni uwezo wa kutenda yaso ya kawaida, sio? Uwezo huu unaweza kutumika kwa malengo chanya, kama inavyoaminika Yesu bin Mariamu alitumia kuponya watu, kulisha na kadhalika. Uwezo huu huu unaweza kutumika kwa malengo mabaya kama kuua, kupatiliza magonjwa, kusababisha ajali na kufitinisha, sio?

Matumizi haya mabaya ndio unaoitwa uchawi, ndio maana watu fulani wakaja na madai kuwa mchawi si lazima aroge, kitendo cha kumuonea mtu husuda, kunuia mabaya kwa wengine, kufitini na kadhalika huonwa kama uchawi (usio wa kimuujiza). Fikiria mtu mwenye roho mbaya kwa mwingine angepewa uwezo kama wa Bw. Yesu, si angeumiza watu?

Umenipata japo kidogo?
 
Kwi! Kweli huyu mmatumbi anachekesha. Si alikuwa 'Atheist' (Asiye Muumini) huyu mmatumbi, tena baada ya kuukana ukatoliki (kristo) uliomkuza na hata kuamua kubadili na jina juu dezaini staili ya Mabutu Seseko aliyekuwa Rais wa Zaire (DRC). Leo kilichombadilisha ni kipi? Hebu tujuzeni zaidi? Au Uzee ameona anaanza kuelekea kule ambako watu wakienda hawarudi🙂 teh teh

Kwa hiyo angebaki na huo Ukatoliki ndio angekuwa salama?
 
Back
Top Bottom