Dini za Kimagharibi na MAshariki ya kati zimewafumba watu macho na uwezo wao wa kuendelea kuisaka kweli. Uislamu na Ukristo vinapingana wazi na moja ni ushetani kwa nyingine lakini wanaonana wote ni wema ukilinganisha na dini zingine nje ya hizo.
Watu wanashindwa kutofautisha imani za Kiafrika na Upagani, upagani ni kutoamini uwepo wa Mungu, uwezekano mkubwa ni kuwa Kingunge sio mpagani, ni muumini wa Uafrika.
Dini za Kiafrika ni zipi zaidi ya ulozi?,kuruka na ungo? kata viongo vya albino na kuua vikongwe? Ni kipi zaidi ya ramli ni kipi zaidi ya wachaga kumwaga pombe damu na nyama kaburini asubuhi wakikuta hamna mbwa kala wanafurahi na kusema babu kala?
Ni zipi zaidi ya wamasai kutundika nyama mtini na kukeketa wanawake?
Ni zipi au ni mdundiko wa wazaramo ngoma inaanzia manzese inaishia mbagala ikiandaa maambukizi ya ukimwi na kuoza watoto? Mi bado sijakuelewa!!! au unamaanisha viongoz kulala makaburini kule kaole ili kushinda uchaguzi? au unajimu wa kimajini wa shkeh yahaya na wanaye?
Ni dini ipi ya Kiafrika? Mi bado sijaelewa au ile ya kichawi ya wambulu kuzuia mvua kichawi?
Ni ipi ya kutoa watoto kafara ili kupata madini mererani?
Nauliza tu bado ni ipi au ile ya wahanzabe ya kupeleka madume mawili ya nyani na debe mbili za asali kama mahari tosha kuoa?
Mi bado sijakufahamu au ile ya kutembea na nyoka nyani ya begi ni ipi?
Ipi hiyo au ni ile ukitaka kushinda uchaguzi au upande cheo unavua suruali unafyekwa chale makalioni au ni ile unaumwa kichwa unachanjwa chale tumboni?
Au ile ya kugombanisha majirani mwanao anaumwa maleria kali inayotaka qunini unaambiwa jirani yako kamloga?
Umeniacha na maswali maana nina masters ya African history lakini sijawai ona dini zaidi ya political and social systems and organizations. Zaidi ya hapo ni uchawi na ulozi tu kwa kinachoitwa African religion.
Labda nisikukatishe tamaa kuna ile ya Kinjekitile Ngwale badala ya kufundisha mbinu sahihi za vita alikupaka watu maji usoni eti risasi isipenye wakaangamia wote kwa bunduki ya kijerumani. Mi sijui dini ipi ya kiafrika.
Maana nilisoma mahali mtu mwenye haya mawazo yako ya kukariri bila kuuliza na kukusanya ushaidi usio na shaka aliandika "we had our own gods" nikacheka sana why should they be uncountable? kwanini wawe wengi hivi hao gods? why dont those gods choose one to head them? Sasa how should i manage to pray each of them?
Au ni wale wa riwaya ya things fall apart? mungu wa aridhi, anga nk. ambao nao wanataka kafara za watoto!! hawataki mapacha!! lkn mwaandishi akasema vizuri kabisa hii fiction yaani riwaya ya kutunga ila ikireflect jamii. Sasa utunzi hauwezi kuwa ushaidi. Sasa hii miungu yenu ndio inatupa mashaka ambayo yenyewe inataka upeleke kuku mweusi paka wa madoadoa mbuzi yuko hivi au vile!! Miungu ikiona haiwez kukusaidia kuloga mtu wa mwenye Yesu inakuambia leta machozi ya simba! utapata wapi?!!! leta mkojo wa kuku, kuku hana kikojoleo!!!
aaaah!! aaaah!!
Acha ulozi mgeukie bwana wa majeshi uiponye nafsi yako na wachawi kabla hawajakukafara.
Ushauri
Hawa miungu wa kiafrika wana uwezo mdogo sana ndio maana sitaki hata kuwasikia. Walishindwa kutuzuia tusipelekwe utumwani na waarabu na wazungu, zikashindwa kumzuia "Mungu wa wazungu" tukawa koloni, zimeshindwa kuzia wizi wa rasilimali zetu zaidi ndizo zinawachukua wezi kuwalaza makaburini na kuwapa uongozi wa nchi. Hizi hatuzitaki na mwaka huu ndio mwisho wa viongoz wenye chale makalioni kutuongoza.