Huyu mzee ndio wale watakao anguka kwenye majukwaa ya kisiasa kwa ajili ya kutaka umaarufu.
Nilianza kumsikia miaka ya 70 wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Tanga. Mpaka sasa nashidwa kumuelewa kama kweli ni mwanasiasa.
Aliwahi kupewa uwaziri kwenye serikali za maraisi watatu waliopita . Sijaona mchango wake. Akawa anapewa nafasi za uwaziri usiokuwa na wizara maalumu {only in Tanzania}.
Katika serikali hizo alizowahi kushika ndio zilizoua azimio la Arusha , na viongozi wake ndio walioamua kutofuata maadili ya viongozi na kujilimbikizia mali.
Kama angekua mwadilifu angekemea maovu na kujiweka pembeni , lakini huwa anavututiwa na vipost vya ajabu ajabu ,sasa hivi eti mjumbe wa wa bunge la katiba.
Hivi Watanzania watafaidika na nini kwa siasa zake .