Kingunge Ngombale Mwiru: Rushwa, makundi, ubinafsi vinaimaliza CCM na taifa letu.

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Akifungua mkutano wa uchaguzi wa CCM mkoa pwani amesema rushwa, uizi, ubinafsi na rushwa vinaitafuna CCM na Taifa kwa ujumla.

source:ITV
 
Akitoa nasaha kwenye Uchaguzi wa M/Kiti wa CCM - Mkoa wa Pwani, Mzee Kingunge Ngombare Mwiru amekiri kwamba Ubinafsi, Rushwa na uroho wa Madaraka ndo vitendo vinavokitafuna Chama Cha Mapinduzi.

ASANTE KWA KULISEMEA HILI.
 
mwanasiasa mkongwe nchini mzee kingunge gombare mwiru amesama kukithiri kwa rushwa na mgawanyiko wa makundi ndani ccm ni ishara ya uroho wa madaraka na manufaa binafsi badala ya wananchi kwa ujumla hivyo kusababisha ccm
kupoteza mwelekeo na hatimaye kupoteza imani kwa wananchi
hayo ameyasema leo alipokuwa akifungua mkutano wa chama hicho ngazi ya mkoa kwa ajili ya kumchagua mwenyekiti mpya wa mkoa huo.

source itv
 
kama analijiua hilo amefanya nini.....dawa ni kulitoa hili dubwana ccm madarakani...full stop
 
ccm imetumia mtaji wa udini hasa waislamu kuvuruga amani tuliyo nayo kwa kulazimisha kukaa madarakani,matokeo ya mbagala na kiongozi wanchi kikwete kushindwa kukkemea hadharani ni dalili tosha kuwa mheshimiwa anaunga mkono hayo matendo au anogopa kuwa watatoa siri za makubaliono hao waumini.kikwete ametumia ukanda kuvuruga ccm yake na hata taifa hii sio siri,na tutegemee mambo mawili kabla ya uchaguzi 2015 vita ya kisiasa hasa ccm na chadema na hii ni kutokana na serikali ya ccm kuzidiwa ngumu na hoja za chadema.lakini la pili ni vita ya dini ambayo anayesoma hii atanikumbkua kuwa ccm wako tayari waislamu na wakristo watwangane kusudi wabaki madarakani,hivi kama si busara za viongozi wa kikristo na wao wakianza kulipa kisasi kweli kikwete utapita wapi kuelekea bagamoyo?lakini dalili zote zinaonyesha machafuko makubwa yanakuja kabla ya 2015 na hii ni sanbabu ya kikwete kuwa dhaifu wa kutokukemea maovu ya makundi ya wahuni wa dini moja mungu ibariki tanzania takbihi na haleluya visitugawanye na kikwete akimaliza muda wake ahojiwe kwa haya.
 
Mwaka 2005 wakati wa campaign kwa mara ya kwanza Tanzania tulishuhudia ubaguzi (discrimination). Dr Salim Ahmed Salim aliitwa mwarab, hizbu na mambo mengi ya hovyo. Labda nilipitiwa lakini kama kuna mtu aliyesikia kauli ya Kingunge naomba aturushie hapa. But we know, mitandao ndio ilikuwa inafanya kazi na Kingunge alichagua upande wa pili. Leo hii anapata wapi moral authority ya kukemea kitu alichopalilia, ama kwa kukaa kimya wakati kinaota mizizi, au kwa kuwapa support?
 
Mwaka 2005 wakati wa campaign kwa mara ya kwanza Tanzania tulishuhudia ubaguzi (discrimination). Dr Salim Ahmed Salim aliitwa mwarab, hizbu na mambo mengi ya hovyo. Labda nilipitiwa lakini kama kuna mtu aliyesikia kauli ya Kingunge naomba aturushie hapa. But we know, mitandao ndio ilikuwa inafanya kazi na Kingunge alichagua upande wa pili. Leo hii anapata wapi moral authority ya kukemea kitu alichopalilia, ama kwa kukaa kimya wakati kinaota mizizi, au kwa kuwapa support?
Mzee kingunge ni mnafiki wa Hali ya juu, yeye kahusika sana na mtandao wa dhaifu katika kumchafua dr. Salim , Leo ndio anagundua Makundi ni mabaya ccm, shame on him
 
Atuambie yeye mwenyewe yuko wapi. Yeye ndiyo babu wa rushwa na madhambi yote hayo. Hatujasahau alivyokuwa busy kukana kuwa hakuna EPA, na kusema hao watu ni wazushi tu, yako wapi sasa? Angekuwa mwungwana aseme kuwa alikosea kuwatetea manyang'au.
 
dawa ya jino ni kuling'oa ukiliziba ipo siku litakusumbua,sisiem nisawa na jino bovu linaitaji kung'olewa tusione aibu kuwa na mapengo.NI HELI KUISHI KAMA MBWA,UFE KIUNGWANA KULIKO UISHI KIUNGWANA UFE KAMA MBWA.
 
mzee mwenzangu kingunge nina swali moja tu.
Aliyelea na kupalilia siasa chafu ndani ya ccm ni nani kama sio wewe na wazee wenzio?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Kinachoitafuna ccm ni uridhishaji... Kikwete kaweka sana undugu kwenye chama mpaka inaboa... Its who u know kwenye ccm sio
 
Mzee anakaribia kufa? Mwizi na fisadi mkuu huyu pale Ubungo Terminal na Parking System Dar. Amepata wapi ujasiri wa kusema haya.
 
Sijawahi kumsikia huyu mzee akiongeaga point hata siku moja.....hivi hakunaga ward za wazee akafungiwe huko? Alivyochukua Ubungo Terminal na Parking za mjini......yeye haoni ni rushwa au wizi au ufisadi?
 
Kama analiona hilo tatizo yeye kama mzee ndani ya chama cha Majambazi anafanya nini kulitatua kama yeye siyo Jambazi kama wao
 
Back
Top Bottom