Kingine kinachomwangusha JK ni lugha!!


duh! You have made my day..
 

Lugha hizi alizozitumia Jakaya zisizoendana na matendo ndio zilizowapotosha Watanzania wengi kumchagua kwa vipindi vyote viwili,wacha wananchi wavune kile walichokipanda tena nnatamani sana hali iwe ngumu zaidi ya hii ili 2015 tuwe wote kwa lugha moja kuikataa ccm na mambo yake yote.
 
Nadhani kichwa kingesomeka kuwa Kinachomwangusha JK ni kauli mbiu zisizotekelezeka.Nilidhani ulimaanisha lugha ya kuongea,ambayo bado pia kwake ni tatizo.
 

Achilia mbali kuwadanganya watu kuhusu maisha bora kwa kila Mtanzania, lakini watu wengi wanadai walimchagua kwasababu ni handsome na angeonekana vizuri kwenye noti. Mibongo tunasafari ndeefu ya kuelekea mabadiriko
 

Unamaanisha Watanzania hupenda kuweka Matumaini yao kwa wanasiasa badala ya kuchapa kazi..?
Akija mwingine kutoka upande wa pili mtamtumaini?

Umeuliza swali la msingi sana hapa. Lakini ni muhimu kukubali kuwa siasa ina mchango mkubwa sana katika harakati za kuleta maendeleo ya mtu binafsi na maendeleo ya jumla. Hebu fikiria unapokuwa na nchi ambayo kipaumbele ni matumizi ya viongozi badala ya kuwekeza, madhara yake ni kudumaza shughuli mbalimbali za kukuza uchumi. Uwepo wa barabara bora, mabenki yenye nguvu, sera bora juu ya utoaji huduma muhimu kama leseni, hati ya umiliki, mgawanyo bora wa rasilimali za nchi, utawala bora (absence grand corruption) nk. Vitu hivi huchochea haraka maendeleo ya watu na nchi kwa ujumla.
 
....Ulikuwa ni usanii tu wa kuhakikisha anaingia Ikulu lakini hana hata chembe moja ya leadership quality hata ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi kumi achilia mbali kuwa Rais wa nchi.

Vp ule mgogoro wa kifamilia, ww umeweza kuusuluhisha ? mbona ww familia inakushinda kuongoza, tusemeje sasa ?:bange:

 

nafikiri akija tena maneno yake yatasomeka kinyumenyume ria yapm sika yapm na vungu yapm!!!

 
Katika kipindi cha Kikwete kaongeza wastani wa umri wa kuishi Mtanzania kutoka miaka 48 (au 50) wakati anachukuwa madaraka mpaka kufikia miaka 55. Au huoni kuwa hapo karibu kila mmoja kafaidika kwa maisha bora? Na hiyo ni kwa miaka 6 aliyopo madarakani, haijawahi chart ya wastani wa umri wa Mtanzania kupanda kama kipindi hiki cha Kikwete ni rekodi ambayo anaishikilia.
 
Ni kweli wa Tanzania tulipenda boom na sasa limetulipukia! Tujifunze kutokana na makosa!.
 

Hahahaha hizo takwimu alikupa daktari Jakaya au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…